Unajenga barabara juu ya maji wakati ndani ya nchi kwa mfano Arusha -Kiteto barabara ni mbaya sana kuna gari moja tu

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,522
7,030
Ukipitia barabara ya Arusha-Kiteto(Manyara) kupitia Orkesumet(Simanjiro) ni mbaya sana, basi linajaa kuanzia Arusha ni kukanyagana ni afadhali miaka kabla ya uhuru.

Upande wa pili barabara zinapita juu ya maji njia 4 Km 3.2 ndani ya nchi ile ile. Niliumia sana na kuwashangaa wamasai.

Bado kuna TANZANITE, KIGAMBONI. Nchii hii kuna ubaguzi mkubwa sana, nenda wilaya ya Mbulu iliyoanzishwa tangia mwaka 1905 ambayo leo ni wilaya 4 za Babati, Hanang, Mbulu na Karatu hakuna barabara kufikia makao makuu ya wilaya ya Mbulu. Nchi iko vipande×2

Soma Pia: Luhaga Mpina: Kuna viashiria vya ufisadi katika mikataba ya Ujenzi wa miradi 7 ya barabara (2035km) kwa utaratibu wa EPC+F
 
Remember resources are limited we need to priotize our priorities kwahyo viongozi wako waliona kujenga madaraja ni best optional kuliko barabara lkn ata hvyo madaraja lazma yaunganishwe na barabara. So just be calm ur time will come.
 
Umenikumbusha Orkesumet mitaa yangu enzi nalima huko na lile libasi moja mnajazana na wamasai kama nyanya. Linakimbizwa balaa. Mitaa ya Nabelela. Cha ajabu kule ni karibu sana na arusha mjini lakini unalazimika kutembea masaa sita tena kwa mwendo mkali sababu barabara mbovu na mashamba yote yale na madini ule mlima Nabelela ni madini tupu bado kuna njia ya kutokea kondoa na inaunganisha mpaka wilaya ya Kilindi. Sielewi waafrika tuna matatizo gani.
 
Wamasai ni jamii inayosahaulika sana.

Hapo Arusha mjini penyewe hakuna stand ya mabasi na afcon ipo njiani kuja.
 
Wamasai ni jamii inayosahaulika sana.

Hapo Arusha mjini penyewe hakuna stand ya mabasi na afcon ipo njiani kuja.
Tatizo washajizoelea kukaa mwituni wao kutembea kilomita 200 sio ishu kabisa cha muhimu ng'ombe ana malisho. Hilo ni tatizo huwezi kusikia wanaomba mabomba ya maji au lami au hospital maana wanajitibu na mizizi. Shida ipo hapo so wanaojitambua ni wachache.
 
Daah uneongea kitu ambacho niliwahi kuwaza siku moja nilipoenda huko Simanjiro ila nilikua na Pick up nilishangaa sana eneo lenye Mali vile lakini ishu ya bara bara halipo kabisaa Bus za kiteto wanapakia Mbuzi,kuku kwenye boot la gari pamoja na mazao humo humo hao abiria wanaoshuka hapo ni kama waketoka kwenye machimbo ya madini aisee ila asilimia kubwa ya chakula cha Arusha na Nairobi hasa kwa mahindi yanatoka hayo maeneo...kipindi cha mvua ni Land Rover tu au Nissan ndio zitaweza kufika baadhi ya maeneo ya kule.
 
Iko hivyo sehemu kubwa ya Nchi sio Simanjiro pekee.

Hapo Sasa ndio anzeni kushangilia SGR
 
Iko hivyo sehemu kubwa ya Nchi sio Simanjiro pekee.

Hapo Sasa ndio anzeni kushangilia SGR
Bara bara ya Tabora inayounganisha Mbeya bado ni vumbi na inasababisha ajali sana kwa hizo Bus za AN na jamaa zake bus linakimbia na fusso nayo imepakia zaga zake inakimbia kwenye bara bara moja ambayo kupishana gari moja inatakiwa lisimame huko na Vumbi la kutosha juzi limeanguka hilo AN na kuua baadhi ya abiria kisa bara bara mbovu na magari machakavu ambayo inabidi yapite huko..
 
Unatumia Trilioni 11 kujenga miundombinu ya reli ya umeme ndani ya km 722 tuu wakati 3/4 ya Nchi imejaa Barabara za matope ambapo hizo 11T zingepunguza tatizo Kwa zaidi ya 1/3.

Akili za mtu mweusi hizo.
Uchumi hauko hivyo. Lazima kupima economic Impact ya mradi. Kwa hili la mradi wa reli nakupinga. Kuwepo kwa SGR kuta boost secta ya usafirishaji na uchumi wa nchi hivyo kuwa na fedha za kuleta maendele sehemu nyingine. Kupanga ni kuchagua

Wewe mwenye unaweza kuwa na pesa kidogo ukaamua kusomesha watoto kwanza kabla ya kujenga nyumba ya kuishi. Watu hawatakucheka kwanini unasomesha watoto wakati hauna nyumba.
 
Magari yanayokatiza kigamboni na kulipa ushuru kwa siku huwezi kulinganisha na magari yote yanayopita mkoa wa Manyara kwa Mwezi.
Labda uzungumzie daraja la Busisi sijui kama litakuwa na faida kama inavyotarajiwa. Lile lingejenga Kilomita nyingi za lami.
 
🚮🚮 Huwezi hata kuweka uthibitisho wa namba Kwa uliyoongea.

Kupanga ni kuchagua ndio mumechagua ujinga huo?
 
Magari yanayokatiza kigamboni na kulipa ushuru kwa siku huwezi kulinganisha na magari yote yanayopita mkoa wa Manyara kwa Mwezi.
Labda uzungumzie daraja la Busisi sijui kama litakuwa na faida kama inavyotarajiwa. Lile lingejenga Kilomita nyingi za lami.
Wanalipishwa kwa sababu ya qliyetoa hela kujenga ni Pension Fund ila kama lingekuwa limejengwa na serkali bila ufadhili. wasingelipia na JPM bridge nadhani patakuwa kupita ni bure tu!
 
Ukabila mbaya na umoja wa kipumbavu waulizeni wawakilishi wenu bungeni mtu anachaguliwa zaidi ya miaka 30 mpk anakufa hajawai changia hoja ht moja na anachaguliwa tn na tena wengine chid ni jdi yao bn
 
Back
Top Bottom