Unaweza kuishi kwa bajeti ya 5000 hadi 10,000 kwa siku? Hebu tujadili!

Leo_Edward

Member
Mar 17, 2025
9
13
Maisha ni magumu, gharama za maisha zimepanda, lakini bado kuna familia zinazoishi na bajeti ndogo. Swali ni moja: Ukiwa na 5000 hadi 10,000 tu kwa siku, unaweza kupata milo mitatu kwa familia yako na ikatosha? 🤔

Hebu tuweke hali halisi mezani. Unaamka asubuhi na hiyo bajeti mkononi. Unahitaji chai, chakula cha mchana, na cha jioni. Je, inatosha? Na kama inatosha, unapanga vipi hiyo hela?

🔹 Asubuhi 🌅

Unaianza siku na bajeti hii, unajipangaje ili kila mtu anywe chai na ashibe?

Je, kuna mbinu unazotumia kupunguza gharama?


🔹 Mchana ☀️

Chakula cha mchana kinahitaji uwiano wa bei na kushiba, unahakikisha vipi familia yako inapata mlo wenye kutosha?

Unapanga bajeti kwa vipi kuhakikisha pesa haitoshi mchana tu?


🔹 Jioni 🌙

Baada ya siku nzima, unahakikisha vipi chakula cha jioni kinapatikana na kinalingana na bajeti yako?

Je, kuna njia zozote unazotumia kuokoa pesa na bado mkapata chakula cha kutosha?


Sasa, naomba watu wa Dar, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kigoma, Mtwara na mikoa mingine waweke uhalisia wa maisha hapa. Unatumiaje kati ya 5000 na 10,000 kwa siku, na upo mkoa gani?

👉 Unagawanyaje bajeti yako kwa siku?
👉 Unafanya nini kuhakikisha pesa haitoshi mlo mmoja tu?
👉 Kuna mbinu zozote unazotumia kupunguza gharama?

Hebu tujadili uhalisia wa maisha yetu! 👇

#MaishaHalisi #BajetiNdogo #Tanzania #MaishaYa5000Hadi10000
 
1. Size ya familia inatofautiana.
2. Huwa haitoshi, tunasukuma siku tu.

Mazingira unayoishi pia yanachangia...kuna sehemu unapata;
  • sukari guru
  • sukari ya sh 200
  • nazi nusu kipande
  • majani ya chai yamechanganywa na sukari kwenye kifuko sh 200
  • bakuli la maharage kwa sh 500
  • wali mkavu sahani jaa sh 1,500
Kuna maandazi, vitumbua, bagia, mihogo, kachori, pweza, nguru, kachumbari etc.

Milo mitatu sio lazima, lishe bora sio muhimu...tunakula kushiba, mlo mmoja unatosha.

Kuna wenye 100,000 kwa siku pia wanaajiuliza swali hili hili, itatosha kweli?
 
Inategemea na unapoishi mkuu. Kama upo sehemu kama mbagala inatoboa kabisa.

Ama uwe unaishi mkoa wa mbeya hapo mnakula mpaka mnasaza
 
Mbona simpo sana kama unavyo baadhi ya vitu ndani kama mafuta ya kupika, unga, mchele n.k
1. Dagaa fungu mbili 2000 (japo hata moja linatosha pilipili nyingiiiiiiiii.)
2. Viungo vya mboga @1500 (hapa bamia na nyanya chungu za kutosha)
Kama huna unga kwa familia ya watu 4 hadi 5 unga robo 3 au kilo unatosha @1400 kwa kilo.
Mchana umepita hivyo unawaza usiku.
 
Back
Top Bottom