Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 95
- 68
UKISHINDWA KUJIBU HOJA, TAFSIRI YAKE HOJA ZILE NI HOJA ZA UKWELI
Hoja nyingi huwa na uchungu kwa sababu zinabeba ukweli unaoumiza. Hatupaswi kuukwepa ukweli, kwani ukweli wa jambo ndio haki yenyewe. Haki hutetewa, na tukishindwa kuitetea haki, tunakuwa viumbe wa ajabu kabisa, ambao tunapaza sauti kuinadi haki huku tukiikumbatia batili.
Nakumbuka tarehe 07/10/2024, Mheshimiwa Rais Albert John Chalamila, Rais wa Mkoa wa Dar es Salaam, alikabidhi vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi. Alisema, Sasa hoja yangu ya msingi inapofikia pahala ambapo pana kweli na haki, ni muhimu tukafanya hivyo. Hii inatufundisha kwamba tunapofika kwenye ukweli na haki, tunapaswa kutetea kwa nguvu zote.
Uzalendo wa mtu yeyote unapatikana kwanza katika kujitoa, kutenga muda, kusoma maandiko ya mifumo ya nchi, na kuyatii. Huu ni uzalendo wa kweli, ambao unalinda dhidi ya upindishwaji unaoweza kufanywa na watu wanafiki. Hawa ni watu wavaa ngozi ya mwanakondoo, wenye mionekano ya utakatifu, lakini ndani yao ni watumishi wa shetani, wenye roho mbaya, wabinafsi, wachoyo, na wenye kulindana hadharani katika maovu yaliyo wazi.
Ili kukabiliana na watu hawa, lazima tuonyeshe uzalendo kwa kusoma vitabu na makala za aina mbalimbali zenye elimu. Hii itatusaidia kujibu hoja zao za kishetani na kupangua kila upotoshaji wanaoufanya. Bila kupangua hoja za hovyo, basi hoja zile zitageuka kuwa za ukweli, kumbe siyo.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika uzinduzi wa Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Ikulu Dar es Salaam, tarehe 07/10/2024, alisisitiza, Tuendelee na moyo huu wa kizalendo kwa nchi yetu. Maneno haya ya Rais yanaonesha mitazamo mipana kwa maslahi ya nchi. Uzalendo wa kweli ni kutanguliza hofu ya kumhofu Mwenyezi Mungu na utii kwa mifumo ya nchi, huku tukitenda haki. Huu ni uzalendo wa kuwatenga wajiitao wazalendo lakini ni machawa wasiojenga hoja zenye mashiko kuhusu taifa letu.
Nakumbuka tarehe 24/09/2024, Mheshimiwa Jumaa Aweso, Waziri wa Maji, alikubali kwamba, Rais aina ya Daktari Samia Suluhu Hassan hapatikani kila mahala, hapatikani kila wakati. Kumpata Rais aina ya Daktari Samia Suluhu Hassan ni baraka. Hii inaonyesha kuwa kumshika Rais wetu ni kumtanguliza mbele yetu kwa upendo, kutafakari kiapo cha Rais alichokiapa na kutekeleza kauli zake kwa vitendo, bila kuzigeuza kinyume.
Kumshika Rais wetu kwa maana halisi ni kutafakari maandiko ya kimfumo na kuyayiishi tukiwa tumetanguliza hofu ya Mwenyezi Mungu mbele, kwa imani ya dini ya kila mmoja. Hii ndiyo maana ya kumshika Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhati ya mioyo yetu huku tukijibu kila hoja kwa uelewa wa kisheria, usio kiuka mifumo.
Tarehe 07/10/2024, Mheshimiwa Rais Albert John Chalamila alikabidhi vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi. Alisema, Tujifunze saana ku-develop vijana wetu wenye talents ya kuongea vitu hadharani kwa usomi na kwa hoja, sio kubwabwaja tu maneno kama vile huelewi direction ya taifa letu. Kama kweli umesoma, kapambane na wasomi wenzio.
Hoja ikileta changamoto, mtu mwenye akili timamu na uwezo wa kufikiri, atatafakari neno moja baada ya jingine, sentensi kwa sentensi. Sio kurupu kurupu umjibu tu kisa unaona kuna mahala unajikomba. Hii inakuaibisha na kukuonyesha useless miongoni mwa watu wasio na maana. Ukiona hoja ikikugonga kimya, ujue kwamba hiyo hoja ni ukweli unaokuumiza. Badilika iwapo hoja inakutaka hivyo, kwani hoja ambayo haijibiwi inakuwa ukweli.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mathias Mugerwa Kahinga