Ukoloni unarudi Tanzania?

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,752
5,600
Na Thadei Ole Mushi.

Miaka 60 ya Uhuru tumeshindwa kabisa kusimamia rasilimali zetu wenyewe.

Migodi tumeitoa kwa Wazungu, Misitu tumeitoa kwa Mwarabu, Posta tumeitoa kwa Mwarabu, Misitu tumeitoa kwa mwarabu, Gesi tumeitoa kwa Mzungu, Uwanja wa ndege wa KIA nao tumeutoa, TPDC tumeitoa, Bandari tumeitoa kwa mwarabu, Loliondo tumeitoa kwa Mwarabu, karibi maeneo yote Muhimu tumeshatoa…. Sisi tumebakia na nini?

Maswali ni Mengi mno….

1. Tulidai Uhuru wa Nini?

2. CCM imeshindwa kuiongoza Nchi? Maana kila eneo tuliloliwekeza tunasema kuna wapigaji hivyo bora tumpe mwekezaji. Je Serikali ni dhaifu imeshindwa kuzuia upigaji?

3. Vyuo Vikuu zaidi ya 31 nchini vimeshindwa kutengeneza wasomi wa kusimamia hizi rasilimali za taifa? Kazi za Graduate wetu kubwa ni kuendesha Bodaboda, kama taifa tunajua tunakoelekea?

4. Tanzania tunaweza jambo gani kubwa hapa nchini? Mambo yote ya muhimu tunaona ni Magumu tunawapa wawekezaji je sisi ni kitu gani tunaweza? Wenzetu wanawezaje sisi tunashindwa? Huu uvivu wa kufikiri tumeutoa wapi?

5. Baada ya Bandari tunaenda kuwekeza rasilimali gani tena? Ukiona wabunge wetu wanavyovaa Suti Pale Bungeni na taifa linapoelekea utatamani kulia. Hawa watu (wabunge) tunawalipa mishahara, tunawanunulia mafuta ya magari, watoto wao tunawasomesha na bado wanatuibia kupitia mikataba hivi nani alituloga tukawa waoga hivi?

6. Tanzania ya watu Milioni 69 plus tumeshindwa kuchaguana miongoni mwetu tupate watu wanaoweza kutuvusha hapa tulipo kwa kuwa taifa linaelekea kutawaliwa kwa mara ya Pili?

7. Wakati Uganda ilipogundua kuwa ni kweli Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbiziwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu Oil Production na asilimia kubwa ya mradi wao wa mafuta ni vijana wanausimamia. Sisi badala ya kuandaa vijana tunatuma kina Steve Nyerere na kina Kitenge kwenda kukagua Bandari za wenzetu hivi nani alituloga?

8. Vijana asilimia 90 sasa hivi hapa nchini bila kujali elimu zao kazi zao kubwa za kujipatia kipato ni Kubet au kuendesha Bodaboda. Huku maeneo muhimu ya rasilimali za taifa lao zikigawanywa kwa wazungu na waarabu kwa jina la kusema ni mwekezaji. Hii ni hatari sana kwa taifa letu…. Tanzania ina wanyamapori kila mahali ila anayekula nyama pori first class kabisa hapa Tanzania ni Mwarabu hii ni aibu…

9. Je tuliwahi kupata Uhuru? Lakini mbona Kina Singapore walipata Uhuru nyuma yetu? Mbona leo ipo mbali sana na wanajisimamia wenyewe?

10. Hata kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa taifa zima tumeshindwa tunaagiza nje ya nchi, Ngano tunaagiza, Mbolea tunaagiza, Maziwa ya Unga na hata ya kawaidia tunaagiza, pale Bandarini asilimia 95 ni bidhaa zinaingia nchini badala ya kutoka hivi tunaelekea wapi?

CCM ikubali sasa kutumia watu ambao wapo nje ya familia zenye Connection kwenye Uongozi wa nchi hii. Babu alikuwa kiongozi, mtoto akatafutiwa connection akawa kiongozi, mjukuu naye akawa kiongozi nk …. Hizi DNA kwa mazingira ya Sasa zimechoka au CCM ikubali kuwaachia wengine wajaribu kutusogeza tulipo.

Kuna siku nilisema kama Africa itaheshimu Sanduku la Kura katika kuchaguana tutafika mbali sana. Na kama askari polisi wa Mataifa ya Africa watatimiza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria hili bara linapiga hatua kubwa. Askari anamlinda mtu mwenye V8, Mke ana gari, watoto wa huyo Mtu wanachukuliwa na School Bus wanakupita getini unawachekelea kama Zuzu, huku kwako ukiwa unafukuzana na Baba Mwenye nyumba anakudai kodi, kijana wako wa kwanza aliyehitimu Chuo kikuu anashinda vibanda umiza anabet, wanao wanasoma shule za makabwela kabisa huku akiwa hana uniform za kubadilisha lakini bado unaendelea kupiga Salute kwenye mageti ya viongozi.

Vijana kwa Rasilimali zilizopo hapa nchini hampaswi kukesha mkiwa mna Bet na kuendesha Boda boda. Wafanyakazi kwa rasilimali zilizopo Hampaswi kulipwa mishahara mnayolipwa. Hivyo basi watu kama kina Steve Nyerere na kina Maulid Kitenge ni wa kuwatenga kwenye jamii yetu…. Tunatakiwa tuanze kutokomeza hizi chawa kwanza kabla hatujawafikia Viongozi wetu.

Wakati ukoloni ukibisha Hodi Africa ulikuja kwa njia ya Mikataba. Ndiko tunakoelekea…..

Vijana tuliopo ndani ya CCM ni wakati wa kujitafuta sasa tuache kusifia ujinga wakati taifa limekwama. Tuzungumze, tukatae kabisa kuwa Chawa wa mtu, wakati ni sasa….. kila mtu kwenye familia yake atoe elimu ya Uraia.

Tumekwama kama Taifa….. share

Ole Mushi
0712702602

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni hili Limama baada ya kupata urais wa kimagumashi ndo kila kitu anawapa waarabu! Anabadili sheria ili kuuza kila kitu kwa waarabu!
 
Wakoloni kurudi Kama wawekezaji kwa hisani ya CCM inayojichora kwa picha Kubwa ndio imeleta Uhuru na maendeleo Kama uliyoyaandika.
Bladfakeni.
 
Huo ukoloni urudi mara ngapi??
 
Barikiwa
 
Huo ukoloni maana yake nini!
Ulikujaje hapa kwetu
Je umewahi kuondoka?
 
God forgive us but on the night we got our independence our ancestor were suppose to right the ship. I dont know if we can steer it right at the pace we are travelling.
 
Wenye mamlaka ndio wafanyabiashara. Utawaambia nini? Wao ni faida tu
 
Hii ni laana ya uvamizi inawapiga Watanganyika baada ya kuuwa watu wasio hatia kwa maelfu huku Zanzibar. Wacha karma iwatese
 
Kila kitu kwani hata makalio yako amewapa waarabu ??
Mkuu! Hivi waarabu unawajuaaa au na wewe ni mwarabu ndo maana unawatetea? Waarabu ni mafirauni! Jamii inayojitambua haiwezi kuwakaribisha hawa jamaa! Wakae zao huko na hela yao ya dezo ya mafuta! Ustaarabu wao wa kifirauni haukubaliki popote ndo maana hawapendwi
 
Wanajimbua sasa jambo zuri sana
 
Mkuu! Hivi waarabu unawajuaaa au na wewe ni mwarabu ndo maana unawatetea? Waarabu ni mafirauni! Jamii inayojitambua haiwezi kuwakaribisha hawa jamaa! Wakae zao huko na hela yao ya dezo ya mafuta! Ustaarabu wao wa kifirauni haukubaliki popote ndo maana hawapendwi

Mafirauni wako makabila yote na zaidi ni waafrika na ndio hatuendelei . Tizama nini muafrika kaifanyia Zanzibar toka 1964 mpaka leo , ni mauwaji , kubaka, kutaifisha , na kila uchafu uujuwao , Watu waliwaingilia maiti wakati wa mavamizi.
Wizi ndio kila mahali huko Tanganyika , hujaenda magerezani watu wanalawitiwa . Huyo Slaa wenu sijui kama jamaa hawakumla huko jela , hali ndio hiyo ya muafrika
 
Akili za panya taabu sana. Ni uchoyo na roho mbaya. Wewe kama una pesa nenda Dubai utapata kibali cha kufungua mradi wako chini ya wiki. Sababu wanajua dunia ya sasa sio ile ya kukalia uchumi.
Hakuna nchi inaendelea bila kufunguka na kukaribisha wawekezaji watakao leta mtsji, ujuzi, teknologja n.k.
Hata huko marekani, ulaya, china, india na wengine wote walio na uchumi mkubwa bado wanakaribisha wawekezaji.

Tanzania bado sana, hawa wasomi tulio nao unawsona mwenyewe hawana ubunifu wa maendeleo ila kukwapua pesa na rushwa
 
Umejibu utumbo tena wenye kinyesi
 
Chama cha Mapinduzi kimekuwa cha ajabu sana kwa sera zake. Kama kinaona kimeishiwa sera, sanduku la kura lipo kijitoe muhanga kifie kwenye sanduku la kura kwa heshima. Kila kitu kinafanya uwekezaji kwa wageni, ina maana watanzania hawana elimu ya kuendeleza rasimali za mpaka wasaidiwe ujuzi na wageni? Kuna vyama vina sera tofauti na zao wavipishe kwa heshima kwenye sanduku la kura viongoze nchi. Hii ni aibu kila kitu kuwekezwa kwa wageni kwa hoja kuwa wageni wana ufanisi. Sasa elimu yetu inasaidia nini kama hatuwezi kuendeleza rasilimali zetu kwa ufanisi, nini malengo ya elimu yetu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom