Ukiwa na miaka 35 na ukaamua kuanza moja kabisa, unatakiwa ujipe muda gani kutoboa au approximation ya kutoboa ipoje?

Brojust

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
344
1,003
Yaani

Tayari ngoma inasoma 35, hujajenga, hujaoa, huna kazi, huna biashara, huna connection yoyote.

Ila vitu ulivyokuwa navyo, una kitanda tayari na mashuka yako na baadhi ya vitu vya ndani, Una degree yako moja, umeamua kurudi nyumbani hapa hapa Dar kwa mzee kujipanga upya, mzee nae amekupokea na amekupa support ya kukwambia kaa mpaka pale wewe utakapo amua kuondoka tena na kwenda kuhusle.

Nafsi yako inasema utatoboa ila kila ukishika simu unaona, kuna yule mwanao wa chuo kaoa, mara unaona kuna mwanao wa secondari kanunua Crown athlete then kaandika God is Good.

Wazoefu ebu tupeni mbinu za hali na Mali, mambo yashaharibika huko.
 
Hiyo miaka 35, jishushe miaka 10 alafu fanya kazi zozote halali ambazo zinaendana au kukaribiana na zile unazozipenda..
Angalia manzi mwenye kujiweza kidogo au angalau kwao ugali uwe haukai , mtandike mimba huku unaendelea kupambana
 
Hata miaka 50 unaweza kuanza moja...
Muanzilishi wa KFC ulishasoma story yake?
Miaka 65 hana issue akataka kujiua, miaka 88 akawa billionaire...
Ndio huyo mzee aliyeanzisha KFC ambapo sasa ipo dunia nzima...

It's Never too old to dream...​

g7wvyxfGQVqw56iAHF6S_dave-hoefler-oJ_H_1wkKEs-unsplash-1024x615.jpg
 
Dunia ipo tayari kumpatia mtu yeyote kitu chochote saa yeyote kila anachokitaka kama ukiiomba?

Swali ni jee nawezaje kuomba na nikapata ninavyovihitaji?

Kila kitu ni siri dunia hii, na ukiijua siri utakuwa free kwa yale uliyoyafichwa kutoyajua.

Jifunze kuomba kupata unachokitaka....
 
Kama una nia unatusua kwa muda mfupi sana before 45.

Ila ushauri wangu, unajua Age35 mwanaume anakua na pressure sana ya kumiliki fixed Assets [Kiwanja, Nyumba, Gari, Fridges, L-sofas, 41 nches Tv nk]

Ili uwin sahau kabisa hivyo vitu hapo, utafika muda utaona pesa inaruhusu unavinunua bila kuathiri kipato.

Wewe kazania tu kuweka pesa kwenye biashara, Na Kama unataka kuanzia "0" kabisa bhasi Anza na biashara ndogondogo, Anza kesho.

Save pesa kwa nguvu kadiri uwezavyo, Itumie hiyo pesa kuwekeza zaidi, wekeza, ukipata wekeza, wekeza, wekeza,,,!!

Usikimbilie kununua vitu, kila unachosave save ajili ya kuwekeza tu [Hii mifano tu 👉Tawi lingine la biashara, Ufugaji kuku au Kilimo cha mazao ya bustani like Nyanya, pilipili n.k]


Next5years utakua na kila Asset unayoipenda, Next 10 years utakua Mfano wa kuigwa.
 
Back
Top Bottom