Unafiki na chuki zinadhihirika katika migogoro ya kimataifa

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
11,725
25,521
Moja kwa moja.

Nimeona nije na mada hii baada ya kuona huu uzi leo Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa! nikakuta za comments mbalimbali.

Nije katika hoja, kwamba mnasema football haipaswi kuchanganywa na siasa na mambo mengine kinyume cha football pamoja na kutoa povu kwa Azam Tv, sasa mbona Ulaya kwa wenye soka hilo jambo lilifanyika waziwazi na hamkujitokeza kupinga?

Nije katika mifano mgogoro wa Urusi na Ukraine tulishuhudia vilabu vikubwa Ulaya, wachezaji nk, waliweka wazi misimamo yao na hakuwa na shida wala chuki kama za baadhi ya wabongo wapuuzi haswa wa humu JF?

Picha za kusapoti uzi.
images (72).jpeg

IMG_20231021_120409.jpg

Football haipaswi kuchanganywa na mambo mengine ila ikiwa kwa Ukraine na Mshoga ni fresh, Palestine ndio hawatakiwi? Nataka mseme bado hamjasema.
images (70).jpeg

Uzi bado Unaendelea..

Cc : Maghayo yoga and others
 
Wadhamini huku mada ikiendelea :Kombe la Dunia jamaa shoga katimba uwanjani na bendera ya ushoga na Shati la kusapoti Ukraine.
images (71).jpeg
 
La Liga mwaka jana katika DSTv walikuwa wanashow flag ya Ukraine ila Azama ni coverage ya tukio bila wao kusema wanasapoti wapi watu wameibuka na chuki na unafiki.
 
Na hapo Kongo DRC kwa mwezi tu wanakufa maelf ya watu,ila huwezi sikia chochote hata Media hazisemi kwasababu wananufaika sana na Mali za hapo,ila unasikia mtazania wa Gezaulole anasema pray for Palestine AU Israel.....huyo huyo hujawahi msikia labda kuusemea mgogoro wa Sudan hapo tu karibu............Watu wanaokufa Africa ni wengi kuliko hata hao tuonajifanya kuwaonea huruma lakini bado fikra zetu zimetawaliwa sana
 
Wadhamini huku mada ikiendelea :Kombe la Dunia jamaa shoga katimba uwanjani na bendera ya ushoga na Shati la kusapoti Ukraine.View attachment 2788126
Mtu kama huyu hajaingia hapo Kwa bahati mbaya,hii planned kabisa.......lingekuwa ni jambo la kuwachukiza hata camera zingemkwepa ila kwasababu ndiyo target yao inakuwa wengi waone ndiyo shida inapoanzia.....hapo huoni hata Stewart wakimfukuzia
 
Kwa hiyo mtoa hoja ulitaka palestina isapotiwa kwenye huo uzinduzi wa ligi mpya kupita azam tv, unajitoa ufahamu hujui kuwa kuna wanaoisapoti israel na wanataka kuonesha hivyo. Kuhusu kuonesha mambo na alama za ushoga kwenye mambo ya mpira, mpira una wenyewe ufahamu hilo we mtoa hoja na ili uelewe hilo kwa kina nenda kasome kitabu cha mazito duniani yenye utata kiitwacho HOW THEY STOLE A GAME kilichoandikwa na mwandishi wa habari za uchunguzi aitwaye David Yallop. Mpira una siasa nyingi na hutumika kupitisha ajenda nyingi duniani
 
Mkuu urokole uchwara unao ibuka kwa kasi ndani ya nchi hii ni hatari sana usipo dhibitiwa, maana wafuasi wa haya makanisa ya kirokole waumini wake wamejaa chuki isiyo na sababu yeyote dhidi ya uislam.
Na wakristo wengi wa humu jf ni wafuasi wa haya makanisa uchwara.

Hiyo mada haijaletwa kwa lengo lingine zaidi ya chuki za kipumbavu dhidi ya waisilam.
 
WAAFRIKA ni viumbe WAPUUZI….

Watu (45,000) wanafariki kila mwezi katika ardhi ya DR Congo kwa sababu ya vita…. Watu 2,000 na ushee israeli na Palestina imekuwa wimbo wa Dunia na waafrika wanaimbishwa pray for this and that..

Utafiti wa International Rescue Committee (@RESCUEorg) unaonyesha watu milioni 5.6 katika miaka 9 pekee (kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2007) walifariki kutokana na vita DR Congo.

Huo ni wastani wa vifo 1,500 kwa siku, lakini sio habari kubwa kwa waafrika. Kwa maana nyingine ni kwamba, kuanzia mwaka 1998 hadi 2007, kila siku DRC kuna vifo vya idadi ya watu karibu sawa hao waliofariki huko Israeli na Palestina

Raia wengi wa DR Congo wanafariki kutokana na kukosa huduma za kijamii kama hospitali, magonjwa mengi ya milipuko na kuambukiza, njaa kutokana na kukosa makazi na utulivu, hawazalishi.

Vita, ukoloni, utumwa, ufisadi yamebadilisha taifa hili ambalo licha ya kuwa miongoni mwa mataifa tajiri zaidi duniani, sasa limekuwa masikini zaidi. DR Congo imebarikiwa kila aina ya madini.

DR Congo nchi tajiri zaidi duniani kwa maliasili. Madini mengi ghafi hayajatumika yenye thamani ya hadi takriban $24 trilioni. Huu ni uchumi wa USA na Ulaya kwa pamoja.

Kuna aina zaidi ya 1,100 za madini katika ardhi ya nchi ya DR Congo. Amana hizi ni pamoja na akiba kubwa zaidi ya madini ya coltan na kiasi kikubwa cha madini ya kobalti.

80% ya ardhi ya DR Congo inafaa kwa kilimo. DR Congo ina eneo sawa na Ulaya Magharibi. Ulaya Magharibi ni England, France, Germany, Italy, Netherlands, Spain, Portugal, Belgium, Austria.. etc.

DR Congo ina hazina ya 10% ya hifadhi ya shaba Duniani. 30% ya cobalt ya Dunia. DR Congo inazalisha 80% ya madini ya coltan yanayotumika kutengeneza simu, ipods, sumaku, Jet engine.

DR Congo inazalisha madini ya Uranium. Vita ya pili ya Dunia, Marekani alipiga miji miwili ya Japan (Hiroshima na Nagasaki) kwa mabomu ya atomic. Mabomu yalitengenezwa na madini ya Uranium.

DR Congo inamiliki ardhi ambayo inatoa madini ya almasi, dhahabu, bauxite, graphite, fedha, zinki. Pia wanayo madini ya lead ambayo yanatumika kutengeneza risasi na mabomu.

DR Congo ina ardhi yenye mafuta. Kuna misitu mikubwa yenye miti mikubwa. Wanyama, vivutio vya watalii katika milima ya Virunga na Ituri. Mito na mabonde yenye unyevu na rutuba. Maziwa na bahari.

Mto Congo ni mto wa pili kwa ukubwa Duniani. Kuna maporomoko (Inga Water Falls) ambayo yanaweza kuzalisha umeme wa kusambazwa Afrika na Ulaya kwa wakati mmoja.

Makundi yenye silaha ya M23, ADF, FDLR, CODECO, RED-Tabara na wengine yamesababisha majanga ya kibinadamu na ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia.

Tangu kuibuka upya kwa kundi la M23 mwezi Novemba 2021, ‘Zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kukimbia makazi yao. Hili ni kundi linalofadhiliwa na serikali ya Rwanda chini ya Rais Paul Kagame.

Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo limelaaniwa kabisa na utajiri wake wa madini hayo. DR Congo ni ulimwengu usio na matumaini kwa raia wake. Ni jehanamu kwa wananchi wake.

DR Congo yenye raia 75 milioni, asilimia 80 ya raia wake, sawa na 60 milioni wanaishi chini ya kipato cha dola moja (Sh2,500). Umoja wa Mataifa wanaeleza, zaidi ya watu milioni 5.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula DRC

Wageni kutoka nje ya DR Congo wamevamia ardhi na kuifanya uwanja wa mapigano na mavuno ya rasilimali za watu wa Congo. Watu wa DR Congo wamebaki kuwa maskini wa kutupwa.

Wageni wamesababisha machafuko, wamevuruga utaratibu wote wa uchumi, wameiba mali nyingi za nchi ya DR Congo. Wananchi wa DR Congo wamekimbia makazi yao sasa ni wakimbizi.

Machafuko yanaifanya DR Congo kuwa nchi tajiri kwa rasilimali Duniani lakini taifa maskini zaidi Afrika wakati mataifa ya magharibi yakiendelea kunufaika na vita ndani ya DR Congo.

Wanaosababisha vita DR Congo ni mabeberu wanaoleta silaha za kivita na misaada ya kijeshi wao wanachimba madini na kupeleka kwao. Tuwaambie Acheni kupora mali ya DRC! Ondoeni mikono yenu DRC!

Hupati waafrika au watanzania wanafunga na kuomba kwa ajili ya nchi kubwa Afrika ya DR Congo. Utawasikia wakichakarika na Pray for Ukraine, Pray for Israeli, Pray for Palestina. DR Congo haikumbukwi.

MMM, Martin Maranja Masese
 
Huko mbali sana Hatukuona bandiko/habari hata kwenye mechi kubwa hapa ndani ya kutetea hata ndugu wamasai au kwavile sio ndugu zetu katika imaan?
 
Wale wamisri walinyanyua mabango kuwatetea waarabu wenzao, sasa mimi Muha wa kasulu kigoma eti ni pray sijui for Palestina au Israel, kwanza hata hawaijui Tanzania ni kitu gani au wanawajua Waunguja wa kidongo chekundu?
 
Kwa hiyo unadhani.., Israel angevamia DR Congo kisha akafanya hicho anachowafanyia Wapalestina,...Watu wangekaa kimya?!!

Hakuna taifa linalostahili kuonea taifa lingine,...hata DR Congo ingevamiwa na kufanyiwa kama yanayoendelea huko Palestina Watu wenye mioyo ya utu wangepaza sauti zao tu.

Lakini pia kumbuka case ya Congo na Palestina ni tofauti kabisa.
 
Umemaliza kila kitu, atakaeandika tena ni bada kichwani
 
Back
Top Bottom