Unasherehekea Pasaka au Easter

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
830
897
Habari Ya PASAKA Wana JF hivi mnajua Mnachokisheherekea Siku Ya Leo Twende Pamoja na Mimi.

UNASHEREHEKEA PASAKA AU EASTER?
Naamini tunajiandaa kwajili ya sikukuu ya Pasaka.Lakinini wengi wetu hatujui kutofautisha kati ya Pasaka na Easter,wengi tunashehekea Ista,siyo Pasaka,na ni kosa kubwa iliyoje!!

Pasaka ni sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina "Pasaka" limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh).

Pasaka ilianza kuadhimishwa kipindi wana wa Israeli wanafanya maandalizi ya kutoka nchi ya Misri(1200KK) walikokuwa watumwa.

Mungu aliwaamuru kupitia kwa mtumishi wake Musa kwamba wapake damu ya mwanakondoo katika miimo ya nyumba zao ili yule Malaika wa kifo atakapopita asiweze kuwadhuru wazaliwa wao wa kwanza, hivyo yule Malaika alipopita na kuikuta ile damu ya mwanakondoo katika miimo ya nyumba zao, alipita juu kwa juu(ali-passover)

Sasa kitendo hicho cha Malaika kupita juu, ndicho kinachoitwa Pasaka, (kwa lugha kiingereza “pass-over”). Hata wakati Yesu alikuwepo hapa duniani,alishiriki kwenye adhimisho ya siku hiyo maalum kwa wayahudi.

Lakini swali lingine ni kuhusu Easter? Je Easter ni nini?, je ipo kwenye biblia? na je sisi wakristo tunaruhusiwa kuiadhimisha easter?

Neno Easter, halipatikani mahali popote katika Biblia, kama jinsi pasaka linavyopatikana katika sehemu nyingi, katika biblia (Easter lenyewe halipo kabisa).

Sasa Easter kama haipo imetoka wapi katika Ukristo?

Asili ya Easter, ni mungu wa kipagani (wa kike), aliyeaminika kuleta “uzao” kama vile “baali” alivyokuwa.. mungu huyu aliabudiwa na jamii ya watu wa Saxons, ambao kwasasa ni maeneo ya Ujerumani, na aliitwa “easter” kutokana na “mawio ya jua”. Upande jua linapochomoza, uliaminika kuwa ni upande wa neema na ndio unaomstahili huyu mungu mke, hivyo upande wa mashariki ni “East” kwa lugha ya kiingereza, kwahiyo kwa heshima ya mungu huyo wa uzao ndio wakamwita “easter”..yaani “wa mashariki”.

Na mungu huyu “easter” alikuwa anatolewa sadaka za kafara kipindi kile kile cha sikukuu za pasaka za kiyahudi, tarehe hizo zilikuwa zinagongana, kipindi ambacho Wayahudi wanasheherekea pasaka, ndio kipindi ambacho watu hao wa-Saxons na wengine wengi walikwenda kumtolea mungu wao huyo easter sadaka.

Kwasababu ni kawaida ya shetani kutafuta kuchanganya ukristo na upagani, alinyanyua watu kadhaa na kuoanisha siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu, na siku ya sadaka za mungu huyo “easter”.

Hivyo ili desturi na kumbukumbu la mungu wao huyo “easter” lisife kabisa kabisa, ndipo wakaiita ile jumapili ya kufufuka kwa Bwana kama “jumapili ya easter”. Narudia,shetani halali na anafanya kazi.Easter siyo Pasaka!

Sasa swali ni je! Na sisi wakristo tunaruhusiwa kuadhimisha easter kama sherehe ya kufufuka kwa Bwana Yesu?

Siku ya kufufuka Bwana Yesu, itabaki pale pale, na ni vizuri kuiadhimisha, kwasababu ni siku ya ushindi wetu, siku ya matumaini, na siku ya shangwe, Mitume na watakatifu wote, kipindi wamejifungia ndani kwa hofu ya wayahudi, siku walipomwona Bwana kafufuka walifurahi furaha kuu.

Luka 24:34-35 “wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni.Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao katika kuumega mkate."

Kwenye aya ya 41" BASI WALIPOKUWA HAWAJAAMINI KWA FURAHA, huku wakistaajabu, aliwaambia, mna chakula chochote hapa?”.

Hivyo na sisi hatuna budi kuiadhimisha siku hiyo kwa furaha nyingi, katika siku ile ile Bwana aliyofufuka, (yaani Jumapili ya pasaka), haijalishi watu wanaiitaje hiyo siku, watu wameipa jina gani, hata kama wangekuwa wameipa jina la “siku kumwabudu shetani” sisi hatutazami majina watu walioyapa siku, (tunaitazama siku yenyewe).. hata siku tulizozaliwa tukizifuatilia katika historia tutakuta zimepewa majina ya ajabu ajabu, lakini wau hawaachi kuziazimisha kisa tu zimepewa majina ya ajabu, au zimeangukia katika tarehe za kuadhimisha mambo mabaya..

Leo ukifuatilia katika historia au kumbukumbu, utakuta kila tarehe imengukia katika maandimisho fulani ya sikukuu za kipagani, hivyo hatuwezi kuacha kufanya mambo ya msingi katika hizo siku, na kuzifuata kalenda za kipagani.

Kwahiyo sisi wakristo tunasheherekea siku ya kufufuka kwa Bwana kama “jumapili ya ushindi” na si kama “easter”. Na hatusheherekei kipagani.

Siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu, tunapoiadhimisha kwa kwenda Bar, kulewa hapo tumeisheherekea easter, na si siku ya kufufuka kwa Bwana, siku ya jumapili ya kufufuka kwa Bwana tunapoisheherekea kwa kwenda disko, au kwenye kumbi za anasa, hapo tutakuwa tunamwadhimisha mungu “easter” na si “ufufuo wa Bwana”. Kwasababu waliokuwa wanamwadhimisha huyo mungu mke easter, katika siku hiyo walikuwa wanalewa na kucheza kipagani na kumtolea sadaka.

Lakini sisi wakristo hatuadhimishi/kusheherekea siku hiyo kipagani hivyo, bali siku ya kufufuka kwa Bwana ni siku ya kufanya ibada, ni siku ya kutafakari maisha yetu ya ukristo, tangu tumempokea Yesu mpaka sasa tumeshapiga hatua kiasi gani? Na kama tumerudi nyuma basi tutengeneze mambo yetu, ni wakati wa kutafakari ni mambo yako mangapi mazuri ya kiroho, yaliyokuwa yamekufa, na je yamefufuka!.. Kama bado ni wakati wa kutafuta kuyafufua.

Mtakie mwenzio Pasaka(Passover) njema, sio easter njema 🙏 🙏
 
Kwenye biblia ni wapi imeandikwa kuna sherehe inayoitwa pasaka?
 
Kama hakuna andiko linalo thibitisha ni usanii kama usanii mwingine
Mpaka Hapo Inaonesha Hujawahi soma biblia hata nikikuuliza passover ni nini huwezi nijibu

Pasaka kwenye Bibilia Ipo sana na imeandikwa siwezi kutafunia kafungue biblia na usome kitabu cha kutoka
 
Mpaka Hapo Inaonesha Hujawahi soma biblia hata nikikuuliza passover ni nini huwezi nijibu

Pasaka kwenye Bibilia Ipo sana na imeandikwa siwezi kutafunia kafungue biblia na usome kitabu cha kutoka
Huna unachojua wala hakuna sherehe inayoitwa pasaka
 
Back
Top Bottom