Ukiachana na kulaani, yapi mamlaka mengine ya TLS?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,609
21,334
Kila tukio likitokea ambalo liko ndivyo sivyo, TLS inajitokeza kulaani. Latest ilikuwa ya Chadema huko Mbeya.
Wakati Mwambukusi akiomba kura alionekana akituaminisha kama TLS ni bonge ya chombo ambacho kinaweza kufanya chochote wakati wowote lakini badala yake nacho kimekuwa chombo cha kulaani kama viongozi wa dini.
Nilikuwa nataka kufahamu uwezo na mipaka ya TLS.
Wenu katika ujenzi wa taifa.
 
Kutoa recommendations tu hawa na wale CHRAGG. Commission for Human Rights and Good Governance ni moja ya vitu vya ovyo visivyo na power yoyote ile
 
Jisomee sheria ilyoanzia TLS usisubiri kila kitu utafuniwe.

Sheria ya TLS imeainisha majukumu ya msingi ya chombo hiki ni suala la wewe tu kujiongeza kujisomea mwenyewe.
 
Kutoa recommendations tu hawa na wale CHRAGG. Commission for Human Rights and Good Governance ni moja ya vitu vya ovyo visivyo na power yoyote ile
CHRAGG imeanzishwa kikatiba kabisa sema mwenyekiti na makamishna ni wateule wa Rais hivyo wanashindwa kufanya kazi zao independently.

Chombo chochote kilichoanzishwa kikatiba kina nguvu na hakiingiliwi na mamlaka yoyote in most cases lakini shida watu wanafanya kazi kwa kufuata maagizo badala ya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.
 
Kwani TLS ina polisi, magereza na mahakama? wao kazi yao kulaani na kushitaki
Sasa kama hawana yote haya si ni wanaharakati tu kama wengine!!!nao wanaingia ktk kundi la kulalamika??

Huyu paka ni kama wa kumfunga kengere amekosekana kabisa.
 
TLS ni chombo cha umma kinachotakiwa kujikita katika usimamizi wa sheria kwa kushirikiana na mahakama lakini kwa sasa imekua ni chama cha wanaharakati na siasa, sasa kwakua hawajui majukumu yao wataendelea kulaani tu.
 
Back
Top Bottom