ARCHBISHOP
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 271
- 484
UJUMBE WA WAZI KWA CLOUDS MEDIA
Binafsi niweke wazi kuwa sina tatizo na Clouds Media Group na nimekuwa mpenzi wa vipindi vya CMG kuanzia 2002.
Nakumbuka kuvutiwa na Jingle ile ya sauti ya zege "Cloooouds Fm", kipindi hicho nikiwa bado secondary miaka ya 2002 walikuwa wanapatikana kwa tabu maeneo ya Temeke. Kati ya watangazaji walionivutia wakati huo ni Dk. Sebastian Ndege, Fina Mango..na Captain Gadner, Vivian(R.I.P).
Baadae nilihamia Mwanza 2004, ambako hawakuwa na uwezo wa kurusha matangazo ya moja kwa moja hivyo walikuwa wakiunganisha matangazo kupitia kituo chao cha Mwanza kwenye jengo la Ccm, mtangazaji wao aliku Robert G. Sengo.
Baadaye nilirudi Dar na kipindi hiki CMG ilianza kubadili mwelekeo na kuwa kituo chenye ushawishi kwa vijana japo si kituo chenye nguvu juu ya IPP na SAHARA media( Huu ni ukweli usiyo hitaji ubishi).
Nimeendelea kuwa msikilizaji wao mzuri wa vipindi vya
-Power break fast( Influence ya Paul James Sweya na Fredwaa cause nawapenda sana tokea wakiwa R.F.A hawa jamaa ni vipaji+Professional)
-Leo tena( Sikifatilii sana japo nikiwa barabarani kati kati ya siku nikiwasha redio nakisikia, hawa watangazaji wake nadhani wakitoka Clouds ni Mussa Hussein pekee anaweza kupata kazi kwenye serious media nyingine mfano Azam, I.P.P, SAHARA, B.B.C..)
-XXL Hawa wana fit kwenye kipondi wanachokifanya Kenedy, Mchomvu, Mamy, B12, but gap la Fetty haliwezi kufutika.
- Jahazi Jamaa wanajitahidi kutusaidia kusukuma foleni wakati tukirudi makwetu, lakini wanajisahau sana kiukweli, wanaongea mpaka vitu vya aibu, especially Kibonde.. muda wote wanaongea ngono na pombe!!!! Pili wana brag sana maisha, ukisikia Kibonde anaongea kuhusu gari lake utafikiri anaendesha ndinga ya hatari kumbe Harrier, sijui akiendesha kama ya kipanya itakuwaje? Kiufupi hiki kipindi kinahitaji kuangaliwa upya maudhui yake na wapewe ukomo wa maneno ya kwenda hewani.
- Amplifier hua Milard Ayo 100% ndo kipindi changu bora, japo ujio wa yule binti umekupunguzia mvuto kwasababu anatumia nguvu nyingi kutaka kuwa kama Ayo. But she is ok!
- Sports Extra hawa waliwahi kuwa bora but wanaonekana walilewa sifa na kupotea au waliokuwa Smart waliondoka! Hapa namzungumzia Geofrey Lea, Ibrahim Masoud Mestro.. waliobaki akina Shaffih ni kelele na ushabiki basi.
-Ala za Roho sina cha kusema maana sipendi mtangazaji wake, na kinakuwa mida ambayo nimeshalala.
Baada ya kuyasema hayo yote niliseme jambo lifuatalo:
-Clouds media wamewekeza pesa nyingi na nguvu kazi kubwa kujenga brand yao, katika jambo hili wamefanikiwa kwa kiasi chake, Tatizo kubwa ambalo linawakumba hawa ndugu zangu nikushindwa kutenganisha "individual battles" na Taasisi. Siyo mara moja au mara mbili tumeona ugomvi kati ya watu fulani na Luge ukigeuzwa na kuwa ugomvi wa Taasisi, nakumbuka hizi:
1. Sugu+Watengwa na Ruge, pale Sugu alipotoa mawazo yake juu ya Ruge, aligeuka na kuwa adui wa Clouds media mpaka nyimbo zake kutopigwa.
2. Lady Jaydee na Ruge nayo ni kama ya Sugu, mpaka leo
3. Rubby+Rachel, hawa kwa sababu alikuwa bado hawajafika popote kimziki walifanywa watumwa na kurudi kuwapigia magoti, eti sasa nyimbo zao zinapewa Air time. Mbaya zaidi CMG wanaenda mbali kutafuta mbadala ya watu wasio wapenda kwa nguvu na kuwekeza muda mwingi kupiga nyimbo zao, kuwasifia, kuwapamba mau..., mfano ni wakati wa ugomvi wa Ruge na Rubby wakaibuka na Nandy,....
-Kubwa sasa ni tetesi zinazoendelea kuwa Ruge amegombana na Meneja wa Diamond! Cha kushangaza baada yakusikia tetesi izo nimekaa nakufanya utafiti mfupi kwa wiki mbili nakugundua hawa CLOUDS hawapigi nyimbo za WCB kwa ujumla! Siyo za Diamond, Mavoko, Harmonize, Ryvan, Lavalava au Malomboso!
Najiuliza kama vita ya individuals kwanini ihame kati ya taasisi na taasisi? WCB na CMG ni taasisi zinazojitegemea. Leo Diamond asipokuwepo Duniani WCB wanaweza wakaendelea kama kampuni hivyo hivyo kwa Ruge. Najiuliza kijinga, hivi leo WCB wamsimamishe Salam kazi, je! CMG wataanza kupiga nyimbo za WCB? na watatoa excuse gani?
Kwanini katika haya magomvi yote hayamhusishi Kusaga? Ina maana yeye siyo sehemu ya Kampuni? Mbona tunasikia yeye ndio Top? Mbona vita zote zinamzunguka Ruge? "Kyoma" unahitaji kujitazama upya, ngoma ikivuma sana upasuka!
Nashauri: CMG itenganishe individual battles na ufanisi wa Taasisi. Mnatengeneza maadui wengi kila kukicha bila sababu.
Ni mimi Msikilizaji wenu kuanzia 2002.