Unaishi vipi na mwanamke wa aina hii?

sizonjemadawa

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
1,053
1,304
Habarini,

Kwa wale wenye uelewa wa saikolojia au uzoefu wa mahusiano bila kuangalia umri wako, ili mradi usiwe mario.

Ni mwanamke anayeonekana ana mawazo kila saa, anafurahi dk 5, anakaa kimya dk 20, ananuna dk 40, ana maamuzi ambayo hajali kama yatakuumiza au yatakufurahisha, ni mtu wa kusimamia misimamo yake bila kuangalia madhara yake, anachoamua hicho ndicho atakachokifanya hata kama utamwambia madhara ya hicho kitu.

Mtu ambaye hapendi kabisa kelele za aina zozote zile, ila ni mtu anayeonekana ana mapenzi ya kweli, japo ni msiri, ukimuuliza una tatizo gani anasema hana, anaamini mambo yake atayamaliza mwenyewe, akisema hapana basi hawezi badilisha hayo maneno, hachelewi kughairi na akighairi basi ujue imetoka hiyo, ni mkali, hapendi kwenda sehemu yoyote ya kufurahi (out) anapenda kukaa ndani tu muda wote, anapenda kukaa peke yake mda mwingi.

Ni msichana mzuri, kila mwanaume akimuona basi atampenda.
 
Wanawake walio wengi na haswa walio bahatika kupata Elimu kidogo kuanzia level ya Degree 1 wamekuwa na misimamo sana ila ukimpata huyo cha msingi ni kumuonyesha msimamo wako mapema kwa kadiri iwezekanavyo...Maana ukiyumba kidogo inakula kwako mazima...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…