Ukiagiza bidhaa au gari na ukakwama ushuru ni vyema baada ya gari kufika ukapeleka Bonded Warehouse.

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
5,392
13,899
Kama umeagiza gari au bidhaa na ikawa imefika Kwenye Bandari na wakati huo pesa ya ushuru umepungukiwa,kukwama au hukuwa na taarifa sahihi za ushuru na makadirio ya kodi yamekuja zaidi ya kiwango ulichopanga njia sahihi ni kumwambia wakala wa Forodha(Clearing Agent) afanye maombi (TRA) ya kupeleka gari au mzigo kwenye Bonded Warehouse.

Bonded Warehouse ni ghala au sehemu ambayo mizigo inayosafirishwa nje au iliyotoka nje ya nchi inatunzwa inaposubiri kulipiwa ushuru.Bonded Warehouse zipo ambazo zinamilikiwa na serikali au watu binafsi zipo mikoa yenye bandari na mipakani.

Endapo umeagiza gari au bidhaa yoyote na umekwama pesa kabla au baada ya mzigo kushuka bandarini usipate pressure. Inatakiwa umwambie Clearing Agent atafute Bonded Warehouse kwa ajili ya kuweka gari au mzigo wakikubali kuna nafasi, inabidi ajaze fomu ya TRA kuomba kupeleka mzigo Bonded Warehouse baada ya kupeleka mzigo Bonded utakapo kuwa sawa utalipa kodi hata baada ya mwaka na mzigo wako utatoka.

Faida za kutumia Bonded Warehouses
1. Gharama za kutunza mzigo (storage charges) zipo Chini na zina chajiwa kwa mwezi. Mfano gari ndogo kwa mwezi bei ni usd 80, wakati bandarini kutunza kwa mwezi bei ni kubwa sana na huchajiwa kwa siku na ukubwa (CBM) unaweza ukapewa bill ya usd 1000

2.Inaondoa mzigo kuwekwa kwenye list ya overstayed good na kuja kupigwa mnada. Mzigo ukikaa sana bandarini unaingia kwenye overstayed goods na mmiliki asipo utoa unapigwa mnada. Kwenye Bonded Warehouse mzigo unaweza kutunza zaidi ya mwaka

3. Mmiliki wa mzigo ni rahisi kwenda kuangalia mzigo au gari yake ikiwa Bonded Warehouse. Gari ikiwa bandarini mmiliki hawezi kuingia kuona gari au mzigo, ila ukiweka bonded unaomba kuingia Warehouse na kuona mzigo ila huwezi kutoa. Pia akitaka auze ni rahisi kumuonyesha mteja gari au bidhaa ikiwa Bonded tofauti na ikiwa bandarini inabidi auze kwa kutumia picha za mzigo ulikopakiwa na documents za mzigo.

Bonded Warehouse ina faida kwa waagizaji wa bidhaa na magari, inaepusha mizigo kuuzwa kwa mnada. Kama ulifanikiwa kuagiza gari ya usd 3000 (CIF) bora upeleke Bonded Warehouse ukalipe usd100 per month kuliko kuiacha bandarini ukaja kupewa storage charges za usd 3500 na ushuru unakusubiri. Hapo gari inaingia kwenye mnada unaingia hasara
 
Ushauri wako ni mzuri unaweza kusaidia vijana wakurupukaji kupunguza hasara.

Yaani, kwa nini uagize gari au mzigo wakati huna uhakika wa pesa ya kutolea?

Hizi ni akili za kimaskini. Mtu mwenye akili za namna hii hawezi kupata maendeleo kamwe. Ni kama wale wanao nunua magari halafu wanauza kwa bei ya hasara baada ya miezi michache. Nikutokuwa na mipango thabiti. Huu ujinga sijui utaisha lini.
 
sio umasikini boss ni upungufu wa elimu kuhusu Kodi zitokanazo na uingizwaji wa mizigo nchini ikiwa itapita bandarini km kituo Cha forodha!

Akijua Kuna kulipia, wharfage charges, hizo exercise fees, d/o fees na nyinginezo inategemea na mzigo unaoingia anajipanga vyema!
 
Kama umeagiza gari au bidhaa na ikawa imefika Kwenye Bandari na wakati huo pesa ya ushuru umepungukiwa,kukwama au hukuwa na taarifa sahihi za ushuru na makadirio ya kodi yamekuja zaidi ya kiwango ulichopanga njia sahihi ni kumwambia wakala wa Forodha(Clearing Agent) afanye maombi (TRA) ya kupeleka gari au mzigo kwenye Bonded Warehouse.

Bonded Warehouse ni ghala au sehemu ambayo mizigo inayosafirishwa nje au iliyotoka nje ya nchi inatunzwa inaposubiri kulipiwa ushuru.Bonded Warehouse zipo ambazo zinamilikiwa na serikali au watu binafsi zipo mikoa yenye bandari na mipakani.

Endapo umeagiza gari au bidhaa yoyote na umekwama pesa kabla au baada ya mzigo kushuka bandarini usipate pressure. Inatakiwa umwambie Clearing Agent atafute Bonded Warehouse kwa ajili ya kuweka gari au mzigo wakikubali kuna nafasi, inabidi ajaze fomu ya TRA kuomba kupeleka mzigo Bonded Warehouse baada ya kupeleka mzigo Bonded utakapo kuwa sawa utalipa kodi hata baada ya mwaka na mzigo wako utatoka.

Faida za kutumia Bonded Warehouses
1. Gharama za kutunza mzigo (storage charges) zipo Chini na zina chajiwa kwa mwezi. Mfano gari ndogo kwa mwezi bei ni usd 80, wakati bandarini kutunza kwa mwezi bei ni kubwa sana na huchajiwa kwa siku na ukubwa (CBM) unaweza ukapewa bill ya usd 1000

2.Inaondoa mzigo kuwekwa kwenye list ya overstayed good na kuja kupigwa mnada. Mzigo ukikaa sana bandarini unaingia kwenye overstayed goods na mmiliki asipo utoa unapigwa mnada. Kwenye Bonded Warehouse mzigo unaweza kutunza zaidi ya mwaka

3. Mmiliki wa mzigo ni rahisi kwenda kuangalia mzigo au gari yake ikiwa Bonded Warehouse. Gari ikiwa bandarini mmiliki hawezi kuingia kuona gari au mzigo, ila ukiweka bonded unaomba kuingia Warehouse na kuona mzigo ila huwezi kutoa. Pia akitaka auze ni rahisi kumuonyesha mteja gari au bidhaa ikiwa Bonded tofauti na ikiwa bandarini inabidi auze kwa kutumia picha za mzigo ulikopakiwa na documents za mzigo.

Bonded Warehouse ina faida kwa waagizaji wa bidhaa na magari, inaepusha mizigo kuuzwa kwa mnada. Kama ulifanikiwa kuagiza gari ya usd 3000 (CIF) bora upeleke Bonded Warehouse ukalipe usd100 per month kuliko kuiacha bandarini ukaja kupewa storage charges za usd 3500 na ushuru unakusubiri. Hapo gari inaingia kwenye mnada unaingia hasara
Asante sana kwa elimu na taarifa hii
 
Ushauri wako ni mzuri unaweza kusaidia vijana wakurupukaji kupunguza hasara.

Yaani, kwa nini uagize gari au mzigo wakati huna uhakika wa pesa ya kutolea?

Hizi ni akili za kimaskini. Mtu mwenye akili za namna hii hawezi kupata maendeleo kamwe. Ni kama wale wanao nunua magari halafu wanauza kwa bei ya hasara baada ya miezi michache. Nikutokuwa na mipango thabiti. Huu ujinga sijui utaisha lini.
Sio wakurupukaji ndio maana kuna neno EMERGENCY
 
Ushauri wako ni mzuri unaweza kusaidia vijana wakurupukaji kupunguza hasara.

Yaani, kwa nini uagize gari au mzigo wakati huna uhakika wa pesa ya kutolea?

Hizi ni akili za kimaskini. Mtu mwenye akili za namna hii hawezi kupata maendeleo kamwe. Ni kama wale wanao nunua magari halafu wanauza kwa bei ya hasara baada ya miezi michache. Nikutokuwa na mipango thabiti. Huu ujinga sijui utaisha lini.
Usikariri mkuu Kuna ups and downs unapoagiza gari inachukua mpaka miezi zaidi ya mitatu kufika bongoland kipindi hicho unaweza pata changomoto ikafanya utumie pesa uliyotegemea kulipa ushuru achana na wewe mhusika kufariki na kufaidisha mamlaka
 
Emergency zinatakiwa ziwe sehemu ya plan. Nataka kuagiza gari leo la $4000 ambayo ni sawa na 10m. Najua ushuru na malipo yote hadi litoke ni 10m. Hivyo nahitaji 20m kuhakikisha gari linafika.

Kabla sijaagiza hili gari lazima niwe na 20m kwenye account. Lakini pia lazima niangalie mzunguko wangu wa fedha. Je nina mzunguko wa kutosha kumili gari (Mafuta, service)? Je nina akiba ya emergency nikipata tatizo au gharama zikiongezeka. Haya yote ni muhimu kuyaangalia kwa kina kabla hujaagiza hiyo gari. So naweza kuji ongezea muda hadi nifikishe 25m kwenye account ndo niagize gari hilo.
 
Bonded Warehouse sio kwa gari tu, hata wale wanaoagiza bidhaa mbalimbali. Kama utaagiza na ukakwama ushuru ni bora uzitoe kwenye Container (Stripping) kisha ukashusha kwenye Bonded Warehouse zikakaa. Ukaruhusu Container irudi Kwa shipping line.

Kwenye Container ukisema ikae bandarini utapata storage charges kubwa na shipping line watakupiga fine kunwa ya kuchelewesha Container yao. Mizigo inaweza ikafanyiwa makadirio ya kodi na ukaanza kulipa kimoja kimoja na kukitoa Bonded Warehouse
 
Emergency zinatakiwa ziwe sehemu ya plan. Nataka kuagiza gari leo la $4000 ambayo ni sawa na 10m. Najua ushuru na malipo yote hadi litoke ni 10m. Hivyo nahitaji 20m kuhakikisha gari linafika.

Kabla sijaagiza hili gari lazima niwe na 20m kwenye account. Lakini pia lazima niangalie mzunguko wangu wa fedha. Je nina mzunguko wa kutosha kumili gari (Mafuta, service)? Je nina akiba ya emergency nikipata tatizo au gharama zikiongezeka. Haya yote ni muhimu kuyaangalia kwa kina kabla hujaagiza hiyo gari. So naweza kuji ongezea muda hadi nifikishe 25m kwenye account ndo niagize gari hilo.
Mkuu kuna magari na bidhaa hazipo kwenye kikokotoo cha TRA. Valuation inafanyika kwa CIF, commercial invoice na physical Valuation mzigo ukiwa bandarini. Makadirio unayopanga unakuta kodi imekuja juu.

Mizigo ya Local inapewa storage bure siku 7, hizo siku 7 zinaweza kuwa nyingi au chache.
Pale unaposubiri au kufanya process za kodi kupungua au kulipa ni bora upeleke Bonded Warehouse, baada ya siku 7 unajikuta unaingia storage mpaka mambo utapoweka sawa.
 
Lengo kuu la Bandari ni kukupa facility ya kupakia na kushusha mzigo wako, kuhifadhi hii ni ziada. Hata Waziri Makame Mbarawa mwaka 2021 nakumbuka baada ya gari kuwa zinajaa bandari ya Dar, aliongea hiki kitu na akaruhusu gari zikapaki kwenye bandari kavu za kutunza magari (ICD-Vehicles)za nje
 
Back
Top Bottom