Ungekuwa na mamlaka na kodi za Tanzania ungeanza na secta gani?

Wamamba

Senior Member
Jan 5, 2024
125
235
Salam

Pato la Taifa,kodi ya MTANZANIA

Nazungumzia fedha inayokusanywa na serikalini kwenye secta zote hapa nchini, namaanisha secta zote, madini,ardh,usafirishaji,mbuga,uchumi wa blue/bahari,hospital nk... zote zote

Kama ungekuwa na mamlaka nazo ungeanza na secta gani? Kuiweka sawa au kuiongezea chochote

Binafsi ningejikita kwenye secta ya Afya, ningejikita tena hapo hapo kwenye secta ya Afya mara ya pili na mara ya tatu

Afya imekuwa gharama sana, ukizingatia tungeweza hata kuitoa bure kulingana na pato nono la Afya, jaribu kufanya ziara binafsi mahospitalini kama una moyo mdogo utaweza ukafunga mwaka mzima kuliombea taifa, raia hapewi huduma mpaka awe na pesa mkononi au akifanyiwa atawekwa pending mpaka alipe pesa ndio atoke/atolewe, nasisitiza kwa pato letu la Taifa tunaweza kuirahisha huduma ya Afya kuwa nafuu au iwe bure kabsa

Huduma hairidhishi, ujuzi finyu, wataalamu wachache, dawa hazina ubora, vifaa duni,

Tungeongeza wataalamu, vifaa vyenye ubora, dawa zenye ubora na ukaguzi mahiri kila baada ya mda na mishahara ingekuwa bora kwa wauguzi, ma doctor na wataalamu wote secta hiyo

Kulikuwa hakuna haja ya kiongozi kutembelea gari nzito ya mil-200 na zaidi wakati kuna mzee/kijana/mtoto anagomewa kufanyiwa upasuaji sababu hana mil-5 kwa ajili ya huduma

Hii sio sawa
 
Ningefungua account nje ya nchi niibe hizo hela, maana hata nikiziacha zitaibiwa na wengine
 
Back
Top Bottom