Unajionamchafu?, Hata simulizi za biblia zinawataja Madent na Mabad boyz!,

Paspii0

JF-Expert Member
Apr 10, 2020
479
683
Kuna hii stori huwa watu wanapenda kuibonga kila siku, eti “Hiki kizazi kimeharibika mbaya!” Wanatuzushia sisi wa kizazi cha amapiano,kana kwamba tumezaliwa na chuki ya ndoa, mapenzi ya ajabu, na ushamba wa kihuni. Lakini we acha! Ukiingia kwa maandiko, utakimbia bila viatu. Hapo zamani watu walikuwa wamelost level ya hellfire premium!

Cheki hii...

Kulikuwa na jamaa mmoja mkora anaitwa Onani. Huyu jamaa alipewa mke wa bro wake (sijui kama ni kama vile tunaita rebound ya kifamilia)… lakini jamaa akasema mimba siyo lazima. Akaleta ubunifu wa ajabu: "akimlalia huyo mdada, alikojoa nje ili mimba isimpate!" (Mwanzo 38:9). Hii ni Bible bana, sio fiction. Mkubwa kabisa akaforce coitus interruptus kabla wazungu wajainvent hiyo term!😃, mwanetu sayansi kitambo!!!

Kuna huyu jamaa mfalme wa staili mkali wa kudunda vijeba kina goliath anayeitwa Daudi. Jamaa kaona mrembo anaoga rooftop, akaanguka majaribuni faster kuliko mtu akiona M-PESA ya 100K imengia kimakosa. Akajua mrembo ana mume, lakini kwa vile yeye ni mfalme, akaona "hii ni deal ya mungu amenitumia." Akaagiza mume wa huyo demu aende vitani... frontline bana! Kisha jamaa akafa, Daudi akabaki nyumbani akiishi kama kingo wa bibi wa mtu. "Mwekeni Uria mstari wa mbele, alafu mvue polepole... apigwe na afe" (2 Samweli 11:15).

Watu walikuwa wameharibu zamani sana. Sisi leo tunapost tu heartbreak kwa status, wao walikuwa wanapanga murder kwa mapenzi.

Halafu kuna madada wa zamani kama Rahabu, mtaa clean, yaani afisa Uroda kama wale wa riverside ubungo😝, Yeye aliwahi kuwa kahaba lakini akatumika kuokoa watu wa Mungu. Chuo alichosoma: Streets University. Lakini bado Mungu alimtumia. "Rahabu kahaba" (Yoshua 2:1) Bible imesema, sio mimi.

Na ukidhani hiyo imetosha, kuna bro mmoja Kaini ,alimchinja ndugu yake kwa sababu Mungu alipenda sadaka ya bro wake kuliko yake. Imagine hiyo petty!


Wanangu eeeehhh………!
Tunaambiwa kila siku kizazi chetu kimeharibika. Lakini ukweli ni kwamba kuharibika siyo jambo jipya, hata wazee wa kale walifanya madudu ya kufa mtu. Swali ni tunaishia hapo au tunajifunza?

We si Onani, usikojoe nje.😄 mnapaisha sana wanangu ……..
We si Daudi, acha wake wa watu.
We si Kaini, acha wivu wa kijinga.
Na kama ulikuwa Rahabu, bado Mungu anakutumia mtaa hii.

Tujitume kuijenga jamii, tukianzia na sisi wenyewe. Sio lazima uwe mtakatifu, unahitaji tu kuwa real na kujaribu kubadilika kidogo kidogo.

Mwisho wanangu ehhh ,Naomba kuuliza... hivi hizi sikukuu za kidini mlikubaliana kuzigeuza homecoming za tumboni ama? Pasaka inamaanisha kufufuka kwa roho nyie mmefufua vyakula, vicheko, na vichupa hadi havina tena heshima. Yaani wengine Pasaka hii wamebugia P2 , nkiri wazi roho zao hazijafufuka, tumbo ndilo linafurahia.


~Chavalikungu
 
Back
Top Bottom