Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,037
- 4,752
Kuna mnyukano wa hoja huko X kati ya wafuasi wa Mwigulu na Wafuasi wa John Pambalu
Pambalu anadai alichukua cash akaenda airport akiwa anasafiri akategemea anaweza kupata dola lakini alipofika airport DAR es salaam akakuta akaambia hakuna dola hata moja kwenye Bureau De change na benki.
Ikamlazimu apande ndege akiwa na pesa ya Tanzania , alipofika Uholanzi anataka kubali pesa ya Tanzania to USD akaambiwa pesa ya Tanzania haitambuliki labda awe na pesa ya Kenya. Ikabidi ashinde bila kula aaaahaaaa
Mwigulu anapojibu hoja anaeleza kwamba Dunia imeondoka kwenye cash economy kwenda kwenye cashless na kwamba kutembea na cash nje ya nchi ni ushamba. Anajibu kwamba viongozi wanatakiwa kubadilika waendane na mahitaji ya dunia akimaanisha Pambalu alipaswa kuwa na visa card kwa ajili ya kumsaidia kufanya matumizi huko nje.
Wananchi kwenye mjadala huu wamegawanyika makundi matatu
1. Wanaokubaliana na Mwigulu kwamba John Pambalu anapaswa kutumia visa card akaachana na kutembea na madafu
2. Wapo wanaokubalina na John Pambalu kwamba Duniani kote kuna maduka ya kubadilisha fedha na lengo lake ni kuhudumia soko la wale ambao wanatambua kwamba gharama za visa card ni kubwa na maeneo mengine siyo huduma zote unapata kwa cashless . Hivyo hata kama dunia inakwenda kwenye cashless bado cash economy inafanya kazi.
3. Baadhi wapo neutral kwamba ni kweli tunatakiwa kutumia kadi lakini wanamuuliza Mwigulu, akisafiri kama waziri anafikia kwenye vyumba au hotel anazofikia Pambalu? Je, soko analopaswa kununua Waziri (Malls na hotel 5 stars) ni sawa na soko la Pambalu anayelala 1st star hotel? Ni kweli kwamba maeneo anayetembelea Pambalu anatakiwa awe na visa card pekee bila cash? Anafahamu kwamba Pambalu anawakilisha wananchi wasio na kipato kikubwa ambao soko lao kubwa linahitaji cash?
Lakini kwangu mimi msimamo na ushauri wangu huu ni kwamba
1. Nampongeza Waziri wa Fedha kutukumbusha Watanzania umuhimu wa visa card unapokuwa nje ya nchi. Nampongeza kwamba ameonyesha anao ufahamu mkubwa kuhusu cashless economy lakini hana uelewa kwanini bado Dunia hasa ulimwengu wa kwanza bado wana cash economy.
2. Nampongeza Pambalu kwa kutofahamu kwamba kwa hadhi yake alipaswa kutegemea zaidi visa card kuliko kutembea na fedha cash. Namshukuru pia kwa kutueleza kwamba huko Duniani fedha yetu haipo sokoni ila pesa ya Kenya inatambulika. Naogopa sana kuona kwamba hoja yake imeonyesha wazi kwamba Waziri wa fedha anayo kazi kuhakikisha pesa ya Tanzania inaingia kwenye soko la Dunia badala ya kudhibiti dola ndani.
Mwisho, Je kama tupo kwenye cashless economy kwanini maeneo mengi Tanzania tunatumia cash? Kwanini Duniani kuna maduka yakubadili fedha? Kwanini pesa ya Kenya inatambilika Uholanzi lakini ya Tanzania hakuna anayeitambua?
Tunakaribisha mawazo