Ukijihisi una wito wa kuwa kiongozi wa kisiasa usisite, thubutu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
18,819
21,000
Dhamira yako ya ndani kabisa, ikupe ujasiri wa kuanzia hapo ulipo, tena kwa mambo madogo kabisa yaliyo ndani ya uwezo wako. Mawazo yako, maono yako, ubunifu wako, ushauri wako, ujengaji hoja wako uthubutu wako kwa maneno na matendo ndio viwe vyanzo vya ushawishi wako kwa jamii. Hicho ndicho kiwe kipimo cha umahiri na uwezo wako katika uongozi, zaidi hata ya vyeti vya mashahada ulonavyo..

viongozi wengi vijana wenye umri wa kati, hasa katika nyakati hizi, wenye uthubutu katika kubuni, kuamua na kutenda mambo madogo kwa bidii na uaminifu, kwa maneno na matendo, wameaminika zaidi kwenye mambo makubwa na kua tushio kwa wanasiasa wazoefu wa muda mrefu, wenye elimu, vyeo na majina makubwa, hali ya kua utendaji kazi wao ni wa kawaida tu, tena ni ule wa kutimiza wajibu na majukumu, kulingana na taratibu na sheria, lakini ubunifu na uthubutu wa kufanya zaidi ya hapo ukiwa hakuna kabisa miongoni mwao...

hakuna cha maana cha kukumbuka katika uongozi wao...

nashauri vijana wenye wito, nia na malengo ya kua viongozi wa kijamii katika siasa, wasikatishwe tamaa au kutishwa na wenye fikra ya kwamba ni lazima uwe na fedha au mali ndipo uwe na uwezo wa kuingia kwenye uongozi wa kisiasa. au kwamba ni lazima ushiriki mambo ya kishirikina ili upate uongozi. Hapana so kweli.

Amini Mungu, vaa ujasiri na uthubutu katika kutimiza ndoto na nia yako ya kua kiongozi wa kisiasa sasa, na kama sio sasa basi ni sasa hivi.

kamwe usiogope kushindwa, jaribu tena na tena, na Kwa Neema na Baraka za Mungu nawe utakua kitu mbele ya vitu, katika muda muafaka wa Mungu, hujachelwea.

This is your time,
nakutakia kila la kheri katika maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu2024, na vile vile nakutakia maandalizi mema sana ya uchaguzi mkuu oct.2025.
 
Dhamira yako ya ndani kabisa, ikupe ujasiri wa kuanzia hapo ulipo, tena kwa mambo madogo kabisa yaliyo ndani ya uwezo wako. Mawazo yako, maono yako, ubunifu wako, ushauri wako, ujengaji hoja wako uthubutu wako kwa maneno na matendo ndio viwe vyanzo vya ushawishi wako kwa jamii. Hicho ndicho kiwe kipimo cha umahiri na uwezo wako katika uongozi, zaidi hata ya vyeti vya mashahada ulonayo..

viongozi wengi vijana wenye umri wa kati, hasa katika nyakati hizi, wenye uthubutu katika kubuni, kuamua na kutenda mambo madogo kwa bidii na uaminifu, kwa maneno na matendo, wameaminika zaidi kwenye mambo makubwa na kua tushio kwa wanasiasa wazoefu wa muda mrefu, wenye elimu, vyeo na majina makubwa, hali ya kua utendaji kazi wao ni wa kawaida tu, tena ni ule wa kutimiza wajibu na majukumu, kulingana na taratibu na sheria, lakini ubunifu na uthubutu wa kufanya zaidi ya hapo ukiwa hakuna kabisa miongoni mwao...

hakuna cha maana cha kukumbuka katika uongozi wao...

nashauri vijana wenye wito, nia na malengo ya kua viongozi wa kijamii katika siasa, wasikatishwe tamaa au kutishwa na wenye fikra ya kwamba ni lazima uwe na fedha au mali ndipo uwe na uwezo wa kuingia kwenye uongozi wa kisiasa. au kwamba ni lazima ushiriki mambo ya kishirikina ili upate uongozi. Hapana so kweli.

Amini Mungu, vaa ujasiri na uthubutu katitka kutimiza ndoto na nia yako ya kua kiongozi wa kisiasa sasa, na kama sio sasa basi ni sasa hivi.

kamwe usiogope kushindwa, jaribu tena na tena, na Kwa Neema na Baraka za Mungu nawe utakua kitu mbele ya vitu, katika muda miafaka wa Mungu.

This is your time,
nakutakia kila la kheri katika maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu2024, na vile vile nakutakia maandalizi mema sana ya uchaguzi mkuu oct.2025.

upo sahihi Mkuu.

2025 lazima uingie Bungeni.
Mikakati ya USHINDI ni nimikubwa Sana.
 
Huu uzi umebeba funzo kubwa na binafsi umeniongezea kilomita nyingi sana katika kutekeleza yote uloyoyashauri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom