Ukiwa na haya umekula bingo Kwa Zama hizi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,022
62,525
Salama!

Siku hizi nimekua mkubwa, mambo ya kuandika madude marefu nimewaachia wengine. Haya nisipoteze muda.
Siku hizi ukiwa na mambo haya basi jua umeula, umelamba dume, umekula bingo. Ni wewe tuu kuamua utoboe au usitoboe.

1. Kujua kingereza au lugha yoyote kubwa kimataifa.
Achaneni na kile kingereza cha kulambia chumvi nazungumzia ujue kingereza kabisa au lugha kama kichina, kiarabu, kireno au kihispania. Umeula, yaani ushindwe mwenyewe.
Huwezi ukajua kingereza au lugha za kimataifa alafu Maisha yakakushinda.
Tena ukiwa Jiji kama Dar na Arusha. Sio ujue kingereza alafu ukajichimbie Huko mkoani. Utakwama.
Ukijua Lugha ya kingereza, itakupasa uwe na Smartphone au Laptop, itakupasa uwe na Akili ya kuchangamana na watu. Keisha!!

2. Kipaji
Ukijua kuimba, mchekeshaji, kuchora, kusuka, Kwa kiwango cha juu. Maisha yakikushinda umeamua mwenyewe. Tatizo la Vijana wengi wa Kitanzania wanasubiri mpaka wawezeshwe. Utahitaji tuu smartphone na bando lako.
Jitangaze, kuliko ukae hivihivi ni bora utumie muda wako mtandaoni kutangaza kipaji chako.
Nawafahamu Vijana wengi ambao wanapata Milo mitatu na kujitegemea Kwa kutumia vipaji vyao. Huenda sio Pesa nyingi wapatazo lakini hawamtegemei yeyote Yule. Wanajilisha, wanalipa bills na wengine wanategemewa na familia.

Unakipaji cha kuimba alafu umejifungia ndani kama Zoba, unaona aibu kuimba Bar? Club? Sio😂 unataka uimbe wapo Ndugu yangu? Anzia mahali ulipo.

3. Simu yenye Kamera Nzuri.
Kumiliki Simu yenye Kamera Kali ni Bingo ambalo bado Vijana hawajui namna ya Kutumia simu zao.
Epuka kukaa bila kazi, yaani katika Maisha yako yote, epuka kukaa vivihivi,
Chukua simu yako, chagua maudhui unayoyapenda, nakupa Mfano, maudhui ya Maua,
Andika" Tropical Flowers Gallery" hiyo ni mfano WA title ya Page au YouTube Channel. Kisha Anza kupiga picha au video hayo maua ya eneo ulilopo iwe Maua ya Nyumbani au ya porini. Yape Stori, elezea faida ya Maua katika ecosystem.

Jitangaze, jipe kazi. Huwezi ukawa na shughuli ya kufanya ukakosa jina, na huwezi ukawa na jina alafu ukakosa Pesa.

4. Mvuto na Haiba.
Mvuto wa kimaumbile au kihaiba unatokana zaidi na jinsi mtu alivyojipokea na kujikubali.
Ni kweli Wanawake wenye misambwanda na maumbo Fulani wanatutikisa wanaume wengi lakini ukweli uliojificha ni kuwa mvuto wao haupo kwenye misambwanda Yao bali upo katika Ile hali ya kukubali lile tako Lao na kujivunia nalo.
Wanawake wembamba sio kama Hawana mvuto, nop! Ila mtazamo wao kwenye wembamba wao ndio unatufanya wanaume tuwaone Hawana mvuto, nazungumzia kutokujiamini kwao.
Ninawajua Wanawake wembamba wengi warembo ambao Kwa namna wanavyojikubali wakipita Mbele yako lazima uzuzuke.
Mwembamba ili awe na mvuto hatakiwi kutamani misambwanda, na mwenye msambwanda ili awe na mvuto itampasa asitamani wembamba na mambo yake.

Vaa kulingana na body morphology yako, tembea kulingana na Mwili wako, keti Kwa mapozi ya kike kulingana na umbo lako.
Zingatia, Akili na mtazamo ndivyo vinamtambulisha mtu na kumuongoza MTU. Halikadhalika na Rangi nyeupe inaonekana ni nzuri sio Kwa sababu ni nzuri Bali ni comfortability Kwa wenye rangi hiyo. Wanawake weusi kukosa kwao kujiamini ndio huwafanya wasioonekane Waziri. Lakini ninawajua Wanawake ma-black ambao nikiri kuwa Wana mvuto WA ajabu kuliko Wanawake weupe.
Hiyo pia itatumika Kwa wanaume.

Uzuri na mvuto ukiwa nao Maisha hayawezi kukushinda. Hayawezi kuwa magumu. Na uzuri na mvuto upo ndani ya MTU, katika Akili yake. Vile mtu anavyojiona na vile mtu anavyoona wengine. Vile mtu anavyotaka Watu wamuone Kwa jinsi alivyo pasipo Kubadili chochote katika mwili wake.
Hapo kidogo nimeongea mambo ya falsafa.

5. Kuishi Mjini.
Kitendo cha kuishi Mjini moja Kwa moja umelamba dume, mjini ni kama msituni, penye miti mingi kuna Siri ya utajiri. Watu ni miti inayotembea, ukiamua Kupata Dawa no wewe, ukiamua Kupata sumu ni wewe, ukiamua Kupata kivuli ni wewe, ukiamua kukaa juani pia ni wewe.
Laizma ujue mti upi matunda yake yanakuwa na mti upi matunda na majani yake ni Sumu. Lakini haimaanishi mti wenye matunda yenye sumu hauwezi kufaa Kwa matumizi mengine kama Kivuli, kuni au kutengenezea zana kama vile mbao n.k
Hivi nilisema Watu ni kama miti? Ndio Watu ni kama miti ambayo mahusiano yako nao ndio yata-determine Future yako.

6. Ardhi na mashamba.
Ardhi ili iwe na thamani lazima iwe na vigezo muhimu. Kigezo cha kwanza kabisa ni Maji. Ardhi bila ya maji haiwezi kuwa Valuable. Eneo lenye maji ni muhimu kwako kijana bila kujali lipo umbali upi.
Ku- control maji ni ku-control Maisha naam Maisha ya viumbe. Yapo maji ya juu kama mabwawa, maziwa, MiTo, na visima, lakini pia yapo maji ya Chini ya Ardhi, pia yapo maji ya angani ambayo yakishuka huitwa Mvua. Vyovyote iwavyo eneo ulilo nalo lazima liwe na Maji. Mahali penye maji elewa Maisha yanawezekana.
Hallelujah!
Ukishamiliki Ardhi kinachofuata ni kufanya Maisha yatokee, anzisha miradi kama ufugaji kama utaweza, kilimo kama utaweza, fanya kile kilichorahisi kwako.

7. Moyo wa kupenda + Akili ya kudhibiti Moyo.
Upendo utakupa maana ya Maisha, furaha na Raha zipo katika upendo lakini upendo pasipo Akili utakuumiza. Utakufanya upende pasipo hitajika kupenda, utafanya yasiyostahili kufanywa Kwa kisingizio cha mapenzi,
Upendo hupofusha Macho, na Maisha hayawezekaniki pasipo Macho yenye Maono.
Hallelujah!

Nilisema nimekua mkubwa, sitasema mengi.
Acha niipokee Sabato Ndugu zangu.

Leo ninajisikia Kuimba Mno, nitaimba! Nitaimba! Nitaimba!

Nawatakia Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Password nyingi leo Mkuu.
 
Ndugu yako amekufa huko unajifanya kama hujui
 
1683908113266.png
 
Back
Top Bottom