Habari wadau, nitangulize salamu
Ni Mwezi sasa au zaidi nimekuwa nikiona na kusikia malalamuko ya baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook akaunti zao kudukuliwa na watu wasiojulikana (hacker) kisha wahusika hao kuposti maudhui yao ikiwemo ambayo yanaenda kinyume na Sheria na utamaduni wetu.
Changamoto hiyo imewakumba watu wengi ikiwemo watumiaji maarufu wa mtandao maarufu kwa Tanzania, hali hii inasikitisha kwa sababu imekuwa ikipelekea kutia doa hadhi ya watu kutokana aina hayo ya maudhui ambayo yamekuwa yakichapishwa.
Najiuliza mamlaka zinawasaidiaje Watu hao wanaokutana na hizo changamoto hasa kutoa elimu ya kujikinga na udukuzi wa aina hii na je, wanachukua hatua zipi kuripoti matukio hayo kwa wahusika, kwa sababu wanaokumbana na changamoto hii wanaendelea kuongezeka siku hadi siku.
Maudhui hayo yanayochapishwa baada ya udukuzi huo yanaathiri pia jamii ya mtandaoni ambayo imekuwa ikikutana na maudhui hayo ikiwemo picha za utupu.
View attachment 2931120View attachment 2931121View attachment 2931122
View attachment 2931123
Sent from my Infinix X665 using
JamiiForums mobile app