Unaweza kuoa mke mwenye sura Personal na akakupasua kichwa tuu!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,081
62,751
Kwema Wakuu!

Kuna ile kasumba ya wanaume waoga, wasiojiamini wanaosema kuwa, Kuoa Mwanamke mzuri ni sawa na kuwa na shamba la miwa karibu na shule ya Kayumba.

Acheni uoga vijana. Yaani uache kuoa Pisikali imenyooka kisa misemo ya waoga, wasiojiamini au Watu waliokataliwa na warembo. Labda sio mimi.

Ni bora useme wanawake wazuri sio type zako, wewe type zako ni zile za kina Achiduke Kingkong.

Kwa taarifa túu nikuambie unaweza kumchukua Mwanamke unayemuona mbaya au wakawaida na bado akakupasua kichwa mpaka ukakonda na kujiua. Kwani wangapi tunawaona huku mtaani.

Nawapa siri ndogo vijana, kuendeshwa na Mwanamke yeyote iwe ni mzuri au mbaya ni wewe mwenyewe ukitaka. Ni maamuzi yako tuu. Lakini ukiwa mwanaume kikamilifu hata Mwanamke angekuwa mzuri kama malaika hawezi kuendesha.

Huyo anayekuendesha akikushinda tuletee sisi tukufundishe namna ya kudili naye. Elewa pia kuwa huyo anayekuendesha akikutana na vyuma kama sisi anajilambalamba na kugeuzageuza macho kwa aibu na kujifaragua.

Kuwa Mwanaume, acha kudekadeka kama mtoto wa kike. Mwanamke ukimdekea anakubandua na kunyoosha kwa upuuzi wako.

Usiwe na shida sana na Mwanamke akijaribu kutikisa kibiriti kama kimejaa muonyeshe wewe haujaribiwi. Akitaka kuondoka mpe mkono wa kwa Kheri.

Onyesha kuwa wewe ni mwanaume bora na ambaye wanawake wenye nguvu wanakutafuta kwa udi na uvumba.
Sio kwa kumtambia au kumnyanyasa, nop! Bali kwa sifa kamili za mwanaume.

Yaani uache kuoa Mwanamke mzuri ambaye unavutiwa naye kisa unasikiliza maneno ya waoga. Ati ooh! Mwanamke mzuri anatongozwa sana. Sasa ulitaka uoe Mwanamke ambaye hatongozwi?

Mimi siwezi kuoa Mwanamke ambaye hajanyooka. Raha ya Mwanamke iwe mashine iliyosomwa mpaka dunia ikuone wewe kweli mwanaume.

Unaogopa Wanaume wenzako kuwa watakuchukulia Mke? Hivi huo woga wa kipuuzi mmeutolea wapi? Hujiamini bablai.

Ni sawa na mtu ati uache kujenga majumba mazuri au kuishi vizuri ati kisa unaogopa kulogwa. Hivi hizo akili huwaga mnazitolea wapi?

Mimi nakuagiza sasa, tafuta chuma kikali, mtoto mzuriii, akitembea Watu wanaacha shughuli zao. Kisha weka ndani. Kula vitu vizuri. Achana na kasumba za kijinga hapa.

Akiku-cheat unaachana naye, unatafuta chuma kingine kikali kilichonyooka. Yaani mpaka wakwanza akupigie simu akuamkie shikamoo. Hakikisha mnakuwa na watoto. Usiwe mjinga mjinga.

Acha kujidharau. Wewe pia unastahili kula vitu vizuri.

Maisha yako ni vile unavyojiona na kujifikiria. Ukijiona haustahili kula vizuri utaishia kuona vizuri vinawenyewe ambao ni sisi.

Kabla hujafa kula maisha Boya wewe. Tembea na Pisikali za aina yote. Tafuta wazungu, waarabu, wasomali, waafrika changanya mbele kwa mbele huko. Usiwe umezubaa zubaa.

Mapenzi yatakuumiza ukishaleta mambo ya kutaka kuamulia moyo wa mtu. Muache mtu afanye anachotaka. Pia mjulishe kuwa wewe nawe unafanya kile moyo wako utakavyokutuma.

Oooh! Taikon unapotosha Watu.
Sikupotoshi, nakuambia ukweli. Ukiishi unavyotaka kuna mambo hayawezi kukusumbua hasa mambo madogo. Ilimradi kuvunjika sheria za nchi.

Mtu anaogopa kuoa mke mzuri alafu akioa sura Personal anaogopa kuongozana na mkewe hata barabarani, sasa hiyo ni akili. Mtu anaogopa hata kumtambulisha mkewe kisa ujinga.

Kuoa sura Personal haimaanishi ati ndio hautaendeshwa na Mwanamke kama unaroho dhaifu. Yaani wewe sio mwanaume kamili.

Mwanaume kama umeoa, imejitahidi kuhudumia familia lakini haujapata hitaji la familia, kama Mwanamke anamdomo mdomo mwambie aondoke atafute hao anaowaona wanafaa, kisha wewe utatafuta Mwanamke mwingine mzuri zaidi yake.

Yaani Wake wa wenzako wakipita mate yakudondoke Wakati na wewe ulikuwa na nafasi ileile. Jitafakari.

Unaogopa ogopa nini? Ati unaogopa kuchapiwa, yaani kama mwehu. Au unaogopa kuachwa kwani wewe mwanamke. Ukiachwa au ukiacha si unaoa tena na tena na tena. Hakuna limit ya kuoa, nani anakupangia, huyo anayekupangia mwambie akuletee Mwanamke mzuri ambaye mtaendana, hawezi basi akae kwa kutulia.

Nitapiga mtu hapa!

Robert Heriel
Mtibeli
 
Nimegairi kuoa ni kheri niwe bachela Maisha yangu yote kuliko kuingia kwenye balaa la kuoa, watu waliooa wanapitia mateso Mungu tu ndio anaejua sitaki kusema sana Ila daah kuna watu wakikusimulia masaibu wanayoyapitia utabakia mdomo wazi

Kwenye hii dunia. Mateso kwa asilimia kubwa mtu hujitakia mwenyewe.
Unaweza ukaishi bachela na bado ukateseka Mkuu. Itategemea unayachukuliaje Maisha
 
Kwenye hii dunia. Mateso kwa asilimia kubwa mtu hujitakia mwenyewe.
Unaweza ukaishi bachela na bado ukateseka Mkuu. Itategemea unayachukuliaje Maisha
Kuoa ni zaidi ya kisanga, waliooa Waite 10 waliooa kisha mwambie mmoja mmoja akusimulie anayoyapitia ndani kwake Mzee kesho unaachana na masuala ya Ndoa kuna watu wanapitia mateso sio kawaida wapo wanaokaa siku nzima wanaongea pekeyao tu sababu ndani hapatoshi, nishashuhudia jamaa anafokewa km mtoto na matusi juu na mke wake wa kumuoa hadi naona huruma jamaa kwanini ulioa hii mwanamke?
 
Kijana unafurahisha Sana.

Ndoa tamu asikudanganye mtu.

Hizo changamoto ni wale ambao wamechanganya ubinafsi ndani ya ndoa
Ingia uone utamu wa ngoma ingia kati uicheze sio unaongea ukiwa pembeni, utamu upo na uchungu pia upo Ila uchungu ni mwingi kuliko utamu
 
Back
Top Bottom