Ukimwangalia hapa Janabi. Ni kielezo cha Afya Bora ambalo Taifa linapaswa kuwa na watu wa namna hii.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
7,869
16,913
Janabi amekuwa akisisitiza sana ulaji mwema. Na "LISHE BORA" Huyu mtaalamu wa Vyakula na Lishe.

Hivi ndivyo anatamani watanzania wote tuwe, tuwe na mwonekano huu wa Siha njema na Afya pia. Nawaza katika umri wake huu wa miaka 65 plus nadhani watanzania tuna mengi ya kuiga. Sijajua mkewe ana umri gani.

Screenshot_2024-08-15-10-43-02-501_com.android.chrome~2.jpg
 
Janabi amekuwa akisisitiza sana ulaji mwema. Na "LISHE BORA" Huyu mtaalamu wa Vyakula na Lishe.

Hivi ndivyo anatamani watanzania wote tuwe, tuwe na mwonekano huu wa Siha njema na Afya pia. Nawaza katika umri wake huu wa miaka 65 plus nadhani watanzania tuna mengi ya kuiga. Sijajua mkewe ana umri gani.
Huyo mnubi wa sudani kusini, ndio wengi wao miili yao ilivyo.
 
Janabi amekuwa akisisitiza sana ulaji mwema. Na "LISHE BORA" Huyu mtaalamu wa Vyakula na Lishe.

Hivi ndivyo anatamani watanzania wote tuwe, tuwe na mwonekano huu wa Siha njema na Afya pia. Nawaza katika umri wake huu wa miaka 65 plus nadhani watanzania tuna mengi ya kuiga. Sijajua mkewe ana umri gani.

View attachment 3070492
Miili ya aina hii huwa inastahimili sana shuruba za uzeeni.
Sawa na mzee Joseph Warioba.
 
Mbona kuna mdau kule juu kampa uasili wa Sudan? Hatari sana nchi hii.
Profesa Janabi apokewa kwa shangwe kijijini kwake
By Gidion Mwakanosya , Nipashe
Published at 09:25 AM Jul 29 2024

MKURGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi, juzi aligeuka kivutio kijijini kwake Mtakanini, Kata ya Msindo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, ambako na timu yake ya wataalamu walikwenda kutoa huduma za afya.

Wananchi hao walifurahi kumwona mtoto wao ambaye ni maarufu kwa kutoa ushauri wa kutunza afya kwa kula vyakula vinavyofaa na umuhimu wa kufanya mazoezi, huku wakishukuru kwa uamuzi huo na kuomba muda zaidi kwa wataalamu kutoa huduma.

Daktari huyo bingwa ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ni mzaliwa wa kijiji hicho ambaye elimu yake ya msingi alianzia kijijini hapo.

Prof. Janabi alikwenda kuungana na madaktari bingwa watatu waliokuwa wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo, kisukari, tezi dume na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa gazeti hili, wananchi hao walisema wamefurahishwa na mtoto wa nyumbani kuwakumbuka na kutumia utaalamu wake na wenzake kwenda kuwasaidia.

“Tulimsubiri yeye na wataalamu wengine kwa hamu kubwa. Wamekaa nasi kwa wiki moja tunatamani wangeendelea kukaa nasi au kwenda kwenye vituo vingine. Tunatamani mpango huu uwe endelevu tupate alimu ya afya kama anavyotoa kwa wengine huko aliko,” alisema Cartas Nyoni.

“Profesa Janabi ni mwanetu, amekuja kwa muda mfupi tunatamani angekaa muda mrefu ili watu waelewe vizuri, tunawaomba wawe wanatutembelea wakiwa na vifaa vya kisasa kama walivyokuja navyo sasa. Wananchi wanyonge wamepata huduma vizuri na bure wangekwenda kwenye vituo vya afya, hospitali za rufani wangetozwa fedha nyingi, tunaomba huduma kama hizi kwa wananchi tunaoishi vijijini,” alisema.

Aidha, wameishuruku Wizara ya Afya na kuomba kusogezewa huduma ya madaktari bingwa kwa watu wanaosumbuliwa na moyo, saratani ya kizazi na tezi dume kwenye vituo vya afya wilayani humo.

Diwani wa Kata ya Msindo, Remna Nchimbi, alisema kuwa kitendo cha serikali kuwaleta madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kimeleta matumaini makubwa kwa wananchi ambao wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa ambayo yanahitaji kuonwa na madaktari bingwa kwa lengo la kupata tiba ambao wako mbali na maeneo ya vijiji.

Diwani Nchimbi aliiomba wizara iangalie uwezekano wa kuwa na mpango endelevu kwa madaktari bingwa ambao wako kwenye hospitali za rufani ikiwamo MNH kufika kila mara kwenye vituo vya afya kutoa huduma kwa wagonjwa ili kupunguza changamoto zinazowakabili za kufuata huduma hiyo kwenye hospitali za juu.

Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Vita Kawawa, alisema amefurahishwa na kazi nzuri zilizofanywa na madaktari bingwa ambao walianza kazi hiyo ya kuwa hudumia wagonjwa wa magonjwa ya moyo, kisukari, saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake na tezi dume.

Alisema Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo na baadaye walikwenda kutoa huduma hiyo kwenye Kituo cha Afya Lusewa pia walitoa huduma kwenye Vituo vya Afya Mputa na Mtakanini na kuleta faraja kwa wananchi.

Aidha, wananchi hao walikuwa wakishindwa kupata tiba kutokana na gharama kubwa ya matibabu ambayo kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja imetolewa bure.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mtakanini, Profesa Janabi baada ya kupokewa na mamia ya wananchi, alisema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri ya afya kuanzia kwenye zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na Hospitali za Rufani ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Profesa Janabi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kuwa kila mtu anapaswa kutunza afya yake kwa kula vyakula ambavyo si hatarishi kwa afya ili wnanchi waache kula vyakula bila kufuata utaratibu.

Aidha, alisema ni vyema kuepuka kula vyakula vyenye sukari nyingi kwa kuwa sukari haijawahi kumwacha mtu salama.
 
Huyo ni mtu wa Dodoma, na asili yake ni mnubi.

Usidanganye watu. Hata jina linakusuta, kuna mngoni akaitwa Janabi?

Back
Top Bottom