Ukweli ni upi kuhusu Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
6,835
9,665
Ni mjadala wa miaka mingi, lakini bado muafaka haukafikiwa.

Kuna wanaotaka Kiswahili kitumike kufundishia kuanzia Chekea Hadi Chuo Kikuu, na kuna wanaotoka English iwe lugha rasmi ya kufundishia madarasa yote.

Mimi nakubaliana na wanaotaka Kiingereza ndiyo kitumike?

Kwa wale wanaotaka Kiswahili kitumike wana nia gani hasa? Wanasukumwa na uzalendo au hawakijui Kingereza fasaha?
 
Wewe unaetaka kingereza kitumike una nia gani hasa ?
 
sub-atomic particles zinaitwaje kwa kiswahili,
Chembe ziada za atomiki , tafuta vitabu ya biology, Chemistry, na geography vya kiswahili uone Kama Kuna neno limeachwa aununua Lambert iliyoandikwa kwa kiswahili ukishindwa tafuta kamusi ya sayansi na teknolojia. Ukweli kuhusu lugha nikuwa lugha yeyote hujitosheleza kwa watu wake na misamiati unaweza kuongezwa wakati wowote hushangau Kwanini Misamiati mingi ya geography katika kingereza Ni ya lugha za kilatini au Hesabu lugha za kiarabu?
 
Wewe unaetaka kingereza kitumike una nia gani hasa ?
Kiswahili ni lugha ya Kimataifa. Watanzania wengi wakikijua itakuwa ni rahisi kujichanganya kwa uhuru na watu wa mataifa mengine. Lugha isingekuwa kikwazo.
 
English is International language,
Daktari usome udaktar kwa kiswahili, uambiwe labia majora ina shavu nene 🤣 kisha uende interview ya UN wakuulize labia majora ni nini ushindwe 🤣🤣🤣🤣

Tusome tu English tuwe international people, no proud in being local ppl
 
Ndivyo. Tanzania ingekuwa na nguvu kiuchumi hata nchi nyingine zingetumia kiswahili kufundishia . Lakini kwa bahati mbaya nchi yetu bado Ni tegemezi hivyo hata lugha na utamaduni inabidi tutegemee wa nje
China Ina nguvu kiuchumi.
Tutajie Taifa jingine linalotambulika na Umoja wa Mataifa lonalotumia kichina kama lugha ya kufundishia?

Cha muhimu ni Nia, maono ya nchi, kwa wataalamu na wanasiasa.
 
English is International language,
Daktari usome udaktar kwa kiswahili, uambiwe labia majora ina shavu nene 🤣 kisha uende interview ya UN wakuulize labia majora ni nini ushindwe 🤣🤣🤣🤣

Tusome tu English tuwe international people, no proud in being local ppl
Lengo la kutoa elimu ni watu wako kusaidia taifa lako au kwenda kuajiriwa U.N ?
 
Back
Top Bottom