Ukweli narudia tena kutamka kuwa Tanzania hatuna Bunge kabisa kama mhimili

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
TANZANIA HAINA BUNGE....

Narudia tena kutamka kuwa Tanzania hatuna Bunge kabisa kama mhimili au 'watch dog' wa serikali, tulichonacho ni jamaa fulani hivi wanaitwa wabunge ambao hukutana pale Dodoma na kutafuna posho na kulipwa mishahara ambayo ni kodi zetu.....

Watu hao wamekuwep tangu mwaka 1995 tulipoanza kuibiwa rasilimali zetu kwa baraka zao.......!!!

Hao wanaojiita wabunge akiwemo pia mtu aliyekuwa anajiita mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato) John Pombe Magufuli......kazi yao kubwa ilikuwa ni kubariki wizi huo. Wale wa kile chama kilichotawala miaka yote, kazi huwa ni kushangilia kila kitu kinachopelekwa na serikali yao

Kama Bunge lingekuwepo Tanzania, wizi huo usingedumu kwa miaka yote hiyo.......

Kwa Tanzania 'Bunge ni chanzo cha ajira hewa'

[HASHTAG]#HakunaJipya[/HASHTAG]
 

Mkuu Francis12 umeandika kiuchochezi sana huu uzi wako.
Yawezekana u miongoni mwa waliokuwa wakijitahidi kupiga simu
ili wapewe 'classified details" za kamati.

Haiwezekani mwenyekiti wako ajiite mkuu wa kambi ya upinzani bungeni wakati
bunge husika halipo "its a null / void parliament" , and worse enough its non -existing pillar of government

siku nyingine usitufanye sisi wote kuwa ni nyumbu, maana nyinyi ndio wale mnaotumwa kijii cha jirani kufata chakula kwa niaba ya wanakijiji wenzenu walio kwenye baa la njaa ,mnapopewachakula hicho ili mle wote, ila matokeo yake chakula hicho mnaanza kukila huku mnakisimanga kuwa chakula gani hiki, hakifai kabisa hata kuliwa na binadamu".
 
Bunge km Jengo tunalo zuri TU kuliko ata LA Uingereza.....Tatizo ni aina ya Binadamu wanaoingia Bungeni ndo majanga....Mfano Binadamu km was Mtera,Msukuma,Kessy na alike unategemea nn? Spika na N/spika wote hawajui km Bunge ni Muhimili sawa na Serikal au Mahakama lakini wote wapo mfukoni mwa Rais utadhan Viongozi was Bunge wanateuliwa na Rais.....hili ndo Tatizo kubwa hatuna viongozi was Bunge wanaojisimamia kua wao ni viongoz wa Muhimili muhimu unaopaswa kuisimamia Serikali..... Hili Nalo ni upepo TU ktk Sauti ya JK
 
SERIKALI KUU ni mhimili ambao unaongoza mihimili mingine kwa hapa Tanzania.Mihimili hii mingine ni kama mapambo tu
 
Mwambieni atutajie majina na namba za simu za wale wote ambao amedai wamekuwa wanawasiliana na Acacia na lini walifanya mawasiliano hayo na yalihusu kitu gani. Kutoa hukumu kwa innuendo peke yake haitoshi, tunahitaji ushahidi thabiti kutoka kwa Rais Magufuli..
Kachukue mshahara wako wa buku 7 huko ulipoajiriwa.
 
Well said bro. Adui wa kwanza wa taifa hili ni fisiem.Wanajitekenya na kucheka wenyewe.
 
Tatizo la lile bunge ni CCM!! . Inajaribu kutawala akili za kila anayeingia humo.

Bahati mbaya kabisa WaTz ni waoga na wanafki hatuwezi kuwawajibisha
 
Hili Bunge kuwa haramu wa kulaumiwa ni wale wale MACCM kwa kuamua kulifanya ni kitengo chao na kuliendesha kidikteta vile atakavyo huyo anayedai anainyoosha nchi kumbe anaivuruga na kuiangamiza Tanzania yetu.
 
Alafu wamekosa hata busara ya kuomba radhi badala yake wamebaki kuwashambulia waliokuwa mstari wa mbele kupinga huu wizi.

Leo hili lilikuwa topic ya maongezi yetu wakati wa chakula cha mchana. Kwa nini hakusema wale wote walioshirikiana na "wezi" watubu kwa watanzania? Kwa nini waliowapa "wezi" wakajichumia wanavyotaka wanasubirishwa?

Wengi wanafikiri hili suala la madini na mikataba mibovu ni kitu kipya. Hawajui kuna waliopinga mikataba ya kidhalimu wakaishia kupoteza ajira zao. Wengi wakadharauliwa na bado wanaendelea kudharauliwa wakati walichokuwa wanakisema ndiyo mapendekezo ya kamati ambazo nina hakika hazikutumia pesa kidogo kufanya kazi waliyotumwa.
 
Wabunge wa CCM hata mwenyekiti wao wa chama akiwaambie wamzomee Spika wanaweza kufanya hivyo bila hata kuhoji sababu ya wao kutakiwa wazomee. Ni kama bendera tu inavyofuata upepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…