Kuna kesi moja kama hii ilitokea zamani Sinza, yule dada 'hear say' zinasema mkono wake ulihusika katika kifo cha mumewe. Mume alijiweka vizuri na biashara, nyumba, magari. Walikuwa na watoto wadogo na mke akawa mrithi wa mali za marehemu. Baada ya muda kama miaka miwili alipata ka-kijana, kijana akawa ndiyo mpangaji wa maisha ya dada. Alimwambia hapendi kuishi kwenye nyumba iliyojengwa na marehemu, ilibidi iuzwe wanunue nyingine, kumbe nyumba ilinunuliwa kwa jina la kijana. Ni mengi yalikotekea lakini katika kipindi cha miaka 10, mke wa marehemu alifisika kabisa.