Ulaya yatapatapa kuzuia ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda hadi Tanzania

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,870
7,752
Kama wewe ni wale waafrika wanahamaki wanamapinduzi tukiwaita wamagharibi mabeberu kutokana na ulevi wa fikra waliyofanikikiwa kukupandikiza, na kama uko Afrika ya mashariki yafaa uzinduke sasa.

Kutokana na mipango ya nchi za maghararibi nchi za Uganda na Tanzania haziruhusiwi kuendeleza miradi ya gesi na mafuta kwa sasa hata kama wao watataka kufanya hivyo ila tu pale wao wakiona itaendana na mipango yao ya kinyonyaji.

Nchi za ulaya ya magharibi baada ya kuona vibaraka wao wameshindwa kuzuia mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania sasa wanatapatapa. Kupitia bunge la ulaya eti wamepitisha azimio kukataza uendelezaji wa mradi wa bomba hilo eti litaharibu mazingira na kuwaondoa watu wengi kwenye ardhi zao.

Tangu lini hawa wakoloni wa Afrika wameanza kua na huruma na waafrika? Siku hizi eti wanatufundisha haki za binadamu ambapo kipau mbele eti turuhusu ushoga ndoa za jinsia moja na utoaji mimba. kusema kweli hawa wazungu wanatudharau na kutukosea heshima kwa kiwango kikubwa.

Bunge la Uganda tayari wamepitisha azimio kulaani azimio hilo la bunge la ulaya. Inafaa bunge la Tanzania pia tulaani azimio hilo la kibeberu lisilo na haki wala ukweli wowote.

Nchi zetu za Uganda na Tanzania tusishtuke wala kukwazika na ubeberu wa magharibi. Tuendelee na mpango wetu na sio kukubali kupelekeshwa na wamagharibi ambao mipango yao ni kuzinyonya nchi zetu na kuhakikisha hazipati maendeleo ya kweli yenye kuwapa wananchi wetu maisha bora.

Baada ya kuondokewa na Magufuli Watanzania tunakutegemea mzee Museveni kuongoza mapambano dhidi ya mabeberu hawa kuhusu huu mradi wa bomba la mafuta.
 
Watu wanaojiita watu wa mazingira wengi wao wanatumika tu kwenye ushindani wa kibiashara au kiuchumi kukwamisha agenda za washindani wa wafadhili wao.
 
Mbaya zaidi kampuni inayomiliki hiyo project TOTAL ni ya huko huko Ulaya.

Mabenki yanayoleta hela ni ya huko huko Ulaya labda Mchina aichukue na kuiendesha hiyo project na wababe wengine kama Russia.

Africa iko utumwani inahitaji ukombozi mwingine na sio ule uhuru wa bendera.
 
Mmezuiwa alaf unasema wanatapa tapa, kuna kiongozi wa kuwakazia wazungu hapo, we kiazi kwel
Bila shaka utakua mchg wa chadema. Nyie ndio mnafikiri lazima kukubaliana na wazungu. Inatokana na utamaduni wenu wa ubinafsi.
 
Wazungu wanajua WaAfrica ni wapumbavu na ili kuendelea kuwatawala lazima waendelee kuwa wapumbavu kwa kutumia kila tool inayoweza kuwafanya wawe wapumbavu.

Ndani ya WaAfrica wapo watu ambao nao wamejiona kama wazungu tayari na Europe and European ndio ndugu zao ilihali ni weusi wa Africa wanaohitaji kusacrifice maisha yao kwa ajili ya Africa na WaAfrica wenzao.
 
Kama wewe ni wale waafrika wanahamaki wanamapinduzi tukiwaita wamagharibi mabeberu kutokana na ulevi wa fikra waliyofanikikiwa kukupandikiza, na kama uko Afrika ya mashariki yafaa uzinduke sasa...
Wakati wa hayati magufuli hawakuona huo uharibifubwa mazingira,kwa nini iwe sasa hiv?
 
Waafrica bado tu watumwa sana, yaani wazungu wanataka kila tufanyalo na wao wahusishwe na maslahi yao yawepo.

Hata magu angekuwepo akafosi mwisho wa siku tungewekewa vikwazo kama zimbabwe maana vikwazo ndio silaha yao kubwa kuliko zote

Kwa hali hii kujikomboa kwenye huu utumwa ni vigumu sana.

Bora wasaudhi waliamua kusimama na Mrusi mapema ndio maana wana maendeleo zaidi Africa, hakuna mzungu anaependa maendeleo ya mwenzake.

Mfano hii vita ya ukraini us anatia nguvu sana iendelee kuwepo ili maana anajua mataifa ya ulaya ndio yanayoumia zaidi na yatadhoofika ili us azidi kuwakalia, unaeza kuta hata urusi na us lao moja ili wabaki wao wenyewe kuwatawala wengi wao kifikra na kiuwezo.
 
Mtanikumbuka!! in jpm's voice
Heri kumkumbuka malikia kuliko huyo Jamaa.

Tanzania na Uganda zikae chini zione zinawezaje kuuanza mradi huu kwa kuutengea badger ndogo AWAMU Kwa awamu, mabeberu watakavyoona unazidi kusonga mbere watajitokeza tu na kubaini ujinga wao.
 
Heri kumkumbuka malikia kuliko huyo Jamaa,

Tanzania na Uganda zikae chini zione zinawezaje kuuanza mradi huu Kwa kuutengea badger ndogo AWAMU Kwa awamu, mabeberu watakavyoona unazidi kusonga mbere watajitokeza tu na kubaini ujinga wao.
Malkia ya nyoko!! potea kaa mbali kabisa
 
Heri kumkumbuka malikia kuliko huyo Jamaa.

Tanzania na Uganda zikae chini zione zinawezaje kuuanza mradi huu kwa kuutengea badger ndogo AWAMU Kwa awamu, mabeberu watakavyoona unazidi kusonga mbere watajitokeza tu na kubaini ujinga wao.
Hata wewe unamkumbuka jpm. Mbona angekua hai angefanya kama ulivyofikiria wewe. Kuanza kwa fedha zetu.
 
Mkuu zoezi limeanza lini? Mbona makampuni yaliopewa izo tenda za huo mradi ziko kimya..yani no process. Au kazi imeanza uko Uganda?

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Imekukata mkuu 😆😆😆😆.

Tulia Mzee kinachoendelea kwa sasa ni maandalizi ya ujenzi hasa kwenye Kambi mbalimbali ambako kutakuwa na viwanda vya kufanya coating za mabomba nk..

Tafuta wahusika utajua stutus ya utekelezaji..Mbona taarifa zipo you tube utazuona.
 
Mbaya zaidi kampuni inayomiliki hiyo project TOTAL ni ya huko huko Ulaya.

Mabenki yanayoleta hela ni ya huko huko Ulaya labda Mchina aichukue na kuiendesha hiyo project na wababe wengine kama Russia.

Africa iko utumwani inahitaji ukombozi mwingine na sio ule uhuru wa bendera.
Mchina na Mrusi wote ni wanyoyaji tuu
Ukombozi wa mwafrika dhidi ya ubeberu upo mikononi mwetu sisi wenyew hakuna mtu wa kutukomboa bure bure tuu mkuu .
 
Back
Top Bottom