Ukifuatilia ripoti za ukasanyaji kodi, mapato na mikopo, Tanzania tungekuwa mbali sana kimaendeleo

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
538
815
Ingawaje nchi nyingi za Afrika ni maskini huku miundombinu, huduma za msingi zikiwa hafifu na wananchi wengi kuishi katika umaskini wa kutisha, viongozi wa Afrika wanafahamika kwa kuishi maisha ya anasa, wanamiliki makampuni na biashara na majumba/magari ya kifahari ambayo hayaendani na mishahara yao kama watumishi wa umma walio kwenye nchi maskini.

Ukifuatilia ripoti za ukasanyaji kodi na mapato mengineyo pamoja na mikopo, Tanzania tungekuwa mbali sana kimaendeleo.

Hali ni tofauti sana kwa kuwa kuna wananchi wachache ambao hawaridhiki na wanacholipwa na hivyo kuwa wezi, wala rushwa na mafisadi wakubwa.

Leo rais kakiri kuwa pesa inatafunwa sana?

Tuachane na mikopo, tusimamie makusanyo ya ndani. Hakuna faida yoyote kwa rais kujisifu kuwa anakuwa na Safari za nje ya nchi kwenda kutuombea mikopo.

Rais abaki nchini asimamie vizuri kinachokusanywa ndani. Tutachukua mikopo baada ya thorough analysis na kujua the gap.
 
Back
Top Bottom