Ulawiti adhabu yake ni miaka 30 jela bado Spika anasema anataka hiyo irekebishwe

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,692
3,857
Eti irekebishwe iwe kali zaidi. Hayo sasa ni masihara.

Ile sheria ni kali sana kwa vitendo vya ulawiti. Ile sheria inapinga hata mwanamke kulawitiwa. That is how mean that law is. Sasa unataka kuifanyia marekebisho gani? Kwa sababu ukianza kusema unataka sheria iwe taiti zaidi ndio utawaibua Wamarekani. They will accuse you of cruelty.

Juzi nilikuwa natazama video clip ya msanii Dudu Baya anaongea katika interview. Anasema aliwahi kumsikia yule mwanaharakati nani sijui, Simba nani sijui (nadhani alikuwa ana maana Helen Kijo Bisimba).

Anasema alimsikia yule akisema walipokuwa Marekani walipewa fedha nyingi wawaletee Wabunge, za kuwahonga Wabunge wapitishe sheria ya kusapoti ushoga. Anasema walizikataa zile hela.

Fikiria complication zinazoweza kutokea tutakapojaribu kujadili haya mambo wakitokea hao watu wanaotaka kuwahonga wabunge hela.
 
Shida ya Tanzania siyo sheria, bali usimamiaji wa sheria.

Tuna sheria kali za ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, lakini viongozi na watendaji ndani ya Serikali wanaendelea kupora kila mwaka.

Tuna sheria kali dhidi ya watoaji na wala rushwa, lakini hao wabunge wakati wa uchaguzi wanahonga kwa kufuru, wakishakuwa wabunge wanakula rushwa na kufanya ulaji rushwa kama ni matendo ya kawaida.

Hawa akina Tulia, hakuna cha sheria kali wala nini. Wameileta hoja ya ushoga kwa dhamira chafu. Wanataka wananchi waondoke kwenye mjadala mzito unaohusu wizi wao ulioainishwa na CAG.
 
Unaandika utadhani unatumia kidole Cha mguu kutype huku ukihariri kwa jicho la tatu..
 
Usimamizi pamoja utekelezaji wa hiyo sheria ni sifuri kabisa. Walawatiwa wanajionesha wazi wazi si wa kike wala kiume ila hakuna hatua zichukuliwazo
 
Ushoga kweli upo na unahitaji kudhibitiwa lakini mjadala wa sasa umezua taharuki kubwa. Umekuwa kama tangazo la promosheni.

Kabla ya kupiga kelele mtu achunguze kwanza nyumba yake, ukoo wake na hata kimtaa chake kama kuna watu wa aina hii. Ikigundulika kwa pamoja tunajadili katika familia ukoo au grupu jinsi ya kulikabili. Tunakemea kwa nguvu zote ndani familia na makundi.

Mgazi ya taifa kuna sheria ambazo hazitekelezwi au ngumu kutekekezwa. Mbona tunakataa uchawi na wizi tukatae pia ushoga
 
Mbona hatoi adhabu kwa wabunge mashoga ambao Masaburi kakiri kuwa wapo??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom