Mnada wa kwanza wa korosho uliofanyika 11/10/2024 ulifunguliwa kwa bei ya TSh 4150/= kwa kilo moja ya korosho. Kwenye mnada huu kulikuwa na tani chache sana za korosho. Ukafuata mnada wa pili ambapo bei ilishuka mpk kufikia TSh 3750/=, napo pia kulikuwa na tani chache sana za korosho. Bei imeendelea kushuka na sasa imefikia TSh 3400/= ndani ya mwezi October. Na kumekuwa na janja ya kihuni ya kukwepa kubeba korosho za wakulima kupeleka kwenye ghala kuu ili kusubiri bei ishuke halafu korosho za wakulima zinunuliwe kwa bei ndogo baadaye.
Mavuno makubwa ya korosho yatafanyika mwezi huu wa November, ambapo ndipo wakulima wengi watauza korosho zao.
Kwa inavyoelekea bei ya korosho itakuwa TSh 2000/= (bei isiyofaa na inayomuumiza mkulima).
Kwahiyo bei ya TSh 4150/= ilikuwa ni danganya toto iliyovalishwa boksa ya kiki za kisiasa iliyolenga kuisaidia ccm kupiga kampeni kwenye chaguzi za serikali za mitaa.