comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Toka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweke ukomo wa mtu kukaa kwenye nafasi ya urais kwa miaka 10 kwa vipindi vya miaka 5, mgombea wa CCM aliye na stahiki ya kugombea mhula wa pili baada ya kumaliza mhula wa kwanza hashindanishwi na wenzake ndani ya chama chake. Ilikuwa hivyo toka kwa Ali Hassan Mwinyi mwaka 1990; kwa Benjamin William Mkapa mwaka 2000; Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2010; kwa John Pombe Joseph Magufuli mwaka 2020, na kwa mantiki inapaswa kuwa hivyo kwa Samia Suluhu Hassan mwaka 2025.
Hoja kwamba samia hajawahi kuchaguliwa
Mh. Samia Suluhu Hassan achaguliwa sambamba na John Pombe Joseph Magufuli mwaka 2015 na 2020 akiwa mgombea mwenza kwa mujibu wa ibara 47 (2) inayosema:-
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.
Kupatika kwa Samia Suluhu Hassan ni kwa mujibu wa ibara 47 (3) inaysema:
(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
Soma Pia: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
HOJA YA URAIS WA SAMIA
Mh. Samia Suluhu Hassan alikuwa rais kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano inayosema ilitokea nafasi ya rais kuwa wazi kwa sababu zilizobainishwa basi makamu wake wa rais ataapishwa kuwa rais.
SAMIA ANASTAHILI MHULA WA PILI AU URAIS WAKE UNAISHA 2025 PALE JPM ANGEKOMEA
Majibu ya maswali haya tunayapata kutoka ibara ya 37 (5) inayotaja sababu zinazoweza kuifanya nafsi ya urais kuwa wazi. Ibara ya 37 (5) ina sema:
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.
Mwaka 2021 Tanzania tulipoteza rais wetu John Pombe Joseph Magufuli na kwa mujibu wa Katiba Makamu wake aliapishwa kushika nafasi yake. Ibara ya 40 (4) inafafanua mstakabali wa na stahiki za Samia Suluhu Hassani na urais wake kwa kusema:-
(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Kwa mujibu wa ibara ya 40 (4) Samia Suluhu Hassani aliachiwa urais kukiwa bado na zaidi ya miaka 3 hivyo anastahili kugombea nafasi ya urais mara moja tena.