Ulishawahi kukataliwa kwasababu hukuwa na kitu kisha ukaja kukubaliwa baada ya kupata?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,571
35,472
Sababu mbalimbali,

Anakukataa kwa dharau Sana, kwa sababu anakuona tu kwamba huna chochote kwa wakati huo kwa sababu huna tabia za kujiinua. Lakini baada ya siku kadaa anagundua kwamba uko vizuri,anaaza juhudi za kutaka kukukubali.

Anakukataa kwa sababu huna kitu kwa wakati huo kwa sababu labda ulikua kimasomo zaidi,au unatafuta faranga,kimwonekano hukua vizuri. Baada ya muda Fulani, kupita unapata maisha baaab kubwa,anaanza kukutafuta ili akukubali,

Anakukataa kwa sababu unaonekana upoupo tu,lakini kwa bahati anasikia habari zako, kutoka kwa watu anaowaamini, anaowakubali na anao watamini sana wakikusifu sana, kuwa wewe ni mtu wa maana kabisa, mtu Bora kabisa.

Kisha akaanza harakati za kutaka kukukubali. Ulishawahi kukutana na Hali hizo?

Ulipokutana na mtu au watu wa hivyo ulichukua uamuzi gani?
 
Kama bado unamuhitaji mambo yaendelee, kama haumtaki basi....

Kumpenda mtu asie na kitu yani hohe hahe yataka moyo nyie!!! Hata ukifanya nae haupati utamu kabisa
Mbona mwanaume anaweza kumpenda mwanamke ambae hana kitu. Inakuaje mwanamke ashindwe kumpenda mwanaume ambae hana kitu. Tunazungumzia nini hapa, mapenzi au biashara ya uchi?
 
Kuna boya mmoja nilimpendaga aise hata hamsini mbovu alikuwa hanipi(hana hela)lakini ulikuwa huniambii kitu loh....nilishindwa maana tulikuwa tukikaa hazijapita dakika mbili tushakwaruzana kha!!muda wote kajawa na amri tu 😔😔siku nyingine natamani kudeka deka..basi hata nikitengeneza mazingira ya kubadilisha sauti iwe kama ya Celine Dion ohooooo...nakutana na sura ya vita...woooooiiii..

Na ubandidu wake hivyo hivyo loh.Shikamoo mapenzi marahaba sit down.kha
 
Onaa sasa mapenzi hakuna pesa hakuna biashara gani hii
 
Mbona mwanaume anaweza kumpenda mwanamke ambae hana kitu. Inakuaje mwanamke ashindwe kumpenda mwanaume ambae hana kitu. Tunazungumzia nini hapa, mapenzi au biashara ya uchi?
Ukiona uko na mwanamke na huna hela...arifu,jua mwanamke ndie kakuelewa Vinginevyo,maneno ya shombo hayatakaa mbali saaana na ngoma za masikio yako.sijui unanielewa...
 
Vyote mapenzi na biashara ya uchi dear....
Dah mapenzi yatoe hapo.. ibaki biashara ya uchi tu. Lakin siku Mungu akikupa pesa mingi, hautotamani tena kuwa na Bwana mwenye pesa mingi zaidi yako. Utatamani upate tu mtu anaekupenda kwa dhati. Hivyo tunaweza kubaliana ni umasikini wetu unasababisha utamani kuwa na mtu mwenye unafuu zaidi yako wa kimaisha
 
Dah mapenzi yatoe hapo.. ibaki biashara ya uchi tu. Lakin siku akikupa pesa mingi, hautotamani tena kuwa Bwana mwenye pesa mingi zaidi yako. Utatamani upate mtu anaekupenda kwa dhati. Hivyo tunaweza kubaliana ni umasikini wetu unasababisha utamani kuwa na mtu mwenye unafuu zaidi yako wa kimaisha
Tatizo watu mkiambiwa pesa basi mnadhani yani mtu awe na maburungutuuu!!!!!
Ndugu mapenzi na pesa are inseparable!!! Ukitaka kwenda kula tunda you need money, mkale, mnywe kidogo, ulipe lodge..... Pesa inahitajika
 
Ukiona uko na mwanamke na huna hela...arifu,jua mwanamke ndie kakuelewa Vinginevyo,maneno ya shombo hayatakaa mbali saaana na ngoma za masikio yako.sijui unanielewa...
Wapo wanawake wanaowaelewa jamaa zao ambao wana maisha ya kawaida tu. Kuna sista mmoja ni Kigogo kwenye kampuni moja kubwa ya kuchimba dhahabu kanda ya ziwa. Ana mume wake choka ya kawaida tu, kamzidi kiuchumi zaidi ya mara 20. Lakin hiyo heshima na love anampa jamaa yake usipime. Hawezi kufanya kitu bila ruhusa ya jamaa. Ingekuwa dada zetu hawa sasa
 
Ukiona uko na mwanamke na huna hela...arifu,jua mwanamke ndie kakuelewa Vinginevyo,maneno ya shombo hayatakaa mbali saaana na ngoma za masikio yako.sijui unanielewa...
Its either utafute pesa au usubiri kupendwa :D
 
Tatizo watu mkiambiwa pesa basi mnadhani yani mtu awe na maburungutuuu!!!!!
Ndugu mapenzi na pesa ni are inseparable!!! Ukitaka kwenda kula tunda you need money, mkale, mnywe kidogo, ulipe lodge..... Pesa inahitajika
Sasa hiyo sio pesa..hiyo ni hela. Maana kuna hela, pesa na fedha. Wenye fedha ndo kama kina Mo
 
Yote haya sababu kubwa ni umasikini wetu hakuna lingine. Imagine wote mnatoka middle class families, wote mna walau kipato kinaeleweka, kila mtu anaweza kubeba majukumu yake walau kwa kiasi kikubwa, hatuwezi kuja na hizi drama.

Mtu unatoka familia Mungu ndio anajua, wewe mwenyewe Mungu ndio anajua, it's obvious utahitaji mtu atakayekujali kifedha kwanza kabla ya kihisia.

Tupambane na huu umasikini ndugu zangu, ili tufikie mahali mtu uingie katika mahusiano sio kwa vile yule dada ana pesa au kwa vile yule kaka yuko vizuri. Such relationships are like slavery!!!
 
Kuna boya mmoja nilimpendaga aise hata hamsini mbovu alikuwa hanipi(hana hela)lakini ulikuwa huniambii kitu loh....nilishindwa maana tulikuwa tukikaa hazijapita dakika mbili tushakwaruzana kha!!muda wote kajawa na amri tu 😔😔siku nyingine natamani kudeka deka..basi hata nikitengeneza mazingira ya kubadilisha sauti iwe kama ya Celine Dion ohooooo...nakutana na sura ya vita...woooooiiii..

Na ubandidu wake hivyo hivyo loh.Shikamoo mapenzi marahaba sit down.kha
Ni miti aliyokuwa anakupiga ilikufikisha.. Inaonekana alikuwa anakujulia kukukuna na kukukojelesha kiasi kwamba hata ukifikiria kuondoka uziache hizo raha unashindwa. Nguvu kubwa ya wanaume tuliyo nayo ni mikandamizo na mikito ya kitandani. .Basi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom