Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 26,933
- 19,448
Ndugu zangu Watanzania,
Umoja wa ulaya umeipatia Tanzania Msaada wa Billion 97,Ambazo zitatumika katika maeneo matano ,ambapo miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na uboreshaji wa maendeleo endelevu katika Miji kama vile Kwanza,Tanga na Pemba.
Lakini pesa hizo zitatumika pia katika kuwawezesha wanawake na ushiriki wa wanawake hususani katika masuala ya uongozi.
Huu ni Muendelezo wa kuonyesha Imani kubwa ambayo Nchi ,jumuiya,Taasisi na mashirika mbalimbali yamekuwa nayo kwa nchi yetu tangia kuingia madarakani kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Sasa tunaendelea kupokea na kupata ushirikiano kutoka kila pembe ya Dunia.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.