JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,775
- 6,592
Zaidi ya wakimbizi, wahamiaji na waomba hifadhi 3,000 wamekufa au hawajulikani walipo kwa mwaka 2021 wakati wakijaribu kufika Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranean na Bahari ya Atlantic.
Hayo yamebainishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ripoti yake iliyotoka Aprili 29, 2022.
Ripoti hiyo inaonyesha idadi ya waliokufa ni kubwa katika miaka ya hivi karibuni.
Maelfu ya Waafrika wanatumia njia ndefu na hatari kufika Ulaya kila mwaka mara nyingi wakipitia Jangwa la Sahara na kuacha ufukwe wa Afrika Kaskazini wakiwa kwenye boti ndogo wakikimbia hali ngumu au kutafuta maisha bora.
Mwaka 2021, UNHCR iliripoti watu 3,077 walikufa au hawajulikani walipo hiyo ni karibu mara mbili ya idadi ya mwaka 2020.
UNHCR ilianza kutoa idadi mwaka 2019 na idadi ya watu wanaopoteza maisha inaongezeka kila mwaka.
Hadi sasa mwaka 2022 watu 553 wanaripotiwa kuwa wamekufa au hawajulikani walipo na kulingana na miaka iliyopita wengi wamekufa kwenye njia ya kati ya Mediterranean, data zinaonyesha.
Source: NEWS UN