Umewahi Kupitia Kadhia Hii?

ipi umepitia hapo Dragon
Mkuu nimepitia sana hiyo ya kandambili, tena nakumbuka nimesoma shule ya msingi nikivaa kanambili, enzi hizo ukivaa kandambili shuleni unaonekana wa kishua. wengi walienda shuleni pekupeku. Hizo za matairi ya gari (katambuga) nimevaa pia, hasa tukienda machungani kuchunga ng'ombe, miiba haioni nyayo. safi sana
 
mwili umeingia baridi hapo
 
Mkuu nakumbuka enzi hizo anaevaa viatu ni mtoto wa mkuu wa wilaya, mtoto wa meneja wa benk na mtoto wa mwalimu mkuu. shule nzima ukihesabu wenye viatu hawazidi wanafunzi 20
hadi leo ukienda na viatu kijijini kwetu unapata cheo
 
Hiyo ya pasi mpaka leo mimi naipitia kutokana na ukatikaji wa umeme hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…