GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,190
- 10,316
Unatarajia mtu aliyelelewa katika mazingira ya ubinafsi kuanzia nyumbani hadi shuleni atakuwa na tabia gani kama siyo ubinafsi mtupu?
Fikiri, alipokuwa mtoto, aliaminishwa kuwa nyama nzuri kama paja la kuku ni mahsusi kwa ajili ya baba. Anaweza akajenga matumaini kuwa naye atakapokuwa mkubwa, atakuwa anakula mapaja ya kuku huku"wadogo" wakiambulia vipapatio. Bahati mbaya ni kuwa anaweza kutembea na huo mtazamo hata kwenye majukumu yake ya kikazi. Akipewa nafasi nyeti, atahakikisha anakula "vinono" vya umma bila kujali kama wengine wanaumia au la!
Shuleni, tulikuwa tukipikiwa uji ambao wakati mwingine ulikuwa hauna sukari ya kutosha huku walimu wakipewa chai na vitafunwa vizuri. Hilo nalo ni sehemu ya mafunzo ya mwanafunzi, kuwa ukiwa "mkubwa" unatakiwa utendewe kwa ubora zaidi tofauti na wadogo.
Kwa aliyesomea sekondari za Serikali hasa za bweni, anafahamu kuwa baadhi ya wapishi walikuwa wakiandaa vyakula vya wanafunzi ovyo hovyo, tofauti na ambavyo vya walimu vilikuwa vikiandaliwa. Hiyo ilikuwa na athari gani? Kumfundisha mwanafunzi "kutokujali"
Hata waliokuwa wakigombea nafasi za uongozi shuleni (viranja), wengi wao walifanya hivyo wakiamini kuwa kiongozi kutawapa ahueni wawapo shuleni. Kwanza, kuliwapumzisha kufanya kazi zisizopendwa na wengi kama kupasua kuni na kudeki vyoo. Pili, kuliwapa uhakika wa kushiba hasa kwa shule ambazo upatikanaji wa chakula cha kutosha ulikuwa ukisuasua.
Mifano ni mingi!
Sasa kama mtu tokea akiwa mdogo mpaka amekuwa mkubwa, mazingira aliyokutana nayo ni kama vile yamemfundisha kuwa "mkubwa" ni kufaidi zaidi ya wengine, unategemea afanye nini kwenye ofisi ya umma?
Hata kama hana njaa ya hela, bado anaweza kufanya ufisadi kwa kuwa tokea utotoni kajifunza kwamba kuwa kwenye "nafasi" ni kufaidi zaidi ya wasiokuwa na nafasi.