Unaweza kukabiliwa na adhabu gani endapo ukitembea kipindi bendera inashushwa?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,321
50,541
Najua humu ndani pia wapo makauzu waliovurugwa na wenye stress zao juu ya ugumu wa maisha hasa ukizingatia kama magari aina ya mashangingi, ma cruiser, na ma fortuna STN Yananunuliwa kila uchwao... ni wale ambao wanapopita karibu na taasisi za umma mida ya 18:00 jioni huwa hawana habari hata wakisikia filimbi.

Kimsingi kabisa ukipatikana na kosa hilo la kutoheshimu wakakubeba ukaleta ubishi mpaka mahakamani adhabu yake kikawaida inaweza ikawa nini kifungo cha muda gani?
 
Hizo sheria za bendera hazipaswi kufanya kazi sehemu za mijini changanyikeni.

Filimbi yako haiwezi kuzidi kelele za miziki barabarani au honi za magari.

Na saizi hata tukisikia sauti ya filimbi hata hatustuki wala kufikiria kuwa inatokea kwenye bendera.

Mijini filimbi zinatumika kwa mambo mengi wengine hutumia kuangazia biashara zao. Wengine jogging nk.

Sasa hauwezi ukawa kila tu ukisikia sauti uanze kutafuta bendera ilipo ili usimame
 
Mara nyingi ukimuweka ndani akionyesha uoga anakupa sukari mnamalizana, Akileta za kuletwa mnachapa na kuachia.
 
Walking or sitting down when the National Flag is hoisted or lowered is regarded as disrespect to the National Flag. It is an offence under section 7 of the National Emblems Act [Cap.10 R.E 2002] to do an act which brings into contempt or ridicule the National Flag or Coat of Arm of the United Republic of Tanzania.

This offence is punishable by a fine not exceeding TZS 20,000 or to imprisonment for a term not exceeding 2 years or to both.

 
Punishment yake ni mbaya ikiunganishwa, fanya vyte usiwe mfano. Na si unajua mfano hutokea muda wwte. Tuheshimu tu kushusha au kupandisha
 
Back
Top Bottom