Ukweli wa maisha tunayoyapitia vijana (true story ya maisha yangu)

apprentice1997

Senior Member
Jun 8, 2016
107
99
Habari za jioni,
Nimekuwa inspired na post ya mshana jr kuhusu vijana ndio maana na mimi nataka kushare na nyinyi story ya maisha yangu.

Najua kuna wengi watatukana ila naomba mnisamehe pale nitakapowakwaza lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. Mimi ni kijana wa kiume umri wangu ni miaka 18. Nimepitia mambo mengi sana ila sitasahau kamwe mambo niliyoyapitia baada ya kuingia sekondari.

Nimeanza mahusiano ya kimapenzi toka nikiwa form one, ila ule ilikuwa ni utoto tu hivyo sikuwa serious sana. Nimeanza kuwa serious form 2 baada ya kuanza mahusiano na msichana ambaye nilijikuta nampenda sana nikaweka mipango kuwa kama penzi letu litadumu ni lazima nimuoe. Bahati mbaya yule msichana hakuwa mkweli kwangu toka muda huo wote alikuwa anatembea na wanaume wengi sana niseme ukweli kuwa tuliahidiana tusifanye mapenzi hadi tutapooana na mimi nilikuwa tayari kuitunza ahadi yangu ila bado yeye aliendelea kuchepuka.

Nikiwa form 3 nikajua uongo wake wote ila nikaogopa kumuacha kwa kuwa alikuwa mzuri na wala sikujali tofauti za kiuchumi za familia zetu nilijitoa kwa kila kitu. Tarehe 12/06/2014 nikiwa form 3 tulifanya mapenzi kwa mara ya kwanza na mimi ikiwa ndo mara yangu ya kwanza.

Kiukweli sikuenjoy kama watu wengi wanavyofikiria na zaidi nilibaki na majuto kwa sababu baada ya kumaliza tu kufanya mapenzi neno la kwanza aliniambia ana mimba yangu. Niligoma kabisa kwa sababu mimba haiwezi kujulikana saa hiyo hiyo baada ya kufanya mapenzi.

Kila tukigombana alikuwa ananitishia ana mimba yangu na mimi nikisikia hivyo nakuwa mpole. Baadae nilikuja kuona ni ujinga nikaamua kumpima na nikagundua hakuwa na mimba. Kiukweli alinichafua sana Kwa watu wengi na zaidi viongozi wa dini waliokuwa wananiamini hawakuniamini tena yote sababu ya mambo aliyonifanya niyafanye ni mengi sana yamenikuta na hadi kutishiwa maisha yangu na wanaume wengine.

Mwaka huohuo mwezi wa saba baada ya kurudi shule niliwaza sana nikafikiria nguvu iliyo ndani yangu na uwezo wangu wa kimasomo ambapo toka nimeanza chekechea hadi leo nimeshika nafasi ya kwanza tu. Nilikuwa nasoma shule ya bweni na sikuwa na simu.

Siku moja baada ya kwenda mjini nilienda internet cafe nikamwandikia msg kupitia Facebook ya kumwambia tuachane, iliniuma sana kwa kuwa sikuwa na jinsi huyu msichana alinifanya hadi nishindwe kusoma Kwa sababu yeye alipenda sana starehe. Alinitishia kwamba atajiua na aliwatuma rafiki zangu waje kunambia kuwa ana mimba yangu tena na kwamba vipimo tulivyofanya mwezi mmoja uliopita vilidanganya niligoma kabisa kurudiana nae na nikaanza maisha mapya ya shule nikiwa single.

Baadae nilikuja kupata taarifa kuwa msichana yule alitoa mimba mwezi mmoja baada ya kuachana na mimi na aliumwa sana. Mimba ile ilikuwa ni mimba ya tatu toka aanze kutoa mimba. Mpaka sasa nasikia alikuwa mjamzito na mimba ilishafika miezi 9 possibly atakuwa na mtoto sasa hivi.

Baada ya kuanza maisha yangu upya nilikuwa na rafiki wa kike ambaye tulikutana easter conference 2014 na toka siku ya kwanza tulipojuana tulianza kupendana hatukuweza kuwa wapenzi sababu tayari nilikuwa na mtu na yeye hakuwa naye alikuwa akinisubiri mimi tu.

Nilikuja kumwambia kila kitu kuhusiana na mahusiano yangu yaliyopita na na akanielewa na akaanza kuwa karibu na mimi, akaniambia nimuahidi kuwa sitarudia tena makosa niliyoyafanya zamani nikamuahidi huku nikijutia makosa yangu, baadae urafiki ukakolea tukaja kujishtukia tumeshakuwa wapenzi bila hata ya kutongozana, nikaapa kuwa nitakuwa mkweli na nitatunza ahadi yangu kwake. huyu msichana ana hofu kubwa sana na mungu yeye alikuwa form 4 mimi nikiwa form 3 akawa ananikazia nikazane na masomo, nikakazana sana na nikawa muwazi kwa kila kitu ninachokutana nacho.

Mwaka huo form 3 nikaanza kutengeneza program za computer na nikafanikiwa kupresent katika makongamano ya kimataifa. nikaingia form four tukaendelea kuonana na mapenzi yetu yakizidi kukua kila siku. nikakazana na ubunifu wangu na yeye akinisapoti japokuwa hajawahi kuona hata project moja mwaka huo nikazindua website yangu ya kwanza.

Nikamaliza shule nikarudi mtaani, mwaka huu nimeitwa kwenye interview ya scholarship ya african leadership academy sikufanikiwa kupita ila ninashukuru mungu kwa achievement kubwa niliyofikia maishani. Wazazi wakanambia nisikate tamaa, nikatengeneza program ya pili ikiwa ni nzuri kuliko zote zilizopita nayo ikafanikiwa. Nikaandika kitabu ambacho bado sijakimaliza ila kiko katika hatua za mwisho kabla sijaanza kukichapa. Mwezi mmoja baadae nikateuliwa kushiriki tuzo za vijana nimefanikiwa na sasa tupo kwenye hatua za kupiga kura nikiwa nimebaki na wiki moja tu kabla ya kwenda kuchukua tuzo hiyo, ninaona mafanikio katika siku zangu za mbeleni.

Mwanzo nilihofu kuwa tayari nimeshafanya ngono sitaacha na nitabaki kuwa player maisha yangu yote. Yeye akanishawishi nikaelewa na mpaka sasa sijafanya ngono tena. Mimi na yeye tunapendana sana mara kadhaa tunaonana na kuishia kushikana bila kufanya mapenzi na pia tumeahidiana tusifanye mpaka siku tutakapooana.

Ninakutana na vishawishi vingi sana na mara nyingi sana nimetamani kufanya ngono na nikanunua condom nikaishia kuzitupa bila kuzitumia. Imefika hatua sitaki kuanzisha mahusiano na mtu na hata nikianzisha mwisho dhamiri inanisuta na kuamua kuachana nayo nimeamua kubaki kuwa mwaminifu kwa huyu niliyenaye nikiamini katika ndoto zangu na mimi pia nikiamua kujitunza nikijua kuwa muda si mrefu nitakuwa rolemodel katika jamii kwa vijana wengine na mpaka sasa ninaongea na wanafunzi katika shule za sekondari zaidi ya 1500.

Nikitazama nyuma ni Mungu tu namshukuru kwa kunipa zawadi ya uhai na kunipa watu wanaonifanya niwe mtu mzuri kilasiku. Ninamshukuru Mungu kwa kuwa haya yote ninayoyapitia anayaficha na hakuna mtu anayejua zaidi yangu mimi tu. nikiangalia mbele ninaona future yangu ikiwa nzuri zaidi na mafanikio nimeshaanza kuyaona yote ni sababu ya mungu. Ninamuomba mungu atulinde tuweze kudumu na pia anipe nguvu ya kushinda vishawishi na jaribu gumu zaidi ni nkuwashinda wasichana wanaoniwinda kilasiku ninajua kuwa maisha yangu na furaha yangu ni kubaki kuwa mkweli kwa mpenzi wangu huyu na kujitunza nisifanye ngono tena hadi nitakaporuhusiwa.

Haya ni mambo machache kati ya mengi niliyopitia na ninayopitia maishani mwangu. nina furaha kuwa msichana huyu amenipa nguvu ya kuendelea kufanya vitu vizuri kilasiku. namshukuru mungu kwa zawadi ya uhai.

ASANTE SANA
 
daaaa,good&smart boy.Usichoke kumshirikisha Mungu kwa kila jambo,hakika amin katika yeye tunashinda.
 
Kwanzaa nikupongeze kwa hatua uliyofikia, hakika ni Mungu tu ndo wakumtegemea usichoke kupiga goti kila iitwapo leo, sali na umwombee pia na huyo mpenzi wako.
 
Kama uliweza kuandika kitabu iweje ushindwe kuandika story yako kwa ufasaha yote bila kurusha rusha matukio??

Ungeandika vizuri tungekuelekeza nini usifanye ili uweze kufika mbali zaidi.Mungu akutie nguvu. Ukiandika tena ukumbuke kuruka mstarii
 
kwaio toka uzaliwe umepiga goli moko tu,hilo hilo ndilo litakalokupeleka motoni coz kuzini nje ya ndoa ni dhambi,kibaya zaidi hakuna dhambi kubwa wala ndogo zote sawa tu,kwa maana hiyo wewe uliyegonga mara moja na wale malaya wanaojiuza mpo sawa tu,hongera anyway!
 
Kazana kusoma ufaulu form4 ,,,umejiingiza kwenye mapenz mapema sana mnafika secondary wadogo kiumr ila mnavamia mapenz kwann shule zimebadilika sana siku hiz,,,enz zetu umri wako tunashindana kufanya pepa tu Kwa Muddy mchikichin,Mtiga mapambano,Sir Walter, soma bhana achana kufatilia snario za huku Jf zitakupotezea muda njoo huku ukimaliza form6 uko chuo nakushaur Uninstall Jf,inst,na zngne ili uongeze kapacit ya material ya shule bado uko under 20,,,dogo mi nina 27 ndio nimemaliza chuo nikiwa chuo ndio nimejiunga na hiz socially network wakat nakula boom sasa ww hata form4 bd? Usije ukafanya ya Jesca tu...una vitu flan unavyo ukipunguza mambo meng u will be the best ever.
 
aaaaah kwa wazoefu huyo ulienae umeshagongewa au utagongewa mapema iwezekanavyo...! usishangae mara ya kwanza utakuta breki p*mb*.hebu mchunguze vizuri.Tumepitia huko kijana
 
Hongera dogo, ila siku nyingine jifunze kutengeneza paragraph unavyoandika, au hamuandiki essay huko shule!?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…