Ukikosa raha au amani kazini, utachukua hatua gani kukabiliana na hili?

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,147
2,630
Wakuu!

Habari zenu? Poleni kwa changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwa ni lengo kuweka sawa maisha yaende vizuri.

Bila kuchelewa, kuna hili la kukosa amani au raha au furaha uwapo maeneo ya kazi.

Wewe binafsi unachukua hatua gani kukabiliana na changamoto hili?

Karibuni...
 
Me Iliwah Kunitokea, Nikaandika Barua Ya Kuacha Kaz Bila Hata Kujua Naenda Wap. Sababu Inaweza Kuwa Masilah, Kashfa, Utendaj Wa Kazi, Mahusiano Kazini, Au Jamii Inayozunguka Sehemu Ya Kazi, Nk Me Nafkr Niwakati Wa Kupata Ushaur Na Saa Kutoka Kwa Watu Wenye Hekma Maa Unakua Umeathrika Kisaikoloj Na Utendaj Kaz Wako Unakua Umepungua, Au Kuanza Kuangalia Mahala Pengine Pa Kupata Mkate Wako Kwa Utaratibu. Kamwe Uckimbilie Kuacha Kaz Kabla Hujapata Shughuli Nyingine Ya Kufanya
 
Aisee kuna sehemu nilifanyaga kazi mwaka nikaona kama karne nzima nilivokuja kuondoka mpaka mkurugenzi aliuliza unajua unachokifanya (nikamwambia tu yes I know just let me go) japo alikuwa hataki kabisa nisepe mana nilikuwa zaidi ya asset kwao. nahisi kuna sehemu nyingine zinakuwaje sijui hata leo ukiniuliza kwa nini ulisepa sina jibu la kukupa
 
ni kawaida ila huwa hakuna furaha ya kudumu wala huzuni ya kudumu itatokea wakati utayazoea mazingira kama itashindikana tafuta kazi nyingine kisha ondoka hapo psychological torture si kitu kizuri
 
Inatokeaga. Mimi ilishawahi kunipata hali kama hiyo ya kukosa amani kazini. Nilitaka niche kazi au kuhama hiyo sehemu. Ilibidi nimwone mshauri wangu wa Kiroho,Padre(mimi Mkatoliki). Aliniambia nifanye bidii kwenye ibada/sala, niwahi kazini/eneo husika kwa wakati na kuifanya kazi yangu kwa uweledi wangu wote, wateja wangu wawe marafiki zangu. Niache kushiriki mazungumzo kwenye makundi kazini. Hakika nilifanikiwa, ni zoezi gumu,lakini niliweka nia. Namshukuru Mungu,Mei mosi hii nilikuwa mfanyakazi mahiri.
 
Kama kazi huipendi
au workmate huwapendi bora kuacha kazi
 
Kitu gani hasa kinapelekea ukose amani au inatokea tu ukifika kazini amani inatoweka bila sababu?pole mkuu
 
Chukua livu/likizo upumzishe akili yako,huenda ukarudi na fresh mind na kila kitu kikawa sawa,jaribu kua unafanya mazoezi ili kujiweka sawa kimwili na kiakili.
 
Solution ni kuacha kazi, lakini usifanye makosa ya kuacha kazi kabla ya kupata nyingine. Na hilo la kukosa amani na raha haliwezi kurekebishwa?

 
Meditation..Mazoezi na kwa mtaalamu wa saikolojia kwa sana vinahusika
 
Solution ni kuacha kazi, lakini usifanye makosa ya kuacha kazi kabla ya kupata nyingine. Na hilo la kukosa amani na raha haliwezi kurekebishwa?
Kurekebishwa kupo, kuna wengine wana njia nyingi za kurekebishwa kuliko nazojua mimi mkuu BAK
 
Pole sana...solution uliyochukua ilisaidia?
 
Kitu gani hasa kinapelekea ukose amani au inatokea tu ukifika kazini amani inatoweka bila sababu?pole mkuu
Inatokeaga tu bila hata sababu, unakuta wakati mwingine hujakorofishana na mtu yeyote
 
Daaa kweli me nakumbk mwak Jan hali hiyo ilinitokea njombe ila niliomb uhamisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…