felakuti
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 413
- 875
Je hii inaingia akilini?
Sijaona na sitoona faida ya pombe kabisa. Nimekaa na kutafakari kwa kina kwamba yani mimi ninunue pombe haswa hizi kali niharibu maini na figo ili nimtajirishe mmiliki na mtengenezaji wa hizo pombe?
Ndugu zangu haswa wakati huu ambao tunaelekea kwenye sikukuu za kumaliza mwisho wa mwaka, watu huona kunywa pombe ndio starehe haswa ya kufurahia sikukuu ndugu zangu tuache pombe. Pombe haina faida yoyote.
Embu one mwana wa valuvalu Jose Chameleone yuko hospitalini hivi sasa afya yake imezorota sababu ya pombe, je nikuulize wale waliokua wanakunywa nae wapo wapi?
Je wamiliki wa hayo makampuni za pombe wako wapi ,? Wao wako wanakula raha kwa pesa zenu mlizowachangia za kununua pombe zao, mbaya zaidi wao hawanywi pombe..
Ewe kijana, jiwekee malengo kua mwaka 2025 hakuna pesa yako itanunua pombe,hujachelewa, jiwekee malengo sasa na Mungu akusaidie.