GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumpa heshima kubwa ya kuwa, Waziri wake kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu akiitumikia nafasi ya Waziri wa TAMISEMI na baadaye Wizara ya Afya huku akisema ameyapokea mabadiliko hayo kwa moyo mkunjufu na kwa moyo wa shukrani.
Ummy ametoa shukrani hizo wakati akiongea kwenye mkutano wa ndani katika ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, ambaye ni Mlezi wa kichama katika Mkoa wa Tanga.
Chanzo: ITV Tanzania
Ungeuchuna kama Wenzako akina Makamba na Nape tungekuelewa, ila kwa Kujitetea huku ina maana Umeumia!
PIA SOMA
- Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya