Una swali lolote kwa Waziri wa Habari, Dk. Harrison Mwakyembe? Atakuwa live Star TV kuzungumzia Sekta ya Habari na janga la Corona, uliza hochote

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,124
120,357
Wanabodi,

Je, una swali lolote la kihabari, kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Dk. Harrison Mwakyembe?

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Dk. Harrison Mwakyembe, kesho asubuhi, kuanzia saa 1:30-3:00 atakuwa live kujibu maswali yako, kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, Kinachorushwa na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi.

Unaweza kuulizwa swali lako hapa na litamfikia, au unaweza kuuliza direct hiyo kesho, kwa wakati wa live.

Sasa ili ku-maintain focus, ningeomba maswali tuyagawe katika mafungu matatu
  1. Maswali ya sekta ya Habari, yaani maswali ya Kihabari
  2. Maswali ya sekta ya Michezo, yaani maswali ya Kimichezo
  3. Maswali ya sekta ya Sanaa na Utamaduni.
Kwa vile kipindi ni dakika 90 tuu, hatutaweza ku cover sekta zote, hivyo kwa kesho, na kwa vile michezo sanaa na utamaduni zimesimama kutokana na janga la Corona, nashauri kwa kesho tujikite tuu kwenye maswali ya sekta ya habari, nitamtafuta tena aje kujibu maswali ya sekta ya michezo, kisha nitamshauri amruhusu Naibu wake, Mhe. Juliana Shonza, aje tumuulize maswali ya Sanaa na Utamaduni.

Naomba maswali yawe mafupi, brief, direct, concise, short and clear, questions, no beating around the bush, ili tuweze kumuuliza maswali mengi, na yeye aweze kujibu kwa ufasaha.

Karibuni.

Pascal
Update
Saa hizi Dr. Harrison Mwakyembe yuko live saa hii.


P
 
Miongoni mwa posti za kijinga ni pamoja na hii. Yani ummulize mwakyembe swali lolote wakati unajua wazi hawezi kujibu lolote. Bora ungesema mafuguli yupo live tumuulize anajisikiaje juu ya wakuu wake wa distrikit wanavyopukutika na Covidi huku yeye akiwa amejificha chota
acha nicheke tu.
Mwambie Mwakyembe kwenye inshu za mpira aache kutuvuruga, akomae na utamaduni huko



"Not everything is for everybody"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TBC ni chombo cha habari cha Umma ama ni cha serikali? Na ni kwa nini habari za kisiasa zinazopewa kipaumbele kwa asilimia 99.99 ni zile zinazoonesha mambo chanya ya CCM na mambo hasi ya vyama vya upinzani hasa CHADEMA?

Je, ni sawa kwa TBC kuonesha kila siku mambo yaliyofanywa na CCM kupitia serikali bila ya kuwapa wapinzani nao nafasi kutoa maoni yao kuhusu mambo hayo hayo? Kwa mfano ujenzi wa miundo mbinu. Sekta ya Afya, Nishati? Jee hapo TBC inakuwa ime- balance story?

Shughuli za CCM nazo ni shughuli rasmi zinazotakiwa kuoneshwa na TBC? Kigezo cha kuonesha shughuli mbali mbali za CCM huku za CHADEMA zipuuzwa ni nini? Yaani kwa nini Hotuba za viongozi wa CCM na wakiwa kwenye shughuli zao mbali mbali kama vile Humphrey Pole pole na Bashiru Ally zinaoneshwa mara nyingi sana huku za vyama vingine hazioneshwi?
 
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi na mashirika mbalimbali duniani pamoja na nchi kama marekani kuhusu haki za wana habari hapa Tanzania inadaiwa kuna ukamataji wa wanahabari usiwo wa haki unaofanywa na serikali (kunyima uhuru wa habari)

Pia kumekuwa na matukio ya kupotea wana habari je yeye kama waziri ana lipi la kusema? na amechukua jitihada gani kushughulikia swala hili?
 
Na hili...

Je, ni kweli tauni hii imeongeza chachu kwenye kuongezeka na propaganda, hasa mitandaoni na kuficha uandishi ambao ni "fact based"?

Kama CD alivyonena " kuwa tauni hii inaonyesha uporomokaji wa kupata habari sahihi"
Je, kuna ukweli wa hayo? hata kutoka serikalini?
 
Miongoni mwa posti za kijinga ni pamoja na hii. Yani ummulize mwakyembe swali lolote wakati unajua wazi hawezi kujibu lolote. Bora ungesema mafuguli yupo live tumuulize anajisikiaje juu ya wakuu wake wa distrikit wanavyopukutika na Covidi huku yeye akiwa amejificha chota
Alafu hili bandiko lilitakiwa kuletwa na kurugenzi ya mawasiliano ya Habari ya wizara anayoiongoza mwakyembe,niaibu kujipa jukumu lisilo lako,kwani japo na wewe kama utakuwa star TV,bado unabaki kuwa mgeni mwalikwa kama alivyoalikwa Mwakyembe.jitaidi nafasi imebaki ya mwisho,wilaya ya Nyanhwale ipo wazi.
 
Pascal Mayalla,
Nawapa pongezi kwa kuanzisha Chanel ya utalii. Lakini wana mkakati gani wa kuanzisha chanel ya michezo, Tbc sports ambayo iwe na mamlaka ya kuonyesha ligi mbali mbali za ndani na nje ya nchi. Maana Azam Tv wamefanya ukiritimba kiasi kwamba kama huna dish la Azam huwezi kutazama ligi za hapa ndani.
 
Pascal Mayalla,

Kuna kesi ilifunguliwa Mahakama Kuu na kisha Mahakama ya Rufaa ikipinga vifungu kadhaa vya Sheria ya Vyombo vya Habari, lakini hukumu ya mwisho iliyotolewa ikatupilia mbali madai kwamba sheria hiyo inakandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini. Kisha waliofungua kesi walienda Mahakama ya Afrika Mashariki na mahakama hiyo ikatoa hukumu Machi 28, 2019 ikisema vifungu kadhaa vinakandamiza uhuru wa habari na mahakama ikaielekeza serikali ya Tanzania kuvirekebisha. Outcome ya hukumu hii ikoje? Je, serikali ilikata rufaa au ili'comply' na ruling hiyo?
 
Bunge mubashara kwenye luninga lini? Kuna maswali bado hayajajibiwa na afya (Mh ndugulile na Abbas), walitawala mjadala, ukawa msiklizaji.
 
Back
Top Bottom