Unamuita mtu mjinga na bado umemfollow!

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
152
371
Mitandao imewafanya watu kukosa amani na furaha, imeua watu wengi na wengine mpaka kupata matatizo makubwa. Watu wameyaweka wazi maisha yao mitandaoni kwa kutegemea watapata kitu fulani halafu ghafla tu hawapati kile walichotegemea kukipata.

Mitandao imewafanya wanawake wazuri, wanaovutia kuliko wengine kujiona wakiwa wabaya, mitandao imewafanya watu kuishi maisha ambayo si yao, mitandao imewafanya watu kuwachukia watu wasiofahamiana nao hata kidogo.

Mitandao inakufanya mwenye akili kujiona mjinga, inakufanya mjinga kujiona mwenye akili. Mitandao inakuonyesha maisha ya uongo ya watu wengine, inakuonyesha upendo wa bandia na chuki ya uongo.

Mitandao imewafanya mpaka watu wanapomshukuru Mungu kwa kupata kazi, wengine wanachukia, mitandao hii hii imewafanya watu kuishi maisha ya wengine.

Wakati naingia kwenye mitandao, nilijisemea kwamba KAMWE sitomuomba mtu msamaha kwenye mitandao hata nikimkosea vipi. Kamwe sitokuja kumuheshimu mtu yeyote kisa posti zake, kamwe sitokuja kumsimanga mtu kisa posti zake, na kamwe sitokuja kumcrash mtu yeyote kwenye posti zake, hii imenifanya hata kutokushiriki kwenye posti za watu wengine kwa miaka na miaka, nipo hivyo, huwa napenda kubaki kimya kwa sababu kila mtu huwa na moyo wake wa mapokeo.

Kuna dada anaposti picha yake, ni mzuri, comments 100 zinasema ni mrembo ila mtu mmoja mwenye chuki anasema yeye si mrembo, dada huyo anawasahau hao watu 100 kwa sababu ya mtu mmoja. Yaani huyo mtu mmoja anamfanya kukosa raha, siku nzima anafikiria, anawasahau watu 100 waliomsifu.

Kitu ambacho kitakusaidia sana kwenye maisha ya mitandao, cha kwanza unfollow watu wote unaohisi ni wajinga. Yaani wale unaowaona hawana akili, waunfollow fasta. Mfano, mtu akisema yaani wewe Mhaya uzi wako hauna maana au wewe huna akili kabisa, jambo la kwanza ndugu yangu huyo mtu asiyekuwa na akili muunfollow, ukiendelea kumfollow inamaana na wewe pia huna akili.

Yaani inakuwa hiviiii! Kama umefollow wacheza x inamaanisha unazipenda x, so hii inaonyesha kwamba na wewe unaweza kuwa mcheza x. Sasa kuepuka hilo, inabidi uwaunfollow wacheza x.

Ni sawa na hao wengine, unamuona mtu ni choko, halafu unacomment kwa posti ya choko tu kwamba hana lolote, bro! Kwanza jua kwamba na wewe una dalili za kichoko na ndiyo maana umemfollow choko.

Mimi huwa naunfriend watu wajinga ambao naona kwangu wanazingua, huwa sipendi kufollow watu ambao tayari akili yangu imekwishajua kwamba hawa ni wajinga. Yaani mtu anaposti kitu kinakuuma weeee, halafu bado umemollow, huyo mtu unayehisi ni mjinga inawezekana si mjinga bali mjinga ni wewe.

Linda sana moyo wako mshikaji wangu, maisha ni magumu, unakuja mitandaoni ili ulifresh akili yako halafu kila siku unakutana na posti za watu na zinakukasirisha, kwa nini ubaki kuwa nao tu? Kwa nini uumie kila siku? Kwa nini maisha yakutese halafu unaingia mitandaoni na kuendelea kuteseka?

Kuna jamaa aliwahi kuniambia: “@nodiebwoy wewe mjinga sana”. Nikasema ili kumsaidia kutokuendelea kuona posti za mjinga, nikamuunfriend, alipoona hivyo, akaamua kunifollow. Kwa sababu gani? Yeye ni mjinga kuliko mimi, sema tu hajajijua bado.

Kwenye mitandao epuka sana stress, epuka sana mahasira. Tatizo letu tunawachukia watu fulani halafu tunapenda sana kufuatilia maisha yao. Kwenye kundi la Simba tulisema kusiwe na posti za Manara kwa sababu anakera, halafu mjinga mmoja anakwenda huko anachukua posti yake, anaiscreenshot na kuja kusema: “Chekini huyu fala alivyoandika”, bro! Manara si fala, fala ni wewe ambaye umemfollow mtu unayehisi ni fala.

Mjanja hamfollow mjinga wala fala. Mchungaji hamfollow mcheza X. Page ya kanisa haiwezi kuifollow page ya msikiti fulani, au page ya msikiti kufollow page ya mwamposa. Watu wanawafollow wale watu wanaoendana. Mtu anayependa kusikiliza nyimbo, anawafollow wasanii, anayependa kufuatilia mpira anawafollow wachezaji.

Kama umewahi kumuita mtu mjinga na bado umemfollow, bro au sista! NIKUHAKIKISHIE kwamba wewe ni mjinga kuliko huyo jamaa. Maybe unasema huyu jamaa anatudanganya sana, halafu hapohapo bado umemfollow, inamaanisha nini? Unapenda kudanganywa, la pili, kama unapenda kudanganywa namna hiyo, wewe si mjinga, wewe ni MPUMBAVU.

Nenda sehemu ya page ulizofollow ama orodha ya marafiki zako, ukiona umefollow watu wajinga, ambao si sahihi kwako, haraka sana waunfollow na kuunfriend, usijipe chuki zisizo na maana kwa kuwachukia watu wasiokujua, utajipa gonjwa la roho huku ukiwa hujafikisha hata miaka 70.

Wazungu wanajiua sana kwenye mambo haya, kwa nini? Kwa sababu nao wameweka urafiki na kufollow page za wajinga. Nakushauri kama kaka yako, unfollow wajinga, unfriend wajinga. Ukiendelea kushikamana na wajinga, na wewe pia utakuwa mjinga bila kujijua.
 
Bro Sema aliyekuudhi tumchape, mtu mmoja mjinga hawezi kukunyima raha wakati unatumia bando lako!
Hivo unavyolalamika bila ya kumtaja ndo anazidi kuvimba pembeni.

Hapo anakucheka huku anasema, “ Lile boya nimelikomesha, nimelipiga spana mpk limenifungulia uzi” 😂😂😂
Sasa wewe mchane ajijue aache unaa
Wanaume hampigi jungu km sie mademu, FUNGUKA MTAJE
 
Back
Top Bottom