Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 153
- 425
Niger, Mali na Burkina Faso ambazo zinaunda umoja wa nchi za Sahel ( AES) zinatarajia kuanzisha kikosi cha pamoja ili kupambana na magaidi.
Hayo yalibainishwa na waziri wa Ulinzi wa Niger Jenerali Salifou Modi mnamo tarehe 21 Januari 2025 wakati wa mahojiano yaliyorushwa na Televisheni ya Taifa ya Niger( RTN)
Kikosi hicho kitakuwa na askari 5000 watakaotoka katika nchi zote tatú wanachama na kitakuwa na bajeti yake inayojitegemea kwa ajili ya intelijensia, ulinzi wa anga pamoja na ardhi. Pia, kikosi hicho kinatarajiwa kuwa tayari kuanza majukumu yake hivi karibuni.
Niger , Mali na Burkina Faso zilitangaza rasmi kujitoa kutoka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika ( ECOWAS) mnamo Januari 29 2024 huku sababu mojawapo iliyotajwa na viongozi wa nchi hizo ni ECOWAS kutotoa msaada kwa nchi zinazokumbwa na tishio la ugaidi.
CHANZO: RTN Social media Pages