Mwanamke aliyefundwa akafundika hawezi kupokea au kukagua simu ya mpenzie,ukiona mwanamke yupo hivyo juakuwa amekosa adabu,utii na hafai kukaa naye ndani ya nyumba.
=======
Katika mambo yaliyo magumu kwenye maisha kwa watu walio wengi, basi ni kupekuliwapekuliwa. Wapo wanawake ambao hudiriki hata kuwapekua simu za viganjani za waume zao na kuweka miaka waliyozaliwa, ili ahakiki mumewe ana shilingi ngapi kwenye akaunti yake ya simu yaani Tigo-pesa, Mpesa au Airtel Money.
Utakuta mwanamke anapekua simu ya mumewe au mwanaume anapekua ya mkewe, pengine msichana anapekua simu ya mpenzi wake au mvulana anafanya hivyo. Kupekuliana simu ni sawa?