Ukishiba usisahau siku za njaaukiwa na njaa usipoteze tumaini

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
4,177
7,301
Unafahamu ni kwa nini gari jipya kabisa linatoka kiwandani na hook ya kuvutwa? Je watengeneza wa magari hawana imani na kazi yao?

La hasha, watengeneze magari wanaelewa kuwa pamoja na upya wake, pamoja na kuwa ni mashine ya kutegemewa, ipo siku kila gari litahitaji msaada wa kuvutwa!

Inawezekana leo una nguvu nyingi, una afya tele, una pesa, una cheo na utajiri, una watoto na ndugu wengi, nikuibie siri, wakati uko na upya wako - weka akiba akilini, kwenye maneno yako na matendo yako kuwa ipo siku nitahitaji msaada.

Nafahamu na ninafundisha katika nguvu ya ukiri chanya [positive confession] maishani, naelewa wengi wetu wanaelewa kanuni ya kupanda na kuvuna [seed v harvest, sowing v reaping, cause v effect].

Changamoto ya maisha haya ni kutotabirika kwake, hakuna ajuaye kesho yake kwa uhakika - leo unatunza na kufuata kanuni bora za maisha kwa uaminifu, kesho waweza kuzivunja. Katika nusu karne niliyoishi, nimeona masikini wakiwa matajiri na matajiri wakifikwa na umasikini, nimeona matabibu wakiumwa na waliokuwa wagonjwa wakiwa matabibu.

Nimeona wenye mamlaka wakiishia gerezani na wafungwa wakitoka na kuwa wenye mamlaka, nimeona wenye kiburi wakitwezwa na wanyenyekevu waki-inuliwa sana.

Tendea wema watu wote, kuwa mnyenyekevu,tumia uwezo na nguvu ulizo nazo kusaidia/kuinua wengine; tafuta amani na suluhu kwa uwezo wako wote na watu wote kila iitwapo leo kwako. Ukifanya hivyo hata kama hutakuja kuhitaji kuvutwa, utaishi maisha bora ya amani na yenye utoshelevu - hutaogopa kivuli chako.
 
Ni Neno jema na limejaa HEKIMA kubwa.
 
Back
Top Bottom