Ulisoma english medium au shule ya serikali? Na nini unakumbuka kuhusu shule yenu?

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,722
4,714
Kwa uelewa ulionao sasa, unafikiri ungesoma shule tofauti ingekusaidia kwenye maisha, ajira au biashara?

Je, watoto wako watasoma shule kama uliyosoma wewe au utawapeleka kwingine?

Binafsi nimesoma shule ya msingi ya serikali, mkoani Tabora. Nakumbuka nilikua na eneo langu la bustani la kumwagilia na kusafisha kila asubuhi, walimu walikua wakarimu sana na nilifurahia shule.
Vifaa vya darasani vilikua duni, bado nina kovu kubwa pajani la kukatwa na viti vya chuma vilivyokua vimechakaa.

Sekondari nimesoma shule ya private, tulikua tunachagua vyakula na kutengeneza meal plans kila term.
Watoto wangu wamesoma EM, kwa sababu baba yao alitaka wasome huko.


CC:
Nomadix
makutupora
realMamy
Mallerina
 
Me nakumbuka nikiwa school PRESIDENT 😊🙏
Her majesty
Madam President
giphy.gif
 
Nimesoma shule za Sekondari kuanzia Msingi Mpaka Advanced Level..

Nimesoma;
1. Borenga Shule ya Msingi, Serengeti Mkoa wa Mara.
2. Kwata Shule ya Msingi, Korogwe-Tanga
3. Mwenge Shule ya Msingi-Dodoma vijijini.
4. Nyanza S/M Mwanza

Hizo ni Shule za Msingi nahama hama
Mkuu rudia kusoma ulicho andika
 
Nimesoma kayumba 3 S/Msingi, nikahamia EM kuanzia darasa la 5-7.
Kayumba imenifundisha uwajibikaji kufagia eneo langu,kuwahi shuleni,kuishi kijamii bila ubaguzi.
Sema kuombana kulikuwa kunaboa, umenunua zako barafu/mihogo mikono kama 20 ishafika "Noma naomba hata kadogoo, naomba aya sitakupa barafu yangu"
unagawia wenzako unakula kadogo, mixer kulamba barafu yote ili usiombwe, but kayumba was fun.

EM ilikuwa poa sana kwanza tuko wachache, miundombinu imara, library ina maencyclopedia kama 200. EM vitoto vinaringa kinoma kuna pisi nilikubali naitafuta mpaka sahivi inaitwa Winnie kama upo humu jitokeze.

Kuanzia sekondari ya awali mpaka sekondari ya juu nimepiga kayumba, wana na wadada wako peace.

NB: Me ni mtoro konki toxic mtoro, nishawahi kufatwa na Discipline,Academic, na Biology teachers home wakisema niende skuli baada ya kukaa utoro 2months.

Nikiripoti kutokea makao makuu ya Kataa Ndoa hapa Jupiter
mimi ni Nomadix, you can call me Noma
Kwenu studio
 
Back
Top Bottom