Ukimya wa Rais Magufuli Ufisadi wa Trillion 8 za Wafanyakazi Wastaafu

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
BARAZA LA WAZEE WA
CHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI NA UMMA

KUHUSU

UKIMYA WA RAIS MAGUFULI UFISADI WA TRILIONI 8 ZA WAFANYAKAZI, WASTAAFU

Ndugu waandishi wa habari, tunapenda kuwashukuru kwa kuitikia wito huu wa kukutana nanyi leo kama ambavyo imekuwa kawaida tunapokuwa na jambo la muhimu kuwasemea wazee wote nchi nzima, kuishauri serikali na jamii yetu juu ya masuala anuai yanayohusu maslahi ya nchi yetu, kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tumekuwa tukitimiza wajibu huu wa kupaza sauti kwa niaba ya wazee wote nchi nzima kwa kuzingatia kauli mbiu ya Baraza la Wazee wa CHADEMA isemayo “Wazee Ni Hazina ya Hekima na Busara”.

Tunapenda pia kutumia nafasi hii ya utangulizi katika mkutano huu, kuunaungana nanyi wanahabari wa Tanzania na wadau wengine wote wa masuala ya habari nchini na dunia nzima kwa ujumla katika kuazimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambayo huazimishwa Mei 3, kila mwaka kwa madhumuni ya kujikumbusha misingi muhimu katika uhuru wa habari, kutathmini mwenendo wa uhuru wa habari kuutetea na kuulinda uhuru huo dunia nzima dhidi ya mashambulio au vitisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao wakitimiza majukumu yao ya kutafuta, kuzalisha na kusambaza habari.

Tunajua hapa nyumbani, Watanzania wanaadhimisha siku hii ya leo wakiwa katika sintofahamu kubwa kwa sababu uhuru wa habari na upatikanaji wa taarifa kwa jumla unapitia katika wakati mgumu kabisa kuliko hata ilivyokuwa wakati wa ukoloni au kuliko enzi za tawala za kidikteta kama akina Benito Mussolini, Adolf Hitler na wengine.

Hujuma, vitisho au mashambulizi dhidi ya haki ya kupata taarifa, uhuru wa habari na wanahabari wenyewe ni mojawapo ya viashiria vikubwa vya jamii inayoongozwa na watawala waliojaa hofu ya kuhojiwa na wasiokuwa tayari kukubali fikra mbadala. Jambo ambalo ni hatari kwa afya ya taifa. Tunaamini kuwa Watanzania wataitafakari kwa kina na kuifanyai kazi kauli mbiu ya wadau wa habari nchini Tanzania kwa mwaka huu, inayosema “KUPATA TAARIFA NI HAKI YA MSINGI, IDAI’.

Tuitumie kauli mbiu hii kuwaambia watawala kuhusu;

 Sheria mbovu zinazominya uhuru wa habari na kukandamiza upatikanaji wa taarifa. Mf;

 Sheria ya Magazeti

 Sheria ya Takwimu

 Sheria ya Makosa ya Mitandao

 Kuzuia upatikanaji wa habari za bunge na taarifa kuhusu wawakilishi wetu wanavyofanya kazi.

 Kuzuia vikao vya bunge kuwa ‘live’

Kuwa hivyo ni viashiria vya kuturudisha nyuma na si kwenda mbele na kamwe hatuwezi kuwa mfano wa kuigwa na watu makini wanaofikiria ustawi wa jamii zao vizazi vingi vijavyo na kwamba tunalaani vikali kurudisha nyuma demokrasia.

2.0 Ukimya wa Rais kuhusu ufisadi wa Trilioni 8 za Wafanyakazi, Wastaafu.

Ndugu wanahabari, baada ya kuzungumzia kwa kirefu kuhusu hali ya uhuru wa habari nchini kutokana na umuhimu wake, tunaomba kuzungumzia hotuba ya Rais J.P. Magufuli aliyoitoa kwa taifa, Siku ya Mei Mosi ambayo hutumika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani.

1. Tunawashukuru wadau wa maslahi ya wafanyakazi wa nchi hii, hususan wachumi ambao wameonesha kwa hesabu zilizo wazi kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushusha kiwango cha kodi ya PAYE kwa asilimia 2 (ambazo ni pesa kidogo) bila kuboresha mishahara ni utani kwa wafanyakazi wanaoendelea kuhangaika na kima cha chini ambacho bado hakitoshelezi mahitaji.

2. Kwa niaba ya Wazee, tunamsihi Rais Magufuli kutoa kauli juu ya hatma ya trilioni 8.43 ambazo ni jumla ya deni kwa mujibu taarifa ya CAG, ambalo Serikali inadaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Wafanyakazi na wastaafu walitegemea kumsikia Rais akizungumzia suala hilo siku ya Mei Mosi.

3. Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa ikiitaka Serikali kufanya jitihada za haraka za kunusuru uhai wa mifuko hiyo kwa kulipa fedha walizochota kwa ajili ya uwekezaji katika miradi mikubwa mingine ikiwa haina tija na iliyojaa harufu ya ufisadi mkubwa.
4. Deni hili sugu la serikali yanatishia uhai wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini. Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko hiyo (SSRA) iliwahi kutoa angalizo kwa serikali kuwa iwapo serikali haitalipa madeni hayo itakwamisha mifuko hiyo kuwalipa mafao wanachama wake, kujiendesha yenyewe na hata kuwekeza zaidi. Taarifa zinasema kuwa fedha zingine zimekopwa na serikali bila hata ya kuwepo kwa mikataba. Huu ni ufisadi. Hizi sio fedha za serikali.
5. Madhara ya hali hiyo yako wazi. Yamesababisha kumekuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wastaafu kuhusu ucheleweshwaji wa mafao yao na hata wengine kufariki dunia kabla ya kupata malipo yao.

6. Kuchelewesha malipo ya mafao ya wastaafu husababisha usumbufu mkubwa na hata kuwaathiri kisaikolojia na kiafya na kuwafanya waishi maisha ya mateso katika umri wao wa kustaafu ambao walipaswa kuangaliwa vizuri na kufurahia mafao yao.

7. Ni madeni haya sugu ya serikali kwa mifuko, yamesababisha kuwepo na mlolongo wa muda na urasimu mkubwa kwa wazee kupata malipo ya mafao, wakati katika nchi zingine inachukua mwezi mmoja tu mtu kupata mafao yake.

8. Mbali ya kutoa kauli, pia kwa sababu ya kuwepo kwa maneno mengi yanayoashiria kuwepo kwa harufu ya ufisadi katika baadhi ya miradi hiyo, Wazee tunamsihi Rais Magufuli kumwagiza CAG afanye ukaguzi maalum katika madeni hayo ya serikali kwa mifuko ya jamii.

3.0 Michango ilizokusanywa na Mifuko ya Hifadhi Jamii kutoka kwa wafanyakazi hewa zitumike kutoa pensheni kwa wazee wote nchini.

Katika hotuba yake hiyo kwa taifa Siku ya Wafanyakazi, Rais Magufuli alisema wafanyakazi hewa wamekuwa wakilipwa shs bilioni 11.6 kwa mwezi, sawa na sh Billioni 139.2 kwa mwaka na sh billioni 696.1 miaka mitano.

Kwa mantiki hii inamaana kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikipokea michango ya wafanyakazi hewa, ukichukulia mchango wa asilimia 10% kila mwezi kwa kila mfanyakazi kwa mijibu wa sheria, utakuta mifuko ya hifadhi ya jamii imekua ikipokea Sh. Billioni 1.16 kwa mwezi, na Sh. Billion 13.92 kwa mwaka sawa na Sh Billioni 69.61 kwa miaka mitano kwa kutumia takwimu za Mh. Raisi hapo juu.

Baraza la wazee CHADEMA linapendekeza michango hii ya wafanyakazi hewa iliyokusanywa na mifuko ya jamii kwa muda mrefu ifuatiliwe na itumike kuanzisha mfuko wa Pensheni ya Wazee wote nchini (wale waliofanya kazi kwenye sekta rasmi na sekta zisizo rasmi) ambacho kimekuwa ni kilio cha wazee cha muda muda mrefu.

Msingi wa kutoa pensheni jamii kwa wazee wote unatokana na hali halisi na changamoto zinazowakabili wazee katika maisha yao pia ni haki yao kwa mujibu wa Azimio la Kimataifa la Haki za Bina Binadamu la mwaka 1948 ibara ya 25 inatamka haki ya hifadhi ya jamii wakati wa uzee.

Mwisho
Imetolewa leo Jumanne, Mei 3 na;

Rodrick Lutembeka
Katibu Baraza la Wazee CHADEMA
 
Hiyo pesa ya watumishi Hewa ilippigwa na Dau na wenzake akina Magoli haipo ilishaliwa na wajanja na ingine ilitumika kwenye kampeni hivyo hakuna kitu hapo zaidi ya Dau na wenzake kupelekwa Jela, vinginevyo atalindwa kama lugumi.
 
Pesa yote imeibiwa kifisadi hiyo pesa ya watumishi Hewa walikuwa wanajua kuwa ni Hewa na walitafuna mafao yao wakiwa wanajua kila kitu.
 
Hiyo pesa ya watumishi Hewa ilippigwa na Dau na wenzake akina Magoli haipo ilishaliwa na wajanja na ingine ilitumika kwenye kampeni hivyo hakuna kitu hapo zaidi ya Dau na wenzake kupelekwa Jela, vinginevyo atalindwa kama lugumi.
Kumbe nimaigizo tu tunafanyiwa
 
Jamaa Hana hata mwaka mnambebesha kila mzigo mnaokutana nao, sasa akideal na mauchafu ya watu wengine lini atatekeleza ya kwake walioahidiwa watu. Halafu akijakushindwa pia mtaanza kumkejeli kama waliopita.
 
Wazee wa Jumuia ya Afrika Mashariki EAC iliyovunjika 1977 walipokonywa mafao yao pale Serikali ya TZ ilipoamua kutowalipa kwa visingizio chungu nzima. Mbaya zaidi mwaka 1995/6 Awamu ya Mkapa ilipoamua kuwalipa, ikawa viroja vitupu!
1. Idadi ya wahusika ilikuwa watu 15,000 lakini waliongezeka karibu mara 2 ya hao, wakawa +-30,000!
2. Serikali ilitenga sh. 417 bilioni kwa hesabu za mafao ya hao watu 15,000 ambapo kama wangelipwa flat rate kila mmoja angelipwa 27,800,000/=
2. Malipo yalifanywa kwa kila mtu sh. milioni 2 ambazo waliambiwa ni 'nauli'! Sijuwi ni ya kwenda wapi na kwa usafiri wa aina gani!
3. Matokeo yake hata wasiostahili walilipwa kama fedha hiyo haikuwa na mwenyewe!
4. Watu haohao waliostaafu chini ya Shirika la Reli Tanzania wapatao 800+ baada ya kuona usumbufu waliopata katika mafao ya EAC waliomba walipwe mafao ya TRC kwa mkupuo ili waachane na Serkali kwa vile TRC ilikuwa inabinafsishwa. Serikali ikakataa, kwa madai kwamba ati watu wangelipwa hivyo kuna wengine wangemaliza fedha hizo na kuomba warudishwe kwenye malipo ya kila mwezi!
5. TRC ilipobinafsishwa mwaka 2008 (kama sikosei), Serikali iliwalipa kwa mkupuo waliopunguzwa ambao walikuwa na umri wa kustaafu!
6. Wale 800+ walioomba walipwe kwa mkupuo wakaomba na walipwe salio la pensheni zao ili wasiendelee kusumbuka kwa ucheleweshaji wa mafao kila wakati.
7. Jibu walilopata ni kwamba fedha liyotengwa kwa malipo yao kwa mkupuo T. Sh. 51 bilioni zilitumiwa kununulia mafuta ya kuendeshea treni!
8. Wazee hao walifuatilia suala hili ofisi ya Waziri Mkuu ambayo iliwaandikia Hazina, Wizara husika na RAHCO kwamba ni nani aliyebadili uamuzi wa Serikali na kutowalipa wazee hao; ambapo Hazina, RAHCO na Wizara husika wote hawakujibu barua hiyo ya Waziri Mkuu.
9. Baada ya muda; Wenzetu hao waliolipwa kwa mkupuo walirudishwa katika utaratibu wa malipo ya kila mwezi kwasababu Serikali iliwakubalia ombi lao baada ya kuishiwa malipo ya ya mkupuo!
10. Wastaafu wale 800+ wa EAC wakaandika barua ya kulalamika kwamba hawakutendewa haki kwasababu wenzao wamelipwa mara mbili kama nilivyoeleza hapa juu. Lakini mpaka leo hawakujibiwa.
11.Ni wazi kwamba sehemu kubwa ya fedha ya mafao ya EAC zililiwa na wajanja.
12. Hata zile bilioni 51 zilizotengwa kwa malipo ya mkupuo nazo huenda wajanja waligawana. Kama sivyo barua ya Waziri Mkuu ingejibiwa kuondoa utata.
13. Kuna majipu makubwa mawili au zaidi hapa: a. Mafao ya wastaafu wa EAC bilioni 417 na b. Mafao baada ya kubinasfsishwa TRC bilioni 51.
14. Inabidi CAG akague na kuhakiki mahesabu ya wahusika wa hizi fedha tujuwe kama hakukuwa na majipu humo.
15. Pamoja na hayo hapa juu, ucheleweshaji wa malipo ya Pensheni za hawa wazee unakera sana. Lakini haijulikani ni nani hasa kati ya RAHCO, Wizara ya Uchukuzi au Hazina wa kuulizwa kuhusu jambo hilo. Mzee wa kijijini Mwanza, Mbozi au Nachingwea kw mfn akitangulia mbele ya haki, warithi wake watamuuliza nani kuhusu mafao ambayo alistahili kulipwa siku au miezi kadha iliyopita? Hapa kunaweza kuwa na wastaafu hewa wengi tu.
MH. JPM TAFADHALI CHUNGUZA HAPA KWA UMAKINI WAKO.
 
Watu hawafahamu maana ya deni la taifa, wanadhani unakopa unanywea then utalipa kutokana na mapato yako
Mikopo yote ya deni la taifa either iwe ya ndani(mifuko ya bima na mabenk) na ya nje(mabenk ya nje na nchi wahisani) inatumika kuendeleza.miradi flani ambapo mapato kutoka kwenye miradi hiyo ndo yanatumika kulipa deni hilo na si kusanyo la kodi ndo linalipa mikopo hiyo
Mfano mdogo, katika ujenzi wa bomba la mafuta kutoka mtwara mpaka kinyerezi, kulikuwa na mkopo kutoka bank ya China then umeme ukianzwa kuzalishwa Tanesco inabidi walipie gharama za uzalishaji umeme na hizo gharama ndo zinatumika kulipa deni la wachina
So baada ya miaka 20, deni la bomba la mafuta litaisha na hapo ndipo nchi itapata faida kutokana na bomba hilo the same applied kwa miradi mingine kama vile ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma .......
 
Sasa hi inahusikaje na mada?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…