UMEME 'KUSHTUKA', TANESCO WATUPE UFAFANUZI...

EMACHA

JF-Expert Member
Jul 16, 2021
582
1,100
Nimetumia neno 'kushtuka' kwa sababu huu si ukatikaji wa umeme uliozoeleka.
Kwamba kwa siku za karibuni nimeshuhudia umeme ukikata na kurudi kwa sekunde moja au mbili; na hii imetokea zaidi ya mara tano katika kipindi cha saa 12. Hali hii nimeishuhudia nikiwa nimejituliza nyumbani siku ya jumanne tarehe 10/09/2024 na jumatano tarehe 11/09/2024. Sasa ni vema TANESCO wakatueleza ni nini hiki kinatokea; maana wengine wanadai kuwa tuna umeme mwingi wa kupitiliza kwa hiyo miundombinu inazidiwa nguvu...!
 
Hii ni shida ya mitambo. Wamemaliza ishu ya kua na umeme wa kutosha, sasa warekebishe na mitambo
 
Sizani Kama watakuja kukujibia hapa Ila kwa uelewa wangu mdogo
TANESCO wamefunga vifaa Kinga kwenye line zao AUTO RECLOSER aambapo kazi yake ni kujizima na kujiwasha automatic
Kwa mfano hujizima tu pale panapotokea short ya mpito kwenye line Kama ndege kugusa nyaya kusababisha kupigwa short au tawi la mti kugusa na kuachia nyaya Hii huwa unafanya auto RECLOSER kujizima na kujiwasha ndani ya muda mfupi itategemea na setting ya hicho kifaa na Kuna short ya kungangania Kama nguzo kudondoka na kusababisha nyaya kugusana Hii huwa kinajizima na kujiwasha mpaka mara tatu au nne Kama vile mtu anachezea switch n ahatikaye kukatika kabisa kwa umeme hiyo ndio inawapa indication kwamba Kuna tatizo kubwa

KWA UELEWA WANGU UNAISHIA HAPO KEA MEENYE NYONGEZA ANAWEZA KUJAZIA JAZIA HAPO
 
Back
Top Bottom