Unazingatia Vitu gani kabla ya kuingia kwenye Ndoa?

Dr Jeremiahs

Member
Sep 4, 2020
39
304
Kabla ya kuingia kwenye ndoa kuna zile FACTORS za muhimu kila mtu huwa anazingatia. Kutokana na utofauti wa kimtazamo na fikra kila mtu anakuwa na Criteria zake.

Kutokana na uelewa, experience na mtamzamo wako unahisi ni kipi kati ya hivyo ni vya kuzingatia zaidi?

1. ECONOMY STABILITY(UCHUMI)
Uwezo wa kiuchumi kukuwezesha kuitunza familia bado hauruhusu Unahisi kwa uchumi ulionao kujiingiza kwenye ndoa ni kujiongezea majukumu ambayo yatakuumiza kichwa kupelekea kuipa shida familia.

2. AGE (UMRI)
umejiwekea baada ya umri flani afe masai afe simba lazima uoe. kwamba 18-29 ni age ya kuutumia ujana hivyo badala ya kuingia kwenye ndoa na kumsumbua mtoto wa mama mkwe unaona ni bora ule ujana kwanza. au kwamba age ya ujana ni AGE ya kujitafuta hivyo ukichanganya na mambo ya familia utachelewa?

3. PARTNER(MTU SAHIHI)
Je, wewe ni miongoni mwa wanaosubiri mtu sahihi ndipo uingie kwenye ndoa? hapa nazungumzia aina ya familia, historia, malezi, tabia ya mtu unayekutana nae na vitu kama hivyo.

ni upi mtazamo/ushauri wako kwa wewe uliopo na ambae bado hujaingia kwenye NDOA? Na kwann unashauri ivyo.

Nb: Ndoa/mapenzi hayana formula ila kwa namna moja au nyingine Ushauri wako unaweza saidia kupunguza kiwango cha taraka karne hii.
 
Mimi vitu nilikuwa najitahidi nipate kwa mwandani wangu
1.Imani
2.Elimu hata kama tunazungumza tukutane mahali.
3.Afate mfumo wa maisha yangu sio mimi nifate mfumo wake.
4.Malezi ya watoto
5.Mwisho mapenzi ,anipende mimi kama mimi.
 
Back
Top Bottom