Unampaje mtu utajiri huku wewe ukiunguza maini na kuharibu figo zako?

felakuti

JF-Expert Member
Aug 16, 2024
417
882
Je hii inaingia akilini?

Sijaona na sitoona faida ya pombe kabisa. Nimekaa na kutafakari kwa kina kwamba yani mimi ninunue pombe haswa hizi kali niharibu maini na figo ili nimtajirishe mmiliki na mtengenezaji wa hizo pombe?

Ndugu zangu haswa wakati huu ambao tunaelekea kwenye sikukuu za kumaliza mwisho wa mwaka, watu huona kunywa pombe ndio starehe haswa ya kufurahia sikukuu ndugu zangu tuache pombe. Pombe haina faida yoyote.

Embu one mwana wa valuvalu Jose Chameleone yuko hospitalini hivi sasa afya yake imezorota sababu ya pombe, je nikuulize wale waliokua wanakunywa nae wapo wapi?

Je wamiliki wa hayo makampuni za pombe wako wapi ,? Wao wako wanakula raha kwa pesa zenu mlizowachangia za kununua pombe zao, mbaya zaidi wao hawanywi pombe..

Ewe kijana, jiwekee malengo kua mwaka 2025 hakuna pesa yako itanunua pombe,hujachelewa, jiwekee malengo sasa na Mungu akusaidie.
 
chemistry ya pombe ni ngano au mahindi mixer additives nyingine kama rangi n.k

sidhan kama pombe inamadhara ikitumiwa kwa kias
Kuna aina kadhaa za pombe

1.Beer

Hapa mchawi ni misosi tu,ukiamka piga supu nzito au mchemsho,vilevile ukiwa bar nyama na ndizi ni muhimu.
Hutoona madhara yeyote kimwili labda kipesa.

2.Grants

Hapa napo panahitaji utulivu kidogo japo mara nyingi pombe hizi ni za gharama na mara nyingi hununuliwa na watu wenye vipato.

3.Spirit

Hapa kuna aina zote za pombe za bei rahisi na za gharama.
Madhara yote ya kimwili kuunguza maini Sura kushuka (kukaa kilevi) yapo kwenye hizi pombe

Makundi yote ya vijana wenye nacho Kwa wasiokuwa nacho wapo hapa

Hata ukiwa na buku mbili za kitanzania unalewa na unakuwa vibe ,kwenye hili kundi la pombe ndipo kwenye pombe feki nyingi na zinatengenezwa kiholela bila kufuata viwango.

SIJATAJA MAJINA POMBE YEYOTE ILI KULINDA BRAND ZA WATU

NB: Pombe ikitumiwa Kwa kiasi na Kwa uangalifu haina madhara,
Ila kinyume chake ni balaa kuanzia kushuka kiuchumi hata afya ya mwili na akili.
 
Maisha yana options nyingi sana mkuu, unaishi upendavyo na unamchangia pesa zako anayekupa furaha so fanya tu kile roho inapenda! Hamna mtu wa kudumu humu duniani, mwingine akiunguza maini yake mwingine anakwenda kwenye maombi kumchangia mwaiposa na maisha yanaenda mwisho wa siku life well spent mnazama futi sita kila ntu kwa wakati wake!
 
Kila kitu kwa kiasi pombe haina madhara kama unakunywa kwa kiasi.
Pombe imenywewa na kila jamii since antiquities, na imekua ishara ya mijumuiko ya kila mtu kwa jamii yake, ndio maana kila mahali duniani ukifika utakua wanatumia mazao waliyonayo kutengeneza aina yao ya pombe, hata Yesu alitengeneza pombe kwenye karamu kwa sababu hizihizi!
 
Mimi binafsi kuna vitu ambavyo huwa vinanichanganya.. Ukienda bar ndio utakuta ndinga za maana zimepaki, wapiga bia ndio wana nyumba kali, wanasomesha watoto shule kali n.k.
Therefore, research ya kwamba bia humaliza hela haina validity yeyote.
Kimsingi kila mtu ashinde mechi zake.
 
Pombe ina faida kwa wenye akili tu ila kwa wapumbavu ni hasara kubwa sana.
 
Waliolazwa na Chameleon ile hospitali wote wanakunywa pombe ndio zimewalaza?

Hebu tupishe please!

Nenda muhimbili mwaisela angalia sensa ya waliolazwa sababu ya pombe kisha kompea na waliolazwa sababu ya visununu vya roho kama chako

Wewe unaepiga punyeto hujihurumii wala huoni unamnufaisha mwenye kiwanda cha sabuni sio?

Kila mtu ashinde mechi zake please
 
Hivi ugonjwa wa chameleon unaweza kuwa associated na zile story zilivuma kwamba jamaa anaangaika kumkacha shetani, nakumbuka kisa Cha kwanza ni kama alitaka kujiua ghorofani kama Sina kumbukumbu nzuri, na baada ya hapo akatoa ule wimbo unaitwa "natamani nikuone"

Then valuvalu, from there nyimbo ziko juu ila dizaini yeye ni kama akawa anasambaa, shortly seems as if the guy sold his soul to Satan, Sasa anastrive to bring it back! Najaribu kuwaza tu lakini kwa kuchunguza mtiririko wa matukio ,na ujumbe kwenye wimbo wa natamani nikuone,

Huo ni mtazamo wangu ulimwengu ule. Ila huku tunajua ni pombe, zimeharibu Figo, science pia Huwa na majibu kwenye mambo ya kiroho,
Any way tumwachie mwenyewe, ila tutaprove kwa mwingine wa level zake

Na Mimi najua ukiona mtu anakunywa pombe sana ujue ana jambo halipo sawa kwenye maisha yake , hivo anapambana nalo, nyie mmekazana kumwambia acha pombe ,badala ya kumuuliza una lipi linakusibu,taraatibu huku mmempa ofa ya beer🍺🍺
 
Ukimaliza ya pombe pia washauri waache matumizi ya sukari kwani huleta kisukari na hatimaye mwili kuanza kuoza.
 
Prof j nae si aliumwa kidgo tumpoteze au nae aliweka bondi roho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…