Ismail Tano
Member
- Jul 23, 2022
- 7
- 1
Ilikuwa ni kama ndoto ambayo uwezekano wake ulikuwa ni mdogo sana kuwezekana kwenye ligi kuu Tanzania bara kwa wachezaji kuuzwa kwa gharama kubwa, wachezaji kusaini mikataba yenye thamani kubwa mpaka kufikia zaidi ya milioni 100 kwa mchezaji mmoja wa ndani mwenye asili ya kitanzania, wachezaji kupewa ile hadhi inayotakiwa kupewa kutoka kwenye vilabu vyetu kama vile matibabu, malazi, vyakula na malazi mazuri bila kusahau usafiri mzuri.
Imefikia kipindi ambacho ligi kuu Tanzania bara inatoa wachezaji kuwania na kushinda tuzo kubwa katika mashindano makubwa mfano Pape Ousmane Sakho ambaye ndani ya mwezi huu ameibuka mshindi wa goli bora la mashindano kwenye ligi ya mabingwa barani afrika huku akitokea Simba Sports Club kutokea ligi kuu Tanzania bara bila kusahau mchezaji kama Feisal Salum "Feitoto" kutokea Young Africans kutakiwa na vilabu vikubwa vya ndanj na nje ya nchi bila kusahau wachezaji kama Luis Miquisone kuuzwa kwa mabilioni ya pesa za kitanzania kutokea Simba Sports Club kwenda Al ahly.
Leo hii Tanzania tuna ligi ambayo malalamiko dhidi ya marefalii yamepungua kwa kiasi kikubwa mno tofauti na ilivyokuwa zamani, leo hii tuna ligi ambayo inatazamwa katika ubora mzuri wa high definition (HD) katika michezo yote hongera nyingi kwa Azam Tv, ligi ambayo inavutia kwa wadhamini mpaka kufikia hatua kuweka fedha nzuri mezani mpaka kufikia milioni 500 kwa mshindi wa kwanza, ligi ambayo inaruhusu hata ukiwa kwenye nchi za jirani kutembea kifua mbele bila wasiwasi kutokana na ubora wake.
Changamoto zipo na nadhani zitaendelea kuwepo kutokana na uhalisia wa binadamu kuwa hakuna kazi ya binadamu yoyote yule duniani ambayo haina makosa, hivyo basi achilia mbali ubora ulioongezeka katika ligi kuu Tanzania bara pia changamoto zipo.
Changamoto ambazo naamini zipo kwa lengo la kuboresha na kutuonyesha wapi tuongeze juhudi na wapi tupo sawa ili kufikia malengo yetu ya kufurahia mchezi huu wetu pendwa wa mpila wa miguu.
Pongezi ziende kwa wanaosimamia na kupanga sheria za mpila wa miguu nchini (TFF) kwa juhudi na jitihada zao katika kusimamia na kuendesha shughuli zote, pongezi vile vile ziende kwa wapenzi na wafuasi wa mpila wa miguu kama vile mashabiki na vyombo tofauti tofauti vya habari nchini kwa kuweza kusimama vyema kwenye kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na pongezi za dhati pia ziende kwa wachezaji wote wanaojitoa na kujituma wawapo uwanjani katika kuhakikisha wapenzi na mashabiki wa mpila wa miguu tunafurahia.
Kwakumalizia, wanasaikolojia na watu waliobobea katika masuala ya akili na mawazo ya binaadamu wanasema kuwa uhalisia wa maisha ya binaadamu ni jumla ya mawazo au picha anazojijengea akilini mwake hivyo katika kuangalia mabaya yanayoonekana ndani ya ligi kuu yetu kama tutaendelea kuyaangalia kila siku ni wazi hatutoweza kuona uzuri wake, vile vile katika kuangalia uzuri pekee hatutoona maovu hivyo tujijengee utaratibu wa kuangalia pande zote ili tuweze kupata picha kamili ya uhalisia wa mpira wetu ndani ya nchi.