Umeme wa jua kuongeza unafuu Shinyanga

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,409
904
UMEME WA JUA KUONGEZA UNAFUU SHINYANGA

Mradi wa umeme wa jua unatekelezwa katika Wilaya ya Kishapu Mkoani wa Shinyanga unaendelea ambapo kwa awamu ya kwanza mradi unatarajiwa kuzalisha Megawati 50 na baadae Megawati 100 kwa awamu ya pili zitakazoongezeka na kufanya jumla ya Megawati 150.

Utekelezaji wa mradi huu kwa awamu ya kwanza umefikia asilimia 57 na unatarajiwa kukamilika kufikia mwishoni mwa Mwaka 2025.

Mradi kwa ujumla unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 275.

FB_IMG_1743326135062.jpg
 
Sijui, nijuavyo mimi garama za ujenzi wa vyanzo vya umeme ni kubwa sana, nimebahatika kuingia Kidatu hydro power na umeme unaozalishwa pale ni mgw 200 tu, ninaogopa sana hizo mgw 50 itakua ni mabioni ya fedha mpaka mradi kukamilika.
Kijiografia naona kama manyara na Shinyanga kupitia Serengeti au Maswa inaweza kuwa karibu zaidi na tukaokoa pesa nyingi kwa kutumia umeme wa muethiopia utakaokuwa umefika pale manyara, ni mawazo yangu tu
 
Huu mradi ni watu binafsi au Serikali na kama ni Binafsi wanapanga kuwauzia UMMA kwa kiasi gani kwa unit ? Ukizingatia Umeme huu ni intermediate na sio continous (Kutunza Umeme bado ndio kikwazo kuzalisha tu tena katika nchi ya kitropiki wala sio tatizo)

Na kama mradi ni wa Kodi zetu na tunaambiwa huku umeme upo za ziada ingawa kule karibia na mpaka wa Kenya kuna uhaba na kusafirish huu kuutoa hapa mpaka kule mwingi unapotea kutokana na miundombinu, Je isingekuwa busara kutengeneza miundombinu ili kufikisha huu unaopotea kwa gharama nafuu na sio kununua kutoka nje ?

Hilo eneo la solar farm si bora lingefanyiwa huduma nyingine ukizingatia hizo solar panels tunaweza kuweka katika majengo na kuunganisha kwenye grid ?

Naona kama motive ya mengi tunayofanya ni kupata political mileage and filling people's coffers na sio kuhudumia mwenye nchi ambaye ni mwananchi..., Case in Point..

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom