Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 16,752
- 22,077
Kijeshi, Admiral wa Navy ni cheo sawa na General wa Army. Muundo wetu sasa hivi unataka kuwepo na General mmoja tu kwenye TPDF ambaye ndiye CDF. Hiyo inakinzana sana na muundo wa jeshi zima, kwani vyeo vya Navy viko juu sana ya vyeo vya Army. Kwa mfano Captain wa Army ni sawa Lieutnant wa Navy, na Captain wa Navy ni sawa na Colonel wa Army, ndiyo maana Captain wa Navy ainaitwa Navy Captain, siyo Captain tu. Lt General wa Army ni sawa kabisa na Vice Admiral wa navy. Sasa hapo ndipo kuna tatizo; ingawa jeshi linaweza kuwa na Lt Generals kadhaa, lakini cheo hiki ni special kwa ajili ya COS; maluteni generals wengine ni wale waliopandishwa cheo wakati mmoja na COS aliyepo madarakani au kabla yake, na hali hii huwa inatokea mara chache sana kwani mara nyingi sana maluteni general hao waliokuwapo ama hustaafishwa au hupelekwa ubalozini haraka sana kabla ya COS mpya kuanza kazi. Sasa kwa mfumo huo jeshi letu la Navy linakuwa na ugumu sana wa kupata Admiral na Vice Adrmiral; kwa maana mkuu wa Navy la Navy Tanzania atakuwa ni Rear Admiral ambaye ana cheo sawa na Major Ganeral au Brigadier General, hawezi kuwa Vice Admiral au Admiral.